MtotoKautaka
JF-Expert Member
- Jul 16, 2018
- 993
- 2,045
Wazee kuna hawa watu wanaitwa migambo (kesho la akina). Naomba niulize hivi anayemfundisha mgambo si ni mjeda? Inakuwaje hawa migambo wanakuwa na uwezo wa kutembea kichapo naweza kusema hata kuwazidi wajeda?
Mwaka 2023 nilipoenda home kutembea nilikuta kuna changamoto moja ya wizi uliokithiri.
Yani hakukaliki umeacha baiskel nje ukitoka huikuti, nguo, viatu yani tafran watu ni kuiba na kuibiwa hovyo.
Ikatokea mchungaji wa kanisa la fpct kaibiwa magunia matano ya mpunga na godoro 5×6 nyumbani kwake yani walivunja store.
Mchungaji ni kakaake na mwenyekiti wa Kijiji, mchungaji kamshawishi na kumsihi mwenyekiti achukue hatua kali na washukiwa wakamatwe. In fact wezi wote wa kijijini pale wanafahamika ila ndo hivo kukingiana vifua na kuleana leana ndo kulikuwa kunawasaidia.
Siku hiyo m/kiti kaitisha la mgambo kukawa na mkutano wa hadhara na kila mmoja alionyesha kuchoshwa na tabia mbaya za hao vijana wachache wanaosumbua kijijini kwa wizi
Yakapita maazimio kwamba walioiba wanapewa siku 2 wawe wamesharudisha Mali Kwa mmiliki. Kila mmoja kwenye mkutano ule aliafiki yale maazimio.
Siku mbili zikapita kavu hakuna kilichorudishwa. Tangazo likapita mtaani kutangaza kwamba kwanzia siku ile msako unaenda kuanza na watakaobainika wataadhibiwa vikali.
Migambo wakapewa TENDA kufanya upelelezi na mwisho wa siku baada ya kama siku 2 godoro likakamatwa Kwa kijana mmoja magetoni kwake kwasabab msako ulikuwa wa hali ya juu na kila mmoja alitakiwa kutoa ushirikiano.
Yule kijana alipelekwa ofisi za Kijiji na godoro lake kichwani, alihojiwa na kutakiwa kuwataja wenzake ila aligoma.
Migambo wakamuingiza kwenye kichomba flan ambamo wanawawekaga watu wanaokamatwa.
Tulikuwa nje tulichosikia ni kilio mwanzo tu baadae kukawa kimya na baada ya dk 10 akatolewa.
Alivotoka kwanza hatukuweza kumtambua kuwa ndo yule yule kijana yani alikuwa kubadilika sura kiasi kwamba kama angepigwa picha za before and after ukaulizwa ulinganishe usingeweza kujua kuwa ni mtu mmoja.
Yule dogo alipewa pen na karatasi aandike majina ya wahuni wenzake.
Wengine walikuwa washatoroka ila baadhi walikamatwa.
Wale vijana walipigwa Kwa muda wa kama dk 15 na baada ya hapo walibadilika sura kiasi unaweza sema walishambuliwa na nyuki.
Kila walichokuwa wameiba Kwa zile siku za karibuni including Mali za yule mchungaji vilirudi na wale vijana walikaa ndani mwezi na zaid ndo wakaonekana nje na siyo kwasabab ya aibu ila ni kichapo kutoka kwa wale migambo.
All in all, cheza kote usije cheza na migambo wale ndugu wanajua kupiga ni balaa.