Ombi la kuteuliwa kuwa Kamishna wa Petroli na Gesi

Halfa ya teuzi tutakutana Pale Richie Richie Inn.

Ukiwa Vwawa jitahidi uwe unapata wasaa unaonana na wakina Mzee Zambi(Mbunge Mstaafu) ni watu poa na wanaweza kukuonyesha njia za kupita au kubadilishana magazine.
Mzee Zambi nilimpigia kampeni sana. Bibi mkubwa alisoma naye na ndiye alikua kampeni meneja wake. Nilijikuta kupitia bibi mkubwa tunampigia kampeni Mzee Zambi. Mzee Zambi ukimwuuliza Matrida Dulle anamfahamu vizuri.
 
Napita maana sijui kwa nini kamishna katenguliwa kama kuna anajua atujuze. Ila kabla sijaishia nikuulize wewe unayeomba kazi hiyo kwa nini nchi isifufue au kujenga upya kiwanda cha refinery. Halafu kwa nini mpango wa kutumia gesi yetu asili kwa matumizi ya nyumbani na kuuza nje unasuasua utekelezaji wake. Kwani haiwezekani kudambaza gesi hoyo kwa mitungi kama hizi za LPG.
 
Kufufua kiwanda cha kuchakata mafuta ghafi ya petroli (petroleum refinery) na kukuza matumizi ya gesi asilia kwa matumizi ya ndani na kuuza nje ni mambo muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu.

Kwanza, kiwanda cha kuchakata mafuta ghafi ya petroli kingeweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika uzalishaji wa bidhaa za mafuta (dizeli, petroli, mafuta ya ndege, vilainishi) kupunguza gharama za kuagiza nje, na kutoa fursa za ajira kwa watanzania.

Kuhusu matumizi ya gesi asilia, kuongeza matumizi ya gesi majumbani kunaweza kuwa na manufaa kwa kuwa ni nishati safi na endelevu. Hata hivyo, kufanikisha hilo kunahitaji mikakati thabiti ya kuboresha miundombinu, kutoa elimu kwa umma, na kuvutia uwekezaji katika sekta hiyo. Pia, kuimarisha uuzaji wa gesi nje kunahitaji mikataba bora, miundombinu ya usafirishaji, na ufanisi wa kusimamia rasilmali hiyo.

Katika nafasi hii, nitajitahidi kuleta mabadiliko chanya na kuweka mikakati madhubuti ili kufufua kiwanda cha kuchakata mafuta ghafi ya petroli (petroleum refinery) na kukuza matumizi ya gesi asilia kwa manufaa ya wananchi na uchumi wa nchi.
 
Kabla ya kuomba kazi hakikisha kwanza unafanya research ya role and responsibility ya nafasi unayoomba na kuonyesha walau transferable skills za nafasi unayoomba kama huna first hand experience.

EWURA ni market regulator wa energy, hana uhusiano wowote na uzalishaji wa umeme, gas wala maji zaidi ya kutunga kanuni za soko na kusimamia au kusimamia sheria za soko kutoka bungeni.



Majukumu ya EWURA it has nothing to do na andika lako hata moja.




Ufahamu hata EWURA mkurugenzi wa mafuta na mkurugenzi wa gas ni watu wawili tofauti (ni regulators tu). Let alone PURA ndio ina majukumu ya upstream na midstream kwenye ‘oil and gas’; whereas TPDC ndio wana role ya downstream.

Halafu mkitoka hapo private ikijaza wageni ohoo, sisi tuna wasomi wa hayo maswala lakini tuna kuwa overlooked.

Uwezi hata kujiuza mwajiri nani atakupa kazi private if you haven’t even researched the role. Halafu unatangaza una biashara ya kuwaandikia watu CV wakati wewe mwenyewe sidhani kama unaweza jiandikia yako.
 
Ombi lako ni gumu sana kueleweka maana kusoma na kufanyia kazi ni vitu viwili tofauti! Unaweza kusoma lakini kutumia elimu kwa manufaa mapana ya umma ni mtihani mwingine na wasomi wengi kufanyia kazi taaluma waliyosomea ni mtihani mkubwa zaidi zimebaki nadharia tu!! Kupewa Mamlaka kwa Wasomi wetu ni mtihani mwingine mkubwa zaidi! Ushauri wangu omba ukafanye kazi hapo ili uone nadharia ulizonazo zinafanya kazi!! Maana mengi uliyonayo ni nadharia!! Hujawahi fanya kazi kwenye nchi za Kiafrika zenye changamoto nyingi za Mabeberu wa Kimagharibi na Mashariki!! Hujawahi jua changamoto iliyopo kwenye kazi hiyo ya usimamizi ukizingatia wanaofanya biashara hizo walishaondoka siku nyingi kupigania mlo wa siku na kupunguziwa nauli!! Hivyo omba upatiwe hata ajira na Kisha utembelee nyingi za Kiafrika zenye mafuta na gesi ndipo uone unastahili kuomba hiyo nafasi au kuwa mbali nayo kama mbingu na ardhi ikiwa nia ya kutumikia umma wa Watanzania na sio kupigania maisha binafsi!!
 
Kwanza nikupongeze kwa kuandika mambo mengi yenye umuhimu mkubwa katika sekta yetu ya mafuta na gesi katika taifa letu.

Hayo yote uliyo yaandika wala sio majukumu magumu na kutisha mpaka uanze kuogopa kutekeleza majukumu utakayo pangiwa pindi unapoteuliwa. Na wala kwenye hizo taasisi ulizoorodhesha yaani TPDC, EWURA, na PURA hakuna majukumu magumu ya kutisha mpaka uanze kuogopa mkuu wangu. Jiamini kila kazi inakua na kanuni na taratibu acha kuogopa.

Sio kila kazi unayopangiwa kuifanya huwa unakua ulisha ifanya kabla. Nazungumzia kazi ya kuteuliwa. Jambo lakukushauri kuwa mwepesi wa kujifunza, jishushe na kufuata kanuni na taratibu zinazo zunguka kazi yako mpya. Jivunie ubunifu sio majukumu ya kazi uliyokariri kabla.

Hivyo ndugu yangu swala la kusema kwamba ili ufanye kazi fulani lazima uwe uliifanya hiyo kazi kabla sio mtazamo mzuri. Yaani kwamba ili uwe makamu wa Rais lazima uwe ulishawahi kuwa makamu wa Rais.

Mwisho kabisa mimi nipo tayari kuifanya kazi hiyo kama endapo nitateuliwa. Nitafuata kanuni na taratibu za kazi hiyo ili nitimize majukumu yangu kama yalivyo ainishwa kwenye sheria ya petroli.
 
Nashukuru kwa maoni yako na ufahamu wako mzuri kuhusu changamoto za kufanya kazi katika nafasi za usimamizi, hasa katika mazingira ya Kiafrika na katika sekta ya mafuta na gesi. Ninaelewa umuhimu wa kufanya kazi halisi na kuona jinsi nadharia inavyoweza kutumika katika muktadha wa vitendo.

Kupata uzoefu wa moja kwa moja katika mazingira hayo ni muhimu, na ninaamini kuwa kujifunza kutokana na uzoefu wa kazi ni njia bora ya kuboresha na kutekeleza elimu na maarifa ya nadharia.

Ninaichukua ushauri wako kwa uzito na nitajitahidi kutafuta fursa za kupata uzoefu wa kufanya kazi katika mazingira tofauti ikiwemo na nafasi hii niliyo omba kuteuliwa.

Kuelewa umuhimu wa nafasi hiyo niliyoomba katika kutoa mchango wa kudumu na wa maana kwa umma wa Watanzania ni kipaumbele changu. Asante kwa mwongozo wako na kushirikisha maoni yako kwa uwazi katika jukwaa hili.

Lakini naomba nikutoe wasiwasi kwamba nina imani kubwa katika uwezo wangu wa kubeba majukumu ya nafasi hiyo na kutoa mchango wangu kwa ufanisi.

Uzoefu wangu katika kujifunza na kutatua changamoto, pamoja na uwezo wangu wa kubuni na kutekeleza mikakati madhubuti, ni rasilimali ambazo ninaamini zitachangia katika kufanikisha majukumu ya nafasi hiyo.

Nina hamu ya kujifunza zaidi, kufanya kazi kwa karibu na wenzangu, na kutoa mchango wangu kwa maendeleo ya sekta ya mafuta na gesi nchini. Nitajitahidi kwa juhudi na nidhamu kufikia malengo yaliyowekwa na kuleta mabadiliko chanya.

Ninaamini kuwa naweza kuimudu nafasi hiyo kwa ufanisi na kuchangia katika kuendeleza rasilimali za nishati kwa manufaa ya taifa letu.

Ahsante
 
Kwa hiyo unaenda kujifunza kazi at senior management position.

Kama tunaokota makatibu wakuu nje ya senior civil servants wa wizara (wakati hizo ni very sensitive posts) kwanini ishindikane mtu yeyote kushika nafasi za mashirika bila ya uwezo.

Matter of fact January Makamba kila siku alikuwa anapeleka rafiki zake wasio na skills wala knowledge za sector kushika nafasi. Why not you walau una basics za oil and gas.

Swali kwako how much is storage capacity ya mafuta kwa sasa Tanzania na sera za inventory control ya nchi inasemaje kuhusu minimum reserves.

Wapi tunanunua mafuta kwa wingi, supply risks zilizopo na mitigation strategy unayopendekeza kuhakikisha nchi aina uhaba watu wakianza kuparurana huko kwenye vyanzo vya mafuta. Mambo unayoandika na nafasi unayoomba ni vitu viwili tofauti.
 
Nimwomba aniteue niwe waziri wa fedha tangu anaapishwa lakini bado hajanijibu. Nakutakia kila la kheri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…