Ommy Dimpoz amkana baba yake

Shida inakuja pale unapouchuna na wewe. Kumbuka ile ni damu yako, sasa mtoto ni mdogo lakini ikifika amefikisha miaka 2 au 3 unaenda kumuona. Mtoto akikuona hata mama hamzuie vipi lazima mtaonana tu.
Wewe hauonekani mtoto mpaka anamaliza chuo kikuu anapata kazi, anaoa na kupata watoto ndiyo unajitokeza. hawezi kukuelewa
 
Huu ndio ujinga wa wengi kama ukumtafuta utotoni usimtafute ukubwani
 
Comment yako imenigusa,, busara hekima huruma na uelewa wangu wote nimeshindwa hiki kitu, kufumbia macho ubaya bila maumivu wala kisasi, napambana ila nashindwa, nikiweza nitakuwa na amani sana maishani mwangu
Pole sana, Jitahidi tena utaweza hatimaye na yoote yatakayofuata kwako utakua mseleleko. Self peace of mind.
 
Ipo wazi anaemkabidhi mtoto kwa baba ni mama km mama hakumkabidhi kwa baba yake basi hata ningekua mimi nisingekua na time nae..

Itoshe kusema mama ndie anaemjua baba wa mtoto ni nani.. nyingine mbwembwe tu
Sawa lakini ukiamua hivyo mpotezee mazima...sio dogo baadae akitoboa kidogo unaanza matangazo ya huyo ni mwanangu
 
Sawa lakini ukiamua hivyo mpotezee mazima...sio dogo baadae akitoboa kidogo unaanza matangazo ya huyo ni mwanangu
Sio nimpotezee nmeshampotezee alafu hujawahi kusikia zile taarifa za kwenye Radio mtoto anajitangaza anamtafuta baba yake ambae hajaonana nae tangu anazaliwa au unaona ya baba kumtafuta mtoto tu na sio mtoto kumtafuta baba?

Kaongee na Farid Kubanda (Fid Q) atakueleza vizuri yeye alimtafuta baba yake alipo.. simple example
 
Huyu dingi angejitokeza kipindi Ommy anaumwa kidogo angeeleweka...amekuja kujitokeza baada ya vi picha picha vya dogo anakula life ulaya..
 
Nishiasikia hata kwenye kesi Mtoto ndio alianza kumtafuta Dingi. Ommy anasema baada mama yake kufariki na yeye kukua kidogo alimtafuta mzee na akampata..Ila bado dingi likampotezea...akasepa zake...sasa inakuaje dingi anajileta sasa hivi ambapo kidogo kijana kafanikiwa..
Halafu juzi juzi tu mshkaji alifanyiwa bonge la operation ya shingo huyu mshua alimjulia hata hali kweli? ( Hiyo ni siri yao).
Mi nafikiri huyu mshua ampotezee tu kijana. Ashukuru tu kijana yupo mzima yeye aendelee na bajaji yake mbona ni bonge la ajira tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…