Ombi la kuteuliwa kuwa Kamishna wa Petroli na Gesi

Weka namba yako ya simu tuangalie jinsi ya kukusaidia.
 
Mimi nimeongea na mama akaniambia anahitaji namba ya mtuma maombi
 
Hii nchi tutafika kwa Mungu tumedhoofika
 
Uvccm mwenzako huyo
 
Mkuu maneno yako makali ngoja nijaribu kuwa hivyo.
Huo ndio uhalisia mzee, chunguza aina ya viongozi wetu, yupi unasema yes huyu timamu kabisa, ana mipango swaafi kichwani, akili zinachaji.
Utashangaa wanatangaza nafasi za ajira kumbe ni ualimu na udaktari tu ๐Ÿ˜‚
 
Hii nchi tutafika kwa Mungu tumedhoofika
Mkuu biblia katika kitabu cha ufunuo inasema mbinguni hakitaingia kinyonge.

Ufunuo wa Yohana 21:27
Na ndani yake hakitaingia kamwe cho chote kilicho kinyonge.
Bado bibilia ikagongelea msumari kwenye kitabu cha Mathayo

Mathayo 11:12
Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.

Kama huna nguvu huwezi kuuteka ufalme wowote duniani.

Kitu kinyonge sikuzote ni kitu kisichokuwa na nguvu ya kustahimili mtikisiko fulani aidha mapigano, ugonjwa, Dhoruba, mateso n.k.
 
Watu wenye qualifications kama zako wako wengi hapa Tanzania na nafasi ya kamishna ni moja, what is special about you mpaka upewe wewe?

Mali kubwa kwa sasa ni uzoefu na ni kitu naona hauna. Unaweza kubeza suala la uzoefu lakini siku ukija kuingia kazini utaona tofauti ya experienced people and inexperienced ones kwenye utendaji.

All in all, malizia masomo kwanza then jijengee uzoefu wa wa atleast five years with atleast two in management ndio ufikirie nafasi ya ukamishana. Otherwise wapo wengi waliokuzidi sifa.
 
Ahsante sana kwa mchango wako mzuri mkuu wangu. Ni kweli hata mimi natambua umuhimu wa kuwa na uzoefu kazini. Uzoefu ni jambo la muhimu sana katika kazi. Uzoefu unaongeza ufanisi katika kazi. Lakini kuwa na uzoefu kwa wengine kisiwe kigezo cha kusema wengine hawana uzoefu. Na tambua mahali pakuupatia uzoefu ni kazini na kazi zenyewe ndio kama hizo.

Lakini tukirudi kwenye katiba yetu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Kuna kifungu chochote kwenye katiba kimesema ili mtu apewe hiyo nafasi lazima awe na uzoefu wa hiyo kazi??

Mimi nafikiri sisi kama taifa huru tujitahidi sana kufuata haki katika kuajiri na kuteua. Tunaposema hana experience sasa tunataka mtu huyo aipatie wapi hiyo experience. Mtu anaweza kuwa na experience lakini kuna sifa zingine hana.
 
Ni kweli hakuna sheria inayozuia mamlaka za uteuzi kukuajiri na nina amini kama mtanzania una haki ya kuajiriwa na serikali.
Ila huoni kama ni sahihi zaidi kabla ya uteuzi wa mtu kushika nafasi za juu serikalini washindanishwe watanzania wenye nia na vigezo na yule mwenye kuwazidi wengine ndiye apewe nafasi hiyo? Je, unadhani wewe una vigezo vya kuwashinda watanzania wote wenye nia ya kushika hiyo nafasi kama wewe?

Kuhusu uzoefu unadhani ni sahihi mtu kwenda kujifunza kazi kwenye nafasi ya juu serikalini (ambayo maamuzi yake yana repurcussions kubwa kwa stability na uchumi wa nchi) wakati zipo nafasi za chini zipo (ambazo maamuzi yake yana madhara madogo hivyo makosa yanavumilika wakati mtu anajifunza)? Unadhani ni sahihi mtu asiye na uzoefu wa kazi akaenda kuajiriwa nafasi ya juu serikalini hali ya kuwa anaoenda kuwaongoza wanamzidi elimu na uzoefu wa hiyo kazi (unaenda kusimamia watu ambao ndio watakufundisha kazi)?

Mimi naona haya mambo huwa yanafanyika kwa nepotism tu ila kama una nia njema na nchi yetu kama unavyojinasibu, basi jijengee uwezo kwanza. Najua vijana tuna haraka ya kutimiza malengo yetu ila ukweli ni kwamba mambo mazuri yanataka subira.
 
Hizi, njaa hizi, hizo, nafasi wanapewa watu waliofsnya makubwa kwenye industry zao, sasa wewe hufahamiki, zaidi ya, kuwa mwandishi, tu hapa JF, ukiona unajipigia debe, wewe hufahi,nafasi kama hizo, watu hupendekezwa, hutafutwa, sasa, wewe unajipendekeza,
Kwanini wakupe wewe, na sio mmoja wa wafanyabiashara wa mafuta kama Shabiby nk,?
 
Mkuu wangu najua unauheshimu sana uzoefu lakini nakuhakikishia kwamba kila kazi ina kanuni na taratibu zake.

Ukiwa mwerevu unaweza kufanya kazi yoyote kwa kufuata kanuni na taratibu za kazi hiyo.

Hivyo mkuu wangu ondoa uoga jiamini na nakuhakikishia mkuu wangu uzalendo unaweza kuwa ni zaidi ya uzoefu unaouzungumzia.

Weka KANUNI NA TARATIBU ZA KAZI ndio uwe mwongozo wako wa kufanya kazi.
 
Ni kweli mkuu wangu tuna njaa sana ya kuwatumikia watanzania wenzetu ili kusukuma gurudumu la maendeleo ya nchi yetu. Tuna kiu kubwa ya kuleta maendeleo katika taifa letu.

Usiogope mkuu wangu jiamini kila jambo linawezekana ukisema unaweza usiogope. Shika kitu hichohicho ulichonacho mkononi sema naweza songa mbele.
 
Weka namba ya simu na email address.
 
Haya mkuu. Nikutakie kila la kheri katika kazi yako hiyo.
 
Mkuu kwanza hongera kwa kuandika jambo ambalo unalifahamu. Lakini mimi sina hakika kama CCM huchukua watu wasio na uwezo.

Kwa ninavyojua ili CCM wakuamini kuwa miongoni mwa viongozi wa serikali yao lazima uwe na kitu cha tofauti. Nikiwaangalia viongozi wote waliopata uongozi kwenye serikali ya CCM wanasifa ambazo pengine watanzania waliowengi wamezikosa.

Mtu mwenye akili ni yule tu mwenye uwezo wa kumtawala mwingine. Viongozi wa CCM wanakuongoza kwasababu wamekuzidi akili.

Hivyo ndugu yangu viongozi hao unaowasema bado wanatumia akili zao vilevile ndio maana wanatuongoza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ