Ombi: Serikali ituruhusu wananchi kutumia uwanja wa ndege Chato kuanikia mpunga, mihogo na mahindi wakati huu hakuna ndege

Ombi: Serikali ituruhusu wananchi kutumia uwanja wa ndege Chato kuanikia mpunga, mihogo na mahindi wakati huu hakuna ndege

Ukiachana na hilo,naomba kujuzwa fursa za kiuchumi zilizoko hapo Chato.Hivi karibuni nitahamishiwa huko kikazi.

Huku niliko nilikuwa najishughulisha sana na kilimo cha karanga,mahindi na ufuta. Sasa huko Chato mmetaja panalimwa mahindi,mpunga na mihogo kwa wingi.Je,ni kata zipi zinafanya vyema kwenye kilimo cha mazao hayo? Na je,ardhi inaweza kuniruhusu kuendeleza kilimo cha karanga na ufuta huko?
 
Kama wengine wanapanga nyanya, vitunguu, vyupi na mapazia barabarani na "hawafanzwi kitu" wapiga kura wetu ajabu ni ipi kuanika mpunga na mahindi kwenye kiwanja cha ndege kilichojengwa na mtetezi wa wanyonge ili kumuenzi?
Genious, na ndege ziwe zinajibanabana zisikanyage mazao ya wanyonge kama yafanyavyo magari kutokanyanga mabeseni yaliyopangwa na machinga.
 
dah mwendazake kijaribu kupitia mitandao hko alipo atasaajabu sn sio kwa mawazo hy
 
Dunia ina mambo... Ukiwatendea watu ubaya utavuliwa nguo... ni moja wapo ya faida kwa wananchi kama watawaruhusu kutumia kwa matakwa ya raia wasio na uwezo wa kupanda ndege
 
njia bora kabisa ya utunzaji mazao
SUN drying haijawahi kuwa njia bora. Mleta mada awatafute TIRDO, UDSM, TAREA, SIDO hata SUA apewe elimu sahihi ya kukausha mazao aliyotaja. Dhiaka haijawahi kumsaidia mtu!
 
Sasa ni msimu was mavuno kwetu wakazi wa chato, mahindi,mpunga na mihogo iko kwa wingi, naomba serikali ituruhusu kutumia uwanja was ndege kuanikia mpunga, mahindi na mihogo,inatoka vizuri bila mchanga.

Ni ombi letu sisi wanyonge na masikini

Kidumu CCM
#matege
Naona historia inajirudia! Huenda wewe mleta mada ni kijana uliyezaliwa awamu ya Mkapa! Kama umekula chumvi kidogo, utajua kwamba historia hujirudia, ulipojengwa KIA (Kilimanjaro International Airport) ulipomalizika, ulikosa ndege maana EMBAKASI ya Nairobi ndiyo ilikuwa inajulikana/inavuma. Lawama nyingi sana na kashfa kemkem /kejeri zilitolewa kwamba serikali imekurupuka kujenga KIA! Enzi hizo watalii wa mbuga na vivutio vyetu walikuwa wanatua Nairobi/EMBAKASI! Safari zinapangwa kuanzia huko, Hata mlima Kilimanjaro ilikuwa unapandiwa upande wa Kenya!
To cut a long story short, sasa hivi KIA Inafanya vizuri Sana.
Kwa hiyo subiri kidogo Chato itatoboa,usikejeri
 
Back
Top Bottom