Watanzania wenzangu Mungu ni mwema bila shaka.Leo nimetafakari sana na mwisho wa siku imenibidi niandike ombi na wito kwetu watanzania. Hapana shaka kua kuna mambo ayako sawa sana asa kwenye nyanja ya siasa zetu. Ukweli wa ili jambo, nikupitia kwenye mitandao,maongezi ya watu, stori vijiweni na makazini.
Kuna kauli na mienendo yetu kama watanzania imeanza kupotea kwa kasi kubwa sana. Tangu awali sisi watanzania tume amini kwenye umoja,upendo,mshikamano maana tuna amani kua sisi ni ndugu wa damu,kabila,imani,dini na taifa. Kuna matukio mabaya ambayo yamelipata taifa ili siku za karibuni ,yakibakiza maumivu na hasira baina yetu. Wapo wanaolaumiwa kusababisha wengine kutenda na wengine kukwepa wajibu wao.
Matukio aya yametufanya watanzania tugawanyike kwa kasi kubwa sana na kubaki na chuki,hasira na visasi mpaka kutakiana au kuombea mabaya
Hapa naomba niwakumbushe asa viongozi wa dini na vyama vya siasa kwamba wametufikisha ambako atukupaswa kufika. Ni hatari sana kwetu tuliopo leo na vizazi vingine tukiendelea kulea na kushabikia hasira,chuki,visasi na maumivu. Ni wajibu wa viongozi wetu kua mstari wa mbele kuona tunarudi kwenye utamaduni wetu wa umoja,upendo,amani na undugu.
Utofauti wetu wa itikadi za kisiasa zisivuke mipaka na kusababisha maumivu makali yasiyo futika mioyoni mwetu. Vyama vya siasa vyote vijue kua lengo la hivyo vyama sio kutugombanisha,kutufarakanisha au kutuondolea umoja na undugu wetu bali vyama vinabidi vifanye zaidi kuona tunu zetu zinarudi na kudum vizazi mpaka vizazi.
Kua CCM,CHADEMA,CUF,ACT-Wazalendo ,CHAUMMA nk isiwe tiketi ya kuharibu au kuhatarisha tunu zetu.
NIWAOMBE WATANZANIA TUJIRUDI NA KUWAJIBIKA KULINDA UMOJA WETU,UPENDO,AMANI nk Tukumbuke vita vya panzi faidaewe. Na kwa mwewe/tai.
AKIBAZI-ITAHWA