Omary Mjenga: Gharama za Gulf Stream kwenda Rio de Janerio Brazil ni mara 7 ya Dreamliner ya ATC

Kwani Rais aliwakilisha Afrika? Jamani Tanzania bado tuna matatizo lukuki tuachane na mikutano sio lazima kwenda huko tunaweza kutumia Tele conference, Video conference na hata Skype ikibidi ili kuokoa gharama ambazo sio za lazima jamani bado tu masikini sana. Wanafunzi darasani wanalala kwa sababu ya njaa na hata nyumbani wanaondoka bila ya kunywa chai na shuleni wazazi wanashindwa kuchangia fedha z chakula cha mchana...Inasikitisha sana
 
Mjenga ni balozi wa Tanzania Dubai licha ya kufanya kazi katika hicho chuo cha kijeshi.
 
Wanamdanganya mama na kumharibia kwa maslahi binafsi
 
Kikwete alitumia Gulsfteram kuzunguka dunia nzima, kwa hiyoi Kikwete alikuwa ni mfujaji? Kuna wakati Kikwete alikwenda Brazili na Gulfstream hiyo, baada ya kurudi nyumbani, Mama Salma alisema alikuwa bado na hamu ya kuiona Brazili; hivyo First Lady akachukua Gulfstream hiyo tena kurudi Brazili lakini safari hii kwa ajili ya "kutangaza utalii" kama kwamba alikuwa wazir wa utalii.
 
Mjenga ni balozi wa Tanzania Dubai licha ya kufanya kazi katika hicho chuo cha kijeshi.
Alikuwa balozi wa heshima huko Dubai kati ya 2013 na 2016 na wala siyo balozi wa Tanzania. Balozi wa heshima hana mamlaka yo yote ni sawa na mkuu wa kitengo wa wizara.
 
Uchawa kazi unaibadili akili kutoka kufikiri kwa kutumia kichwa hadi kutumia vikalio.
Usipokuwa chawa unakuwa na akili za kipuuzi na za kitoto kama hizi za kwako.

SSH anaifungua hii nchi kwa vitendo, hasubiri wapuuzi wa aina yako wakosoe eti ndio aonekane hafanyi kazi.

Zunguka huko mikoani uone mabadiliko makubwa sio siku nzima kujifungia nyumbani kwako.
 
JPM yeye alikuwa akisafiri anakwenda zake chato huku akaitumia muda huo kufanya ziara mabarabarani huko, ilisababisha watu wawe active na watu waliona matokeo.

Hakuna bepari atakayekusaidia kukuza uchumi wako, uchumi wako utaukuza Kwa sacrifice ya watu wako, wewe mwenyewe kiongozi mkuu na watendaji wako kufanya kazi kwa bidii na maarifa mengi huku mkiacha kutumiatumia hovyo na kuhakikisha mfumo wa elimu unakuwa Bora.
 
Mpaka muda huu ni balozi kule Dubai, usalama wa taifa huyo mzee.
Mara mwanajeshi mara usalama wa Taifa! Itoshe kusema ni mwanadiplomasia! Watu wengine hutumia neno usalama wa Taifa kutishia watu kitu ambacho ni upuuzi mtupu! Kila mwananchi ni mwana usalama wa Taifa lakini pia ana shughuli yake inayomuingizia kipato!
 
Sio kila mwananchi ni mwana usalama wa taifa tusidanganye watu humu ndani.

Sio kila mtu anazifahamu siri za nchi na mipango ya ndani ya kiulinzi na kiusalama. Ni kweli tusitishane lakini kuwa nyoka ni kazi ya wachache.
 
Sio kila mwananchi ni mwana usalama wa taifa tusidanganye watu humu ndani.

Sio kila mtu anazifahamu siri za nchi na mipango ya ndani ya kiulinzi na kiusalama. Ni kweli tusitishane lakini kuwa nyoka ni kazi ya wachache.
Matapeli wengi hujifanya usalama wa Taifa! Na hakuna mtu ambaye anafahamu siri za kila idara au kila kitu nchini! Hata Rais wa nchi hafahamu kila kitu ndani ya serikali. Usalama wa Taifa hawafahamu kila kitu kilichopo jeshini au polisi au uhamiaji au hata magereza na ndiyo sababu viongozi hupenyeza informers ambao hata wao hawapati kila kitu! Kwa hiyo hao unaowasema wewe ni waratibu tu.

Bw. Omary siyo usalama wa Taifa ila wewe unamkweza kuliko yeye binafsi alivyo! Omary ni mwanadiplomasia ingawa anaweza kutumika kama informer kama ambavyo wewe, mimi au mtu mwingine ye yote anaweza kutumika!
 
Ninamfahamu ndio maana nasema ni mtu wa usalama.
 
Meja Jenerali Mjenga ndio cheo chake. Huyo namfahamu vyema, alitaka kupangisha eneo langu hapa mbezi beach.
Sema wewe jamaa na yule choice variables huwa ni waongo waongo sana

Lini omary mjenga kawa meja jenerali? Kweli unamfahamu? Napata mashaka kama unamfahamu kweli

Meja jenerali😂😂
Uache utani aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…