Ombi la wazi kwa Rais samia kuhusu ujenzi wa uwanja wa ndege katika manispaa ya kahama mkoani Shinyanga

Ombi la wazi kwa Rais samia kuhusu ujenzi wa uwanja wa ndege katika manispaa ya kahama mkoani Shinyanga

Manala An Academician

Senior Member
Joined
Oct 10, 2016
Posts
119
Reaction score
57
Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan
Kupitia kwa Mhe. Waziri wa Uchukuzi

Kwa heshima na taadhima, napenda kuchukua nafasi hii kukupongeza Mhe. Rais kwa kazi kubwa na nzuri inayoendelea kufanyika chini ya uongozi wako thabiti. Nikiwa mwananchi na mdau wa maendeleo katika Manispaa ya Kahama, napenda kuwasilisha ombi langu la kujenga uwanja wa ndege ndani ya manispaa hii muhimu, ili kuleta mapinduzi ya kiuchumi na kijamii katika eneo hili na nchi kwa ujumla.

Manispaa ya Kahama, kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, inakadiriwa kuwa na idadi ya watu takribani milioni 1. Hii inaashiria kwamba nusu ya wakazi wa Wilaya ya Kahama wanatoka ndani ya manispaa hii. Ukosefu wa uwanja wa ndege katika eneo hili umekuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya kiuchumi, kijamii, na usafirishaji wa haraka wa abiria na mizigo. Watu wengi wanakosa huduma hii muhimu, hali inayosababisha gharama kubwa za usafiri na muda mwingi kwa wakazi wa Kahama na maeneo jirani wanapotumia viwanja vya ndege vya Shinyanga au Mwanza.

Kahama ni miongoni mwa wilaya zinazochangia kwa kiasi kikubwa katika Pato la Taifa kupitia vitega uchumi mbalimbali kama vile madini, kilimo, na biashara. Uwepo wa uwanja wa ndege katika Manispaa ya Kahama utachochea zaidi ukuaji wa sekta hizi kwa kuvutia wawekezaji wa ndani na nje, kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na huduma, na kuongeza mapato ya serikali. Takwimu zinaonyesha kuwa uwepo wa uwanja wa ndege unaweza kuongeza mapato ya serikali kwa kiasi kikubwa kupitia ada na kodi mbalimbali zinazohusiana na shughuli za usafiri wa anga.

Pamoja na faida hizo kwa serikali, wananchi, wafanyabiashara, na makundi mengine yatakayohusishwa moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja na huduma hii, watapata fursa za ajira, kuongezeka kwa usafirishaji wa bidhaa za kilimo, madini, na biashara, pamoja na kuboresha hali ya maisha kwa ujumla. Manispaa ya Kahama ikiwa na vitega uchumi vingi, mabadiliko haya yatakuwa na athari chanya kwa uchumi wa eneo hili na taifa kwa ujumla.

Iwapo utekelezaji wa mradi huu muhimu utachelewa kutokana na sababu mbalimbali, napendekeza hatua mbadala kama ifuatavyo:

1. Uwanja wa Buzwagi ambao sasa ni mali ya serikali, unaweza kufanyiwa tathmini na kupanuliwa ili kukidhi mahitaji ya usafiri wa anga kwa Kahama na maeneo jirani.

2. Kupitia na kuongeza idadi ya siku za safari za ndege zinazotumia uwanja huo kwa wiki, ili kupunguza gharama kwa wakazi wa Kahama na maeneo jirani wanapolazimika kusafiri hadi Shinyanga au Mwanza kwa huduma hiyo.

Napenda kumalizia kwa kutoa pongezi kwa serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuendelea kutekeleza ahadi kwa Watanzania, wakiwemo wananchi wa Kahama. Naomba maombi yangu yaweze kupokelewa na kufanyiwa kazi kwa ajili ya maendeleo ya Manispaa ya Kahama na taifa kwa ujumla.

Nakutakia kazi njema na utekelezaji wa majukumu yenu kwa maslahi ya Watanzania wote.

Wako katika ujenzi wa taifa,
Manala Tabu Mbumba
Mhandisi wa Nishati Safi na Magari
Mdau wa Maendeleo Kahama
+255 765 374 146
Airport.jpg
 
Mnayo maji ya bomba majumbani na barabara za lami nje ya mji kwanza??
Mtoa Mada Yuko sahihi. Kahama kwa Sasa imeanza kuvutia Wawekezaji wakubwa ..hakuna mwekezaji mkubwa anataka apelekwe na ma V8bkm 1000.

Nakumbuka Mkurugenzi aliyetoka nikiwa na Taasisi Moja hivi ya Dubai tuliwahi kufikisha wazo la upanuzi wa uwanja ule wa ndege tukiwa tumepitia TAA ...akasema yeye kipaumbele chake ni ujenzi wa Stand ya Mabasi.. ten plus years later hakuna stand Wala uwanja...😁😁😁

Wenye huo Mji mkikaa kizembe, mtatumika na mwisho kuachwa kama Ganda la muwa... Kila siku sifa za kukusanya mapato makubwa ..na mwisho nothing to show for it.

Maji Kahama yapo Tena ya kutosha, shida ya Kahama ni ni mfumo wa maji taka. Na sijawahi kuwaelewa Kashwasa lengo ni nini.. tunapeleka maji mjini ila sio kuyaondoa... No wonder kipindupindu hakiishi Nyakati za mvua Kahama.

Mavi yamepandwa kila konda kama yanaota vile. Mji unanuka vibaya tbh
 
Halafu unakuta huyo muombaji hatapanda hizo ndege maisha yake yote, lakini yeye atafurahi tu kuweka ligi ya kahama kuna uwanja wa ndege
 
Kuhusu
Mtoa Mada Yuko sahihi. Kahama kwa Sasa imeanza kuvutia Wawekezaji wakubwa ..hakuna mwekezaji mkubwa anataka apelekwe na ma V8bkm 1000.

Nakumbuka Mkurugenzi aliyetoka nikiwa na Taasisi Moja hivi ya Dubai tuliwahi kufikisha wazo la upanuzi wa uwanja ule wa ndege tukiwa tumepitia TAA ...akasema yeye kipaumbele chake ni ujenzi wa Stand ya Mabasi.. ten plus years later hakuna stand Wala uwanja...😁😁😁

Wenye huo Mji mkikaa kizembe, mtatumika na mwisho kuachwa kama Ganda la muwa... Kila siku sifa za kukusanya mapato makubwa ..na mwisho nothing to show for it.

Maji Kahama yapo Tena ya kutosha, shida ya Kahama ni ni mfumo wa maji taka. Na sijawahi kuwaelewa Kashwasa lengo ni nini.. tunapeleka maji mjini ila sio kuyaondoa... No wonder kipindupindu hakiishi Nyakati za mvua Kahama.

Mavi yamepandwa kila konda kama yanaota vile. Mji unanuka vibaya tbh
Kuhusu project ya maji taka Mpango , nilipata nafasi ya kuongea na Bwana Afya wa Manispaa. Alinihakikishia na maeneo ya kupokea maji taka yamekwisha ainishwa.
 
Mtoa Mada Yuko sahihi. Kahama kwa Sasa imeanza kuvutia Wawekezaji wakubwa ..hakuna mwekezaji mkubwa anataka apelekwe na ma V8bkm 1000.

Nakumbuka Mkurugenzi aliyetoka nikiwa na Taasisi Moja hivi ya Dubai tuliwahi kufikisha wazo la upanuzi wa uwanja ule wa ndege tukiwa tumepitia TAA ...akasema yeye kipaumbele chake ni ujenzi wa Stand ya Mabasi.. ten plus years later hakuna stand Wala uwanja...😁😁😁

Wenye huo Mji mkikaa kizembe, mtatumika na mwisho kuachwa kama Ganda la muwa... Kila siku sifa za kukusanya mapato makubwa ..na mwisho nothing to show for it.

Maji Kahama yapo Tena ya kutosha, shida ya Kahama ni ni mfumo wa maji taka. Na sijawahi kuwaelewa Kashwasa lengo ni nini.. tunapeleka maji mjini ila sio kuyaondoa... No wonder kipindupindu hakiishi Nyakati za mvua Kahama.

Mavi yamepandwa kila konda kama yanaota vile. Mji unanuka vibaya tbh
Ila stendi ya Kahama ni mbaya
 
Nadhani wangejikita mambo yanayogusa umma zaidi....hivyo vindege kwanza wapandaji n wachache......watanzania bwana! Badala ushauri wawekeze kwenye mambo yanayogusa umma( watu wengi) unaleta ushauri kulenga kijikikundi cha wachache....pitisha dodoso uliza watu wanahitaji nn mavijijini huko sio kutuletea hizi bla blaaa.
Barabara hazipo afu raia anaomba uwanja daaah
 
Back
Top Bottom