Nimesoma na kusikiliza maoni mbalimbali kuhusu nachoweza kuita kutowajibika kwa malezi kwa baba yake Ommy kwa mwanae.
Hapa nitaeleza mkasa unaonihusu mimi wa kutowajibika kulea mtoto wangu.
Mwaka 2001 binti niliyekuwa na mahusiano naye aliniambia kuwa ana mimba, sikuikataa.
Jirani a nilipokuwa naishi kulikuwa na muuguzi rafiki yangu, nikamuomba ampime kuthibitisha ikiwa ni kweli ana mimba. Jibu la muuguzi lilikuwa tata kwangu, akaniambia ni kama ana mimba lkn inatakiwa turudie kupima tena.
Mimi nikahukumu kuwa hana mimba.
Maisha yakaendelea nikahama huo mkoa na kuhamia mkoa mwingine.Mwaka 2019 namba ngeni ikapigwa kwangu baada ya kuipokea akajitambulisha kwangu na kwa uhakika nikamkumbuka.
Akaniambia mtoto wako kakua na kamaliza kidato cha nne.Nilipigwa na butwaa kisha nikapuuzia. Nikajiuliza kama kweli ana mtoto wangu imekuwaje kwa miaka yote hii hakuniambia?
Nikahisi Kuna namna ya kutengenezewa mazingira ya kupigwa.
Siku nyingine akanipigia kusisitiza kuwa Kuna mtoto, mara ya pili nikahisi huenda Kuna ukweli nikamuambia mke wangu kuhusu hili.
Nikampa namba wife wakaendelea kuwasiliana na wife akanieleza kweli yule mwanamke ana mtoto wako.
Ikafanywa mipango mtoto nimuone, akaja na mamake mkoa nilipo lkn mtoto akakataa kuonana na mimi, akakutana na rafiki yangu, rafiki akasema kweli mtoto ni wa kwangu kwa muonekano.
Nikaamua tukutane rasmi, toka 2019 mpaka leo sijafanikiwa kumuona pamoja na kuwekeza nguvu kubwa kumtafutia.
Baadaye nikaona isiwe shida nikaachana naye na kamwe sitakuja kuja kumfuatilia.
Binafsi nahesabu kuwa mimi ni 'sperm donor 'kwa yule mtoto. Sijichukulii kama ni baba mzazi.
Moyo wangu unahisi hatia kidogo sana na kamwe sitakuja kuomba msaada kwake kama baba yake.
Baba Dimpoz komaa na maisha yako, muache dimpoz aishi maisha yake.