inawezekana maana ya funga kwetu na kwenu ni tofauti. sisi tukifunga tunakuwa tunautafuta uso wa MUngu katika jambo fulani, hata Yesu alielekeza kwamba kuna baadhi ya mambo huwezi kuyapata hadi kwa kuomba na kufunga. na alisema tukeshe tukiomba, na zaidi ya yote mtu aliyeokoka anaongozwa na Roho Mtakatifu, haongozwi na tamaduni wala desturi.
kwa upande wako najua funga kwako maana yake ni kujinyima kula kwa kipindi fulani ili uhesabiwe haki au upate thawabu kwa sababu ya kufunga, sio kwa sababu umetafuta uso wa Mungu na kuuona. ni condition mojawapo ya kwenda ahera, wakati mimi ni condition mojawapo ya connection na Mungu hapahapa duniani. kwa sababu hiyo, sihitaji kuwekewa schedule kwenye vitabu ila nitafunga pale panapohitajika.