Omba usishikwe na tumbo la kuharisha ukiwa katikati mjini na hakuna vyoo karibu

Omba usishikwe na tumbo la kuharisha ukiwa katikati mjini na hakuna vyoo karibu

ngoja nihadithie kidogo tunatoka arusha kwanza ile alfajiri tunaondoka pale home nikapiga chai nzito naambiwa kunywa chai kavu tu mm tena cha uroho acha ninywe mpk nimeshiba

tumepanda bus letu mchana kufika kwenye mgahawa wa dar express acha nile manyama na chips niliekua nae ananiangalia tu ananiambia sijui kama utafika salama hahahhah

kufika mlandizi tumbo silielewi kabisa linaanza kuvuruga nakiona kijasho mwenzangu ananiambia unakumbuka asbh haya ndio majibu yake na uroho wako

tumbo limechachamaa kwenda kilimanjaro bus halisimami hovyo naona najiharishia hivi

kufika kibaha bus halijakaa sana limeondoka nakumbuka nilivaa pedo ya jens ngumu kwa kweli uzalendo ulinishinda [emoji23][emoji23] watu kwenye wananishangaa mm wala ujue hata aibu huon

kufika ubungo tukashuka kuingia home moja kwa moja kuoga toka siku hiyo mm tena nimekoma na uroho wangu wa kula kula mm ni mroho
Duuh pole mkuu
 
Nakumbuka nilikuwa nasafiri kutoka Dar kuelekea Dodoma. Tulipofika Kisasa tumbo likanivuruga. Yaani nilikuwa ninatoka jasho mwili mzima, bus likitikisika kidogo mimi taaani. Ile kufika bus stand pale Dom nikatoka nduki kuelekea kwenye vyoo vya pale stand. Kufika pale pa kutolea pesa wala sikutaka kukawia wala nini nikatupa bag la laptop kwa yule anayekusanya pesa nikazama chooni ile kuinama tu huo uharo ulikuwa unatoa mlio kama tarumbeta. Baada ya kumaliza nikaenda kutoa tsh 200 yao, yule mhudumu alikufa kwa kicheko. Mimi wala sikujali nikasepa zangu.
[emoji38] [emoji38] [emoji38]
 
halaf nilisahau bada ya kuharibu hali ya hewa [emoji23][emoji23] niliekua nae kaanza kunitenga uwiiiiiii mpk tunashuka ubungo hatuongeleshani jamaan haya mambo ya uharo ya ghafla uyasikie tu kwa mwenzio

kama hivi usikie yalivyomtokea shunie
 
Hii yangu ni tofauti kidogo.

Ilikuwa ni siku ya Presentation, nipo zangu mbele kabisa natoa semina yangu mbele ya Wanafunzi wasiopungua 500.

Wakati nafika pale mbele, nikaanza kusikia hali ya tumboni inabadilika. Nikaendelea zangu kushusha madude, nafika katikati ya presentation naona kama vile nikiongea dude linashuka. Ikabidi nipunguze sauti ya kuongea, lecturer akadai niongeze sauti maana watu hawasikii. Nilipojaribu kuongeza sauti Salaleeh, naona kitu kabisa inaanza kutoka.

Nilipoona hivyo, nikanyamaza kimya kwa sekunde kadhaa huku nimeduwaa. Nikapiga mahesabu chap chap, nikasema ngoja nishuke taratibu.

Kushuka kwenyewe natembea taratibu, kama mtu ambaye mguu mmoja haujakaa sawa. Ile nafika mlangoni nikakimbia puuh! Haa, kitu kinanifata kabisa. Ikabidi nishikilie kwa mkono.

Nafika toilet, watu wamejaa. Ikanilazimu kumwaga uharo sehemu ya kukojoa. Nisingeweza kusubiri tena.

Huku Class watu wanakufa kwa vicheko wakati mwenzio naangamia.

Omba isikukute.
Hahaha! Pole sana!!!
Hiyo kitu ikukute chuo alafu ile unakimbilia chooni unakuta majangili washaharibu vyoo vyootee!!! Kudadeki... Huoni ajabu kuachia mzigo juu ya mzigo wa mwingine. I salute uharo aisee!!
 
Back
Top Bottom