Ombi la kuteuliwa kuwa Kamishna wa Petroli na Gesi

Mkuu asante sana kwa maneno ya baraka. Umenipa kani moja kubwa sana ya msukumo. Sisi kama vijana jamani hatuna haja ya kuogopaogopa na kujificha bali tuendelee kupambana mpaka mwisho katika kutumia kile kidogo tulicho nacho.

Kikubwa msamiati kujiamini uendelee kulindima ndani ya mioyo yetu ili tujawe na nguvu za kuweza kukileta kwa jamii kile tulichonacho bila kuchoka.

Mimi huwa naamini kwamba ukikuta mtu ni kiongozi anakuongoza ujue amekuzidi vingi na ndio maana anakutawala na kukuongoza. Kuna jambo la ziada alilifanya lililomwongezea pushing force ya kufika hapo kwenye uongozi ambapo mwingine hawezi kufika kwasababu ya kukosa hiyo pushing force.

Hivyo sisi kama vijana tuna kazi ya ziada ya kufanya ikiwemo na kuondoa uoga ili tuweze kufika hapo walipofika wengine kwa maana walitumia kanuni hiyohiyo kufika hapo walipofika.

Tusijali vikwazo vyovyote tuweke uzalendo mbele ili tupate kuwatumikia watanzania wenzetu.
 
Aisee
wewe sio Mtanzania..
Haya ni majibu ya usaili wa mkuu wa BP kimataifa.....
Hebu tupe details za utaifa wako tuanze kurekebisha mambo uhamiaji
 
Aisee
wewe sio Mtanzania..
Haya ni majibu ya usaili wa mkuu wa BP kimataifa.....
Hebu tupe details za utaifa wako tuanze kurekebisha mambo uhamiaji
Mkuu wangu ondoa shaka kabisa juu ya uraia wangu. Mimi ni mtanzania mwenzako mzalendo mwenye kiu kubwa ya kuungana na watanzania wenzangu katika sekta ya mafuta na gesi na serikali yetu ya Jamuhuri ya Muungano kwa ujumla ili kuongeza nguvu ya kuwaletea maendeleo watanzania wenzetu katika sekta yetu ya nishati hasahasa katika upande wa mafuta na gesi.
 
Shida ya waswahili ni kwamba hata awe mtu mzuri huku nje, akishafika mule ndani akaonjeshwa asali, maandiko yote yale mazuri hayafanyii kazi tena. siunamkumbuka Yuda?
Mkuu wangu ni kweli kabisa lakini yote hayo yanasababishwa na ukosefu wa uzalendo. Lakini nakuhakikishia wapo vijana wazalendo ambao hawawezi kuyumbishwa katika misimamo yao. Mkuu wangu mimi ni kijana mwenye uzalendo wa kweli. Nacho angalia ni kutekeleza majukumu yangu ili kuwaletea maendeleo ndugu zangu watanzania.
 
Mbona hujaweka CV yako mkuu.Ili sisi tunaomshauri Boss,angalao tuone academic qualifications zako.Isije ikawa High School ulisoma combi ya HKL,na Varsity ukasoma BA in History,Halafu unataka kuwa MD wa Petrol & Gas !
 
Hakika una stahili katka nyuzi zako zote hzo Basi mama akuone una kitu unakijuwa kwenye nishati na gesi

Kila kheri manager wa makampuni
 
Kuna watanzania wan upeo mkubwa sna wewe Ni mmoja wapo
 
Mbona hujaweka CV yako mkuu.Ili sisi tunaomshauri Boss,angalao tuone academic qualifications zako.Isije ikawa High School ulisoma combi ya HKL,na Varsity ukasoma BA in History,Halafu unataka kuwa MD wa Petrol & Gas !
Mkuu wangu kuhusu elimu wala usijali nitaweka. Niliepuka kuweka elimu yangu kwasababu wenye elimu kama yangu ni wengi kidogo. Nikaona ngoja mimi nikomae na sifa yangu ya uzalendo, kiu na kile nilichobeba kichwani ili kuwatumikia watanzania. Ndio hicho nilichokileta hapa jukwani mkuu wangu.
 
Hongera kwa andiko zuri, ningekuunganisha na mtu muhimu ambaye angekusaidia kupata nafasi nyingine kwenye taasisi hiyo hiyo ila sio nafasi uliyoandika hapo.

Bahati mbaya nimepitia CV yako naona bado upo shule unapambana na phD, mwisho kabisa kwa umri wako nakuona ukifika mbali miaka ya mbeleni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…