Ombi la kuteuliwa kuwa Kamishna wa Petroli na Gesi

Ombi la kuteuliwa kuwa Kamishna wa Petroli na Gesi

Meneja Wa Makampuni mkuu kwa hizo thread hapo itoshe kusoma upo na ufahamu wa nini unachokiomba na kama ulivyotanabisha hapo umesema CV zipo.

Wengi wamejaa chuki, na wivu endelea kupambana mkuu Wapo viongozi wengi wanapita hapa jukwaani utakuwa upo exposed kwa kiasi fulani.

Hongera kwa uthubutu huu.
Mkuu asante sana kwa maneno ya baraka. Umenipa kani moja kubwa sana ya msukumo. Sisi kama vijana jamani hatuna haja ya kuogopaogopa na kujificha bali tuendelee kupambana mpaka mwisho katika kutumia kile kidogo tulicho nacho.

Kikubwa msamiati kujiamini uendelee kulindima ndani ya mioyo yetu ili tujawe na nguvu za kuweza kukileta kwa jamii kile tulichonacho bila kuchoka.

Mimi huwa naamini kwamba ukikuta mtu ni kiongozi anakuongoza ujue amekuzidi vingi na ndio maana anakutawala na kukuongoza. Kuna jambo la ziada alilifanya lililomwongezea pushing force ya kufika hapo kwenye uongozi ambapo mwingine hawezi kufika kwasababu ya kukosa hiyo pushing force.

Hivyo sisi kama vijana tuna kazi ya ziada ya kufanya ikiwemo na kuondoa uoga ili tuweze kufika hapo walipofika wengine kwa maana walitumia kanuni hiyohiyo kufika hapo walipofika.

Tusijali vikwazo vyovyote tuweke uzalendo mbele ili tupate kuwatumikia watanzania wenzetu.
 
Bila shaka kama nilivyo eleza kwa kina kwamba kila kazi ina kanuni na taratibu zake. Ukifuata kanuni na taratibu za kazi hakika unaweza kuifanya kazi yoyote. Tusifanye kazi kwa kukariri bali tufuate kanuni na taratibu za kazi hiyo. Kufanya kazi kwasababu ulisha ikariri kunajenga mazoea kazini na kupunguza ufanisi.

Kuhusu makatibu wa wizara sina hakika na ulicho kiandika ninachojua makatibu wote wanateuliwa kwa kufuata katiba ya nchi yetu. Sidhani kama katiba imesema ili kumteua katibu lazima awe ni senior civil servant wa wizara hiyo. Katiba haisemi hivyo, tulishakubaliana kuteua kwa utaratibu unaotumika kila siku. Ukitaka wateuliwe kama hivyo unavyotaka badilisha katiba. Lakini kwasasa uteuzi unafuata misingi ya katiba tuliyo nayo. Na teuzi zote za wakurugenzi wa mashirika na makamishina unafuata katiba ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania.

Kuhusu January Makamba kwamba alikua anapeleka marafiki zake mimi kwa uelewa wangu sina hakika. Bado nipo palepale kwenye mwongozo wa taifa letu katiba. Alikua anafanya hayo kwa kuzingatia katiba kama kulikua hakuna kifungu chochote cha katiba kilichokuwa kinamzuia kufanya hivyo sidhani kama ni makosa. Katika hili kila kitu kinafanyika kwa kufuata katiba. Kama katiba haijasema kwamba mteuliwa lazima awe na basics za oil na gas basi mtu yeyote anaweza kushika nafasi hiyo. Kama sio hivyo basi itengenezwe katiba mpya itakayofuata hayo unayo yahitaji.

Kuhusu uhifadhi wa mafuta, tunayo kampuni inayofanya kazi ya kuhifadhi mafuta yanayo ingizwa nchini inaitwa TIPER ni ubia wa asilimia 50 kwa 50 kati ya serikali yetu ya Tanzania na kampuni ya Oryx Energies. Hivyo taarifa zote za uwezo wake wa kuhifadhi mafuta tunazipata katika kampuni hiyo ya TIPER wala hatuhitaji kukariri ni kufuata kanuni na taratibu za kazi. Ukienda TIPER wanakupatia taarifa zote unazohitaji. Tovuti ya TIPER Tiper Tanzania Ltd.. Unapokua umeteuliwa unapaswa kujua mahali pakuzipata taarifa unazohitaji. Na tena unahitaji real time information. Unaweza ukasema TIPER wanauwezo wa kuhifadhi lita millioni 255 za mafuta kumbe jana wameongeza matanki mengine ya mafuta.

Lakini nitakuchambulia walau kidogo juu ya uwezo wa kuhifadhi mafuta katika taifa letu kwa faida ya jukwaa hili.

Taifa letu kupitia kampuni yetu la TIPER linauwwzo wa kuhifadhi mita za ujazo 255,000 za mafuta. Katika hizo mita za ujazo 180,000 ni za Automotive Gas Oil (AGO), mita za ujazo 56,000 ni za Motor Gasoline (MOGAS), mita za ujazo 9,000 ni za Dual Purpose Kerosine (DPK) na mita za ujazo 10,000 ni za Fuel Oil/Heavy Fuel Oil/ Industrial Diesel Oil (FO/HFO/IDO).

Sera za inventory control za nchi zinaweza kutofautiana kutokana na ongezeko la idadi ya watumiaji wa mafuta kutokana na ongezeko la idadi ya vyombo vya moto. Lakini mara nyingi zinajumuisha kuweka akiba ya chini (minimum reserves) ili kuhakikisha usalama wa usambazaji na kuepuka upungufu wa haraka wa bidhaa za mafuta. Lakini kama nilivyo kueleza tangu mwanzo data zote hizi zipo documented kwenye vitabu vya kanuni na taratibu. Hivyo hutakiwi kukariri fuata kanuni na taratibu ili kuelewa sera za uhifadhi wa mafuta na akiba ya chini za kipindi hicho cha uongozi wako. Kama mtumishi mpya kazini ni vyema kutafuta taarifa za hivi karibuni kutoka kwa vyanzo rasmi vya serikali au mamlaka husika ya nishati katika kipindi chako.

Lakini kwa faida ya wengi katika jukwaa hili kulingana na uwezo wetu wa kuhifadhi mafuta nchini, sheria inahitaji uwepo wa hifadhi ya mafuta inayotosheleza angalau kwa siku 15. Lakini kwa uelewa wangu namba hiyo inaweza kubadilika huko mbeleni endapo kama watumiaji wa mafuta wataongezeka. Nikiwa na maana kama vyombo vya moto vitaongezeka.

Kuhusu kununua mafuta utaratibu ni uleule wa manunuzi wa kufuata kanuni na taratibu. Tanzania inaweza kununua mafuta kwa wingi kupitia mikataba ya moja kwa moja na kampuni za kimataifa au kupitia mnada wa kimataifa wa mafuta.

Hata hivyo, changamoto za usambazaji zinaweza kutokea kutokana na mabadiliko ya bei duniani, migogoro ya kisiasa katika maeneo ya uzalishaji, au matatizo ya usafirishaji.

Njia ya kupunguza hatari za usambazaji ni kujenga mkakati thabiti wa kuhifadhi akiba ya mafuta, kukuza vyanzo vingine vya nishati, na kushirikiana na nchi nyingine kwenye mikataba ya muda mrefu ili kuhakikisha uthabiti wa usambazaji. Pia, kuwekeza katika miundombinu ya usafirishaji na kuhimiza uzalishaji wa ndani wa nishati kunaweza kuwa njia muhimu za kupunguza hatari za usambazaji wa mafuta.
Aisee
wewe sio Mtanzania..
Haya ni majibu ya usaili wa mkuu wa BP kimataifa.....
Hebu tupe details za utaifa wako tuanze kurekebisha mambo uhamiaji
 
Aisee
wewe sio Mtanzania..
Haya ni majibu ya usaili wa mkuu wa BP kimataifa.....
Hebu tupe details za utaifa wako tuanze kurekebisha mambo uhamiaji
Mkuu wangu ondoa shaka kabisa juu ya uraia wangu. Mimi ni mtanzania mwenzako mzalendo mwenye kiu kubwa ya kuungana na watanzania wenzangu katika sekta ya mafuta na gesi na serikali yetu ya Jamuhuri ya Muungano kwa ujumla ili kuongeza nguvu ya kuwaletea maendeleo watanzania wenzetu katika sekta yetu ya nishati hasahasa katika upande wa mafuta na gesi.
 
Shida ya waswahili ni kwamba hata awe mtu mzuri huku nje, akishafika mule ndani akaonjeshwa asali, maandiko yote yale mazuri hayafanyii kazi tena. siunamkumbuka Yuda?
Mkuu wangu ni kweli kabisa lakini yote hayo yanasababishwa na ukosefu wa uzalendo. Lakini nakuhakikishia wapo vijana wazalendo ambao hawawezi kuyumbishwa katika misimamo yao. Mkuu wangu mimi ni kijana mwenye uzalendo wa kweli. Nacho angalia ni kutekeleza majukumu yangu ili kuwaletea maendeleo ndugu zangu watanzania.
 
Mbona hujaweka CV yako mkuu.Ili sisi tunaomshauri Boss,angalao tuone academic qualifications zako.Isije ikawa High School ulisoma combi ya HKL,na Varsity ukasoma BA in History,Halafu unataka kuwa MD wa Petrol & Gas !
 
OMBI LA KUTEULIWA KUWA KAMISHNA WA PETROLI NA GESI

Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan,

Kwa heshima na taadhima, naomba kuteuliwa kuwa Kamishna wa Petroli na Gesi katika Wizara ya Nishati, ili kujaza nafasi iliyo wazi.

Nikiwa na uelewa mkubwa katika masuala ya mafuta na gesi, na kufahamu umuhimu wa nafasi hii, nina imani kuwa ninaweza kuleta mchango mkubwa kwa maendeleo ya sekta hii muhimu.

Nipo tayari kufanya kazi kwa bidii na ufanisi ili kusimamia rasilimali hizi kwa manufaa ya taifa letu.

Ninapenda kutumia fursa hii kusema kwamba nipo tayari kuchukua jukumu hili kwa uaminifu, nidhamu, na dhamira ya hali ya juu.

Naamini ninaweza kufanya kazi kwa kushirikiano kwa lengo la kuleta maendeleo na ustawi wa nchi yetu.

Asante sana.

Rejea za maandiko yanayo onyesha kiu ya kuchochea maendeleo katika sekta ya mafuta na gesi Tanzania.

1. Kuongeza Ufanisi na Kukuza Sekta ya Mafuta na Gesi Tanzania: Mapendekezo ya Kuanzisha Wizara ya Mafuta na Gesi

2. Kwanini hatuna Wizara ya mafuta na gesi kama mataifa mengine yenye gesi na mafuta

3. Tuunganishe nguvu tuwavutie wawekezaji kwenye haya maeneo ya mafuta na gesi tusiichie serikali pekee inatingwa

4. Vituo vya kujaza CNG kwenye magari vinavyotembea vitasaidia kujaza CNG kwenye magari kwenye mikoa mbalimbali

5. Kukabiliana na Changamoto za Upungufu wa Dola na Kuongezeka kwa Bei za Mafuta serikali ifanye mambo yafuatayo

6. Watalaam wa mafuta na gesi Tanzania waishauri serikali juu ya ongezeko la bei za mbolea, mafuta ya petroli na dizeli nchini

7. Ni hatari sana bei ya mafuta ya taa ikiwa chini sana kuliko bei ya petroli na dizeli

8. Siasa za Gesi na Mafuta Tanzania: Uhusiano wa Gesi Asilia inayozalishwa Tanzania na sekta nyingine za kimkakati.

9. Tujenge kiwanda cha kuibadili gesi asilia kuwa petroli na dizeli

10. Siasa za Gesi na Mafuta Tanzania: Uhusiano wa Gesi Asilia inayozalishwa Tanzania na sekta nyingine za kimkakati.

11. Siasa za Mafuta na Gesi: Uzberkistan inaanza kuibadili gesi asilia kuwa petroli, dizeli, mafuta ya ndege, mafuta ya taa, na gesi ya LPG

12. Tuache kudanganyana hakuna gesi iliyowahi kuuzwa na kusafirishwa kwa bomba kwenda nje ya Tanzania

13. Maeneo muhimu ambayo wataalamu wa Serikali wanapaswa kuzingatia wakati wa mazungumzo zidi makampuni ya mafuta na gesi

14. Maeneo muhimu ambayo serikali zetu zinapaswa kuzingatia wakati wa mazungumzo yao na makampuni ya mafuta ya mafuta na gesi

15. Serikali kuja na kifurushi cha gesi ya kupikia cha Sh 500 au 1,000 ili Mtanzania anunue gesi badala ya mkaa na kuni

16. Gesi Asilia Iliyoshindiliwa (CNG) Ndiyo Mwarobaini wa Bei ya Mafuta Tanzania

17. Kukokotoa punguzo la bei ya mafuta ya petroli na dizeli kwa mwezi wa sita 2022 baada ya kuongezewa ruzuku ya billioni 100 (100B)

18. Mchanganuo wa bei za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa Mei 2022

19. Kama ulikuwa hujui hii ndio mikataba ya Utafutaji wa mafuta na gesi na ugawanaji mapato

20. An Open Letter to Her Excellency Dr. Samia Suluhu Hassan, President of the United Republic of Tanzania

21. An Open Letter to President Dr. Samia Suluhu: Proposal for the Establishment of a High Education Graduates Bank (HEGB)

22. Barua ya wazi kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

23. Barua ya Wazi kwa Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Dkt. Dotto Mashaka Biteko: Waagizaji wa Mafuta watumie Dhahabu kununua Mafuta Nje ya Nchi

24. SoC03 - Mwarobaini wa Tatizo la Upungufu wa Maji Jijini Dar es Salaam ni Serikali yenyewe: Jukumu la Serikali na Maazimio ya Kutatua Tatizo hilo

25. SoC03 - Ndoto ya asubuhi ya Watanzania ya kuwa na Tanzania ya uchumi wa gesi na madini imo mikononi mwa viongozi wa Taifa hili

26. SoC03 - Ni jinsi gani Viongozi wa sasa wanaweza kurejesha Tanzania ya Viwanda ya Mwalimu Nyerere?

27. SoC03 - Je, Serikali inawezaje Kuweka Msingi Bora kwa Vijana ili Kutengeneza Timu Bora ya Taifa itakayoweza kushiriki na kushinda michuano ya kimataifa?

28. Uhusiano wa Katiba Bora, ukuaji wa uchumi na hali ya maisha ya raia wa Tanzania

29. SoC03 - Mkopo maalumu kwa kila kijana kutatua tatizo la ajira nchini Tanzania

30. Tufanye yafuatayo ili kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato katika bandari yetu ya Dar es Salaam (TPA)

31. SoC03 - Faida za Kubinafsisha Bandari ya Dar es Salaam ni Nyingi. Lakini Changamoto Tatu (3) Zinapaswa Kudhibitiwa Ili Tuweze Nufaika Zaidi

32. Watanzania tusiogope bali tuwekeze. Kuna Fursa za biashara zenye faida katika sekta ya mafuta na gesi Katika Taifa letu

33.

34. Tujenge kiwanda cha kuibadili gesi asilia kuwa petroli na dizeli

35. Usiogope unaweza kujenga na kumiliki kituo cha kujaza mafuta ya vyombo vya moto vijijini cha gharama nafuu

36. Siasa ya Mafuta na Gesi: Kuibadili gesi asilia kuwa mafuta ya petroli inaweza punguza gharama tunazotumia kuagiza mafuta hayo kutoka mataifa ya nje

37. Barua ya wazi wa Waziri wa Kilimo: Matumizi ya gesi asilia kuzalishia mbolea za kilimo (UREA, NA, CAN, SA, PA, CAN, MAPS na DAP)

38. Tukiibadilisha Gesi Asilia (CH4) iliyopatikana Tanzania kuwa Mbolea za kilimo tutainua uchumi wa nchi

Rejea za maandiko ya kuongeza mchango wa kukuza maarifa ya uhandisi na teknolojia ya mafuta na gesi duniani.

1. https://www.sciencedirect.com/science/article/pii/S294989102300310X

2. Numerical Simulation of the Oil Production Performance of Different Well Patterns with Water Injection

3. Equations governing fluid flow and transport in porous media and their applications in oil and gas production

4. Numerical Simulation of the Oil Production Performance of Di

5. Shu Jiang - Scilit

6. 概念ガス田のプラトー速度を拡大するための天然ガス生産システム制約の最適化に関するノードおよび最小コスト解析【JST・京大機械翻訳】 | 文献情報 | J-GLOBAL 科学技術総合リンクセンター

Mawasiliano:
Email: tsha87916@gmail.com
Hakika una stahili katka nyuzi zako zote hzo Basi mama akuone una kitu unakijuwa kwenye nishati na gesi

Kila kheri manager wa makampuni
 
Kuna watanzania wan upeo mkubwa sna wewe Ni mmoja wapo
 
Mbona hujaweka CV yako mkuu.Ili sisi tunaomshauri Boss,angalao tuone academic qualifications zako.Isije ikawa High School ulisoma combi ya HKL,na Varsity ukasoma BA in History,Halafu unataka kuwa MD wa Petrol & Gas !
Mkuu wangu kuhusu elimu wala usijali nitaweka. Niliepuka kuweka elimu yangu kwasababu wenye elimu kama yangu ni wengi kidogo. Nikaona ngoja mimi nikomae na sifa yangu ya uzalendo, kiu na kile nilichobeba kichwani ili kuwatumikia watanzania. Ndio hicho nilichokileta hapa jukwani mkuu wangu.
 
Hongera kwa andiko zuri, ningekuunganisha na mtu muhimu ambaye angekusaidia kupata nafasi nyingine kwenye taasisi hiyo hiyo ila sio nafasi uliyoandika hapo.

Bahati mbaya nimepitia CV yako naona bado upo shule unapambana na phD, mwisho kabisa kwa umri wako nakuona ukifika mbali miaka ya mbeleni.
 
Back
Top Bottom