Ombi: Serikali ituruhusu wananchi kutumia uwanja wa ndege Chato kuanikia mpunga, mihogo na mahindi wakati huu hakuna ndege

Mwenye picha atuwekee huo uwanja hapa.
 
Umenikumbusha miaka ya 2004, 2005, 2006 Maeneo ya Maseyu na vijiji fulani kabla ya kufika Morogoro ukitokea Dar walikuwa wanaanika mazao yao kandokando ya highway ya Dar - Moro (nje ya ule mchirizi wa njano)
 
Je kabla ya uwanja kujengwa hawakuwa na mahali pa kuanika mazao mpaka waende uwanja wa ndege?
Kama wengine wanapanga nyanya, vitunguu, vyupi na mapazia barabarani na "hawafanzwi kitu" wapiga kura wetu ajabu ni ipi kuanika mpunga na mahindi kwenye kiwanja cha ndege kilichojengwa na mtetezi wa wanyonge ili kumuenzi?
 
Uwanja unatumika na ndege za ATCL zinatua kila Jumatatu, Alhamisi na Jumamosi kushusha na kupakia abiria wanaotoka Dsm na wanaoelekea Dsm kupitia Mwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…