Halafu baada ya kuvutana na Mbowe, Dr. Slaa akarudi CCM na akawa mpiga debe wa CCM dhidi ya upinzani.
Huyo mtu atakuwa ana akili timamu kweli?
Yaani mtu aliyekuwa kwenye upinzani kwa miaka 20, akizunguka nchi nzima kuhakikisha CCM inaondolewa madarakani, ghafla anatofautiana na Mbowe kwa suala la Lowassa kuhamia CHADEMA na hapo hapo anahamia CCM kinyemela na kuhakikisha inapata ushindi.
Bora Yuda aliyemsaliti Yesu (maana usaliti wake ulizaa wokovu kwa wakristo) kuliko Slaa, mtu mpuuzi aliyehakikisha watanzania wanabakia kwenye utumwa wa CCM huku yeye akitafuna vitu vinono kwenye hoteli ya kifahari na kutunzwa Canada kwa pesa za wavuja jasho la watanzania.
Kuna uwezekano mkubwa sana kile kilichomkuta Yuda ipo siku kitamkuta Dr. Slaa, otherwise Dr. Slaa azunguke nchi nzima kuwaomba radhi watanzania kwa uovu wa kisaliti aliowafanyia watanzania kuanzia 2015.