Ombi la kikao CHADEMA lakataliwa kutokana na tishio la Ugaidi

Ombi la kikao CHADEMA lakataliwa kutokana na tishio la Ugaidi

Hivi hao walioandaa hiyo barua wanajua madhara ya kutumia neno ugaidi kwenye barua yao katika kipindi hiki ambapo dunia ya utandawazi imekuwa kama kijiji cha ujamaa "Gezaulole", Wakati huo huo mheshimiwa raisi anahangaika dunia nzima kutafuta watalii mpaka ameenda mbali akatengeneza kitu inaitwa "Royal Tour". Wakati mwingine binadamu anapofanya mambo yasiyo ya haki Mungu naye humpiga upofu. Hivi kweli hao wandaaji wa hiyo barua wanafahamau kuwa majirani zetu ambao tunanyanganyana nao watalii wapo "smart" sana na wakiinyaka hiyo barua wataitumia vizuri sana. Nasema hivyo kwa sababu wao pamoja na kuwa na ugaidi wa kweli kweli na vivutio vichache vya utalii lakini wanatupelekesha puta sisi wenye kila aina ya vivutio vya kitalii.

Na haya mambo kadiri yanavyoendelea yakiachwa bila kukemewa na mamlaka za juu basi tutegemee siku moja tutafika kwenye mnara wa Babeli maana huyu wa juu anasema leta watalii huyu wa chini yeye analeta magaidi badala ya watalii kama alivyoagizwa wakati haviendani kabisa kama mafuta na maji. Hao walioandaa hiyo barua kwenye mpira wa miguu ndio huwa wanasema jamaa kapiga fyongo au boko tena lile baya kabisa la kujifunga wenyewe goli.
 
Sasa kipi kipya,kiongozi wa magaidi yupo Cerro naamini pia bado Kuna masalia yake,

By the way mkuu Okw hujambo ? Nina siku mingi hatukutani jukwaani
 
View attachment 2025853

Baada ya kupeleka ombi la kufanya shughuli za siasa kwa mujibu wa katiba tumeambiwa kuna tishio la ugaidi mikusanyiko haitakiwi. Tumewaandikia mapolisi watuambie magulio na minada haipo kwenye target ya magaidi? Hajajibu
Wewe wacha waendelee kuwa beep magaidi wakiamua kupiga tusisikie mayowe yao

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Kuna Jamaa mmoja humu JF (johnthebaptist) alimshutumu JJ Mnyika kukaa ofisini huku Chongolo akichanja mbuga kuimarisha chama. Atakuwa amepata majibu.
Anajua sana CCM ni Chama maiti mbele ya CHADEMA.
Chongolo na MaShaka wazunguke mpaka mwisho wa dunia, hawana uwezo wa kuipa CCM maiti uhai tena.
 
Kama wewe wanavyokubong'oresha akina Salum hapo Ufipa!
Michezo hiyo mnayo huko CCM tu kuanzia yule mwenezi wenu.
tapatalk_1570946898001.jpg
FB_IMG_1570960151009.jpg
tapatalk_jpeg_1571937092693.jpg
FB_IMG_1591963091092.jpg
FB_IMG_1603615079875.jpg
Screenshot_20210126-171647.jpg


Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Huu ugaidi unaotuwasha bado kitambo kidogo tu tutatafutana.maana naona muwasho unazidi.
 
Bila kuingia barabarani itakuwa story tu. Hata Kenya walinusana kwanza mwisho wa siku wanakaa na kuandika katiba mpya
 
Kuna Jamaa mmoja humu JF (johnthebaptist) alimshutumu JJ Mnyika kukaa ofisini huku Chongolo akichanja mbuga kuimarisha chama. Atakuwa amepata majibu.
Daaah, ila maisha haya! Mimi sielewi kabisa wanaosema huyu mama anaponya nchi huwa wanaangalia nini? Katika demokrasia JK was 100 miles away from his successors
 
Taarifa jeshi la polisi wamepewa na Nani Mana wanazidi kutuchonganisha
 
Unaoneka
Kisasi tunamuachia Mungu,kama alivyokwisha kutulipia kisasi kwa kulifyekelea mbali lile kubwa la maadui .Na wote wanaotuonea njia yao itakuwa hiyo hiyo.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
Unaonekana wazi kuwa una karoho Fulani ka kisasi! Muombe Mungu akusafishe maana akifa mtu usifurahi bali busara iongoze jazba!
 
Kamanda unachosha kwa kubandika threads zenye maudhui yale yale mitandaoni kila siku.

Ingia barabarani uandamane.
Ukitaka usisome mambo yale yale kila siku, basi jitoe kwenye mitandao ya kijamii hasa hii ambayo watu wako huru kutoa maoni yao. Kuna mitandao mingi ambayo inamilikiwa na watu wa ccm na serikali kwa ajili ya kusifia kila kitu, jiunge huko.
 
Nani asiye na habari ya mizunguko ya akina Chongolo au Shaka nchi nzima, wakikusanyika na kufanya siasa bila kubughudhiwa?

View attachment 2025817

Vipi hii kuwahusu hawa wengine?

View attachment 2025819

Bado Rais Samia na serikali nzima wangependa kuaminika kuwa haki na usawa ni agenda zao pia?
Chongolo ni chama tawala, yuko kazini. Anasimamia serkali kuhakikisha inatekeleza Ilani zake. Angeweza kuwaita mmoja mmoja au makundi makundi waje Lumbumba Street kujieleza lakini uchungu wa kazi na uzalendo zimemwongoza aende mwenyewe asingoje ya kuambiwa. This has nothing to do with kongamano or mbowesiyogaidi au tumehuru: hii ni kazi.
 
Chongolo ni chama tawala, yuko kazini. Anasimamia serkali kuhakikisha inatekeleza Ilani zake. Angeweza kuwaita mmoja mmoja au makundi makundi waje Lumbumba Street kujieleza lakini uchungu wa kazi na uzalendo zimemwongoza aende mwenyewe asingoje ya kuambiwa. This has nothing to do with kongamano or mbowesiyogaidi au tumehuru: hii ni kazi.

Kama unadhani hujayasahau maneno haya: "kwa maoni yangu ..." kabla ya kuanza kuandika lolote, wahi mirembe mjomba.

Kumbuka huko ni kama mhimbili tu ambako vigogo haswa wametajwa kuwa na mafaili huko.
 
Back
Top Bottom