Ommy Dimpoz amkana baba yake

Ommy Dimpoz amkana baba yake

Kuna mambo mengine wanawake wanayatengeneza wenyewe mimi mwanangu sijawahi hata mgusa zaidi ya kupewa picha mbili tatu tena kwa mbinde sana, mama yake ni kiburi tuu kimemjaa kisa kwao uwezo upo mtu anakaa kibaha anataka kuandikisha clinic lugalo nikahoji huko kibaha hakuna hospitali??

Akajibu ooh kugalo hospitali tunayoitumia familia nikamwambia huoni kwamba utajitesa na mambo ya nauli akadai atapelekwa na mamaake mdogo usafiri upo nikatulia nisikilizie siku ya clinic sasa anataka nauli sijui sasa hapo nilimpaga hela ya vifaa ili akiamua kwenda mambo yakae sawa siku ya kwenda anataka nauli hela ya clinic vifaa ile anadai alikula so jumla 270k kila kitu nikamwambia sina hela iyo nilichukia sana.

Ila ni kama ilikuwa sababu akaniambia namchukulia kama ana njaa sana basi nitulize nione kama ataniomba tena, akanilia buyu nikajua labda hasira za mimba mwee ndo ikawa ntolee iyo..nikimwambia nikutumie hela za kujikimu anadai Bi mkubwa wake kashalipa hana shida mapaka anajifungua ni kuchuniwa.. mwenyewe nikaona nibalansi shobo tu..
Shida inakuja pale unapouchuna na wewe. Kumbuka ile ni damu yako, sasa mtoto ni mdogo lakini ikifika amefikisha miaka 2 au 3 unaenda kumuona. Mtoto akikuona hata mama hamzuie vipi lazima mtaonana tu.
Wewe hauonekani mtoto mpaka anamaliza chuo kikuu anapata kazi, anaoa na kupata watoto ndiyo unajitokeza. hawezi kukuelewa
 
Shida ya sisi wanaume tunajiona tupo sahihi asilimia 100%. Kumbuka suala la kuhudumia familia ni la baba, chakula, malazi na mahitaji mengine.
Umegombana na mama yake, unamsusa na mtoto, unaoa mwanamke mwingine. Humtafuti mtoto. Umri umeenda na mtoto ameshakuwa mkubwa tena na maisha mazuri unamtafuta. Kwanini usimtafute akiwa utotoni?
Wanaume tunazingua sana wakati mwingine
Huu ndio ujinga wa wengi kama ukumtafuta utotoni usimtafute ukubwani
 
Comment yako imenigusa,, busara hekima huruma na uelewa wangu wote nimeshindwa hiki kitu, kufumbia macho ubaya bila maumivu wala kisasi, napambana ila nashindwa, nikiweza nitakuwa na amani sana maishani mwangu
Pole sana, Jitahidi tena utaweza hatimaye na yoote yatakayofuata kwako utakua mseleleko. Self peace of mind.
 
Ipo wazi anaemkabidhi mtoto kwa baba ni mama km mama hakumkabidhi kwa baba yake basi hata ningekua mimi nisingekua na time nae..

Itoshe kusema mama ndie anaemjua baba wa mtoto ni nani.. nyingine mbwembwe tu
Sawa lakini ukiamua hivyo mpotezee mazima...sio dogo baadae akitoboa kidogo unaanza matangazo ya huyo ni mwanangu
 
Sawa lakini ukiamua hivyo mpotezee mazima...sio dogo baadae akitoboa kidogo unaanza matangazo ya huyo ni mwanangu
Sio nimpotezee nmeshampotezee alafu hujawahi kusikia zile taarifa za kwenye Radio mtoto anajitangaza anamtafuta baba yake ambae hajaonana nae tangu anazaliwa au unaona ya baba kumtafuta mtoto tu na sio mtoto kumtafuta baba?

Kaongee na Farid Kubanda (Fid Q) atakueleza vizuri yeye alimtafuta baba yake alipo.. simple example
 
Na Mimi sijawahi kusikia mzazi akaenda kumng'ang'ania ubaba au umama kwa mtoto teja

Ommy mama yake kafariki akiwa la pili huko, ina maana hizo sumu alilishwa wapi

Kama alimtafuta mzee na kumpata na bado akaonesha kwamba watoto aliozaa nje kwake ni extra tu, ulitaka jamaa afanyaje

Nina wasiwasi kama hata umelelewa malezi ya single parenting let alone kumuona hata mtu wako wa karibu kapitia. Ungefuta haya maneno
Huyu dingi angejitokeza kipindi Ommy anaumwa kidogo angeeleweka...amekuja kujitokeza baada ya vi picha picha vya dogo anakula life ulaya..
 
Sio nimpotezee nmeshampotezee alafu hujawahi kusikia zile taarifa za kwenye Radio mtoto anajitangaza anamtafuta baba yake ambae hajaonana nae tangu anazaliwa au unaona ya baba kumtafuta mtoto tu na sio mtoto kumtafuta baba?

Kaongee na Farid Kubanda (Fid Q) atakueleza vizuri yeye alimtafuta baba yake alipo.. simple example
Nishiasikia hata kwenye kesi Mtoto ndio alianza kumtafuta Dingi. Ommy anasema baada mama yake kufariki na yeye kukua kidogo alimtafuta mzee na akampata..Ila bado dingi likampotezea...akasepa zake...sasa inakuaje dingi anajileta sasa hivi ambapo kidogo kijana kafanikiwa..
Halafu juzi juzi tu mshkaji alifanyiwa bonge la operation ya shingo huyu mshua alimjulia hata hali kweli? ( Hiyo ni siri yao).
Mi nafikiri huyu mshua ampotezee tu kijana. Ashukuru tu kijana yupo mzima yeye aendelee na bajaji yake mbona ni bonge la ajira tu.
 
Back
Top Bottom