Huu nimjadala mzuri! Ni sahihi kumjadali "raisi ajaye" naomba tuanze kukiangalia kwanza chama anachokiongoza sasa maana kuna wakati tutalazimika kumuonganisha na chama hasa tutakapotaka kujadali uwezo wa mtuhuru kuongoza!
Chama cha Demokrasia na maendeleo tofauti na vyama vingine ni chama kilichokua kitaasisi na si ukuwaji wa puto(buble growth)kama vilivyo vyama vingine. Ninaposema ukuaaji wa puto nina maana gani? NCCR ilipata ukuaji wa gafla ambao ulitokana na umaaarufu wa watu binafis kwa historian a rekodi zao na si kuwaji wa chama wenye miundo ya kitasisi katika kukiendesha. Kumbuka wake ule NCCR ilikusanya watu wengi mashuhuri waliokuwa tayari wanafahamika kama kina Mrema, Marando, Lamwai,Makongoro, Abrahama Babu, Price Bagenda, Tenga na wengine wengi. Ilionekana kama "dream tema kwa wakati ule. Walichosahau ni kuwa ule ulikuwa ni umaarufu wa watu binafisi, watu waliambatanisha kwanza umaruufu watu kwanza badae chama.Ulikuwa mkusanyiko wa watu wengi wenye uelwea mkubwa na ushashi sana kwenye jamii, lakini udhaifu mkubwa chama kwa wakati ulle kiklikuwa hakina muundo uliokomaa kuweza kupokea haraka na hatimae kuendeleza ukuaji ule wa ghafla. Migogoro kwenye katika jamii ni jambo la kwaida na ipo kila siku kwa chama chochote, wengi wanadhani NCCR ilikufa kwa ajili ya mgogoro, kile kilikuwa kichochoe tu, udhaifu halisi ulikuiwa muundo na uteke wa chama kitaasisi kuweza kuwa na mamlaka zisizotiliwa shaka katika kutatua mogogoro. Matokeo yake mgogoro ule ulikipasua chama katikati, chama kilishutukizwa na ukuaji wa haraka na matokeo yake puto likapasuka!
Wakina Mrema wakahamisha ‘ukuaji', TLP nayo ikafumka kama puto ila baada ya mda kutokana na kufubaa kisiasa kwa Mrema TLP nayo imechanika msamba kwa maana umaarufu wa chama umejiambatanisha na umaruufu wa mtu. CUF nayo ilipata faida ya kisiasa ya hali ya kihistoria Zanzibar, matokeo ya uchaguzi wa Zanizbar NA Msuguano na mnyukano uliokuwepo kule ulikisogeza chama cha CUF katika ramani za Siasa Tanzania, huu nao hakuwa ukuaji wa kitaasisi wa chama sehemu ikuwa ni umaarufu binafis wa watu Maalims Seif( ambae amawahi kuwa Waziri kiongozi na baadae kufukuzwa chama katika hali iliyotingisha nchi) pia Haji duni shabani Mloo na wengine ukichanganya na makovu ya kihostoria ya kule(jumlisha na makovu ya mapinduzi) CUF ilipata ukuaji bandia. Tofauti na vyama vingine vya upizani ukuaji wa CHADEMA ulikuwa ni ukuaji wa kitaasi, ni kweli waasisi wake kama Mzee Edwin Mtei(Muasi na mwenyekiti wa kwanza) pamoja na Bob Makani(Katibu wa kwanza na mwenyekiti wa pili) kuwa wanajulikana lakini si katika kiwango cha kina Mrema na seif kwa maana hawa ni wataalam Mzee Mtei ni Gavana wa kwanza Mzalendo TZ na badae Kuwa Waziri wa fedha na badae kuja kujiuzulu miaka ya sabini baada ya kutofaotiana kimtazamo na Mwalimu pia Makani amawahi kuwa naibu Gavana. Hawa na wengine waasisi walitulia na kuunda chama kwa unagalifu mkubwa.
Walikuwa na Maono ya mbali walitaka kujenga chama chenye nguvu walitambua wao ni waanzilishi tu kazi itakuja kukamatwa na makamanda wengine hawakutaka kukurupuka! Ndio maana mwaka 1995 CHADEMA hakisimamisha mgombea wa Uraisi bali waliunga Mkono mgombea wa Uraisi wa NCCR kwa wakati ule(Mrema) na mwaka 2000 pia hakumsimamisha mgombea wa uraisi bali walimuunga Mkono mgombea wa CUF(Lipumba) wao walikazana kujenga muundo wa chama na kukijenga kitaasi kwanza! Pia hii ni sifa nyingene muhimu ya CHADEMA, kwamba kinaamini katika siasa zilizojuu ya vyama, yaani ni watanzania kwanza kisha ndio wanachadema na si kuwa wanaccm kwanza kisha watanzania! Ukifuatilia utabaini kwamba kati mwaka 95na 2000 CHADEMA ilikuwa na wabunge wawili tu bungeni(shujaa slaaa-Karatu na Walid Kaborou- kighoma Mjini) ilipofika mwaka 2000 walifanya ongezeko la wabunge toka mili mpaka tano(Slaa-karatu, Walid Kaborou- kighoma Mjini, Freeman-Hai{Takwimu zinasema ndio alikuwa mbunge wa upinzani alingie na kura nyingi kwa mwaka ule}, Ndasemburo(Moshi Mjini) na Grace Kiwelu-Viti maaluum) baada ya hapo mwaka 2005 chama kikaongeza wabunge kufikia 11(slaa, Ndesa,Wange{takwimu zinasema ndie mbunge wa upinzani mwenye kura nyingi kuliko wote}, Saidi Arfi-Mpanda Kati, Zito Zuberi Kabwe- Kigoma Kaskazinina sita wa viti maalum) somo hapa ni kuwa chama kimefanikiwa kutanuka na kuja na ngome mpya za tarime(kanda ya ziwa) na Mpanda Kati(ukuaji wa kustajabisha na kuvutia). Lazima ukumbuke pia kupitia uchaguzi mkuu CHADEMA ina ngoma nyingne nyingi sana zimetengenezwa ambapo wagombea wake ‘walitangaza' kuwa washindi wa pili haya ni majimbo nusu ya CHADEMA!
Leo tunazungumiza chama pekee chenye wenyeviti wa tatu wa kitaifa tangu kuanzishwa kwake, Mtei, Makani na sasa Mbowe. Kwa hiyo chama kina awamu tatu za uongozi. Unaweza tasfsiri kwamba awamu ya kwanza chini ya mtei ilikuwa na jukumu la kuanzisha na kukipa uhai(survival), awamu ya pili chini ya Makani kujenga miundo imara kitaasi na kukianda chama kwa ukuaji(Maintance) na awamu ya tatu chini ya Mbowe amabyo ina dhima ya kukikuza chama kwa haraka na kukiandaa kuakamata dola. Wachumbuzi wanasema kati ya awamu ya tatu na ya nne ya uongozi wa chama CHADEMA itakuwa chama tawala. Kwwa hiyo kama tunaovyuoona katika mtririko huu CHADEMA imekuwa na ukuaji wa kitaasi na si ukuaji wa puto kama vilivyo vyama vingine.
Awamu ya tatu imeweza kuwa na ujasiri wa kuvutia watu wengi kwa kuwa ina uhakika na miundo yake. Unapovutia watu wengi kwa haraka wanakuja watu wenye mitazamo tofauti na nia tofauti kwa mchanganyiko huo na hulka ya asili mgogoro ni jambo la kawaida swali ni je ipo miundo na taasisi zinazoeleweka kukabili migogoro itakajitokeza na ukuaji huu? Kwa maono ya mbali CHADEMA ilikuwa imekwsiha jiandaa. Majuzi ulipotokea Mgogoro wa Chacha watu walianza kupayuka kuwa ndio mwisho wa chama wakalinganisha na hatma ya NCCR na wanachosahanu ni kuwa kitaasi CHADEMA ilikuwa imekwisha vuka hatua hiyo ya ukuuaji sasa ni taasisi imara, inauwezo kukabili migogoro bila kuathiri au kutingisha uhai wa chama! Mgogoro wa chacha ulitutatuliwa kwa ustadi mkubwa na kufuata taratibu na miongozo ya chama ila kwa saababu kuna watu wenye nia mbaya waliamua kuukuza na kuonyesha kuwa eti chama hakijakomaa? Huu ni unafiki wa ajabu je ni taasisi gani ambayo hakabiliani na migogoro? Migogoro si kipimo cha ukomavu bali uweozo wa kutatua migogoro. Ndio mana hata ukiondoa chacha, Kaboru aliondoka akiwa makamu mwenyekiti pia Shaibu akilwombe akiwa naibu katibu mkuu bila kuathiri chama. CCM nayo ipitia misukosuko mingi katika uhai wake, imewahi kumfukazi unachama makamu mwenyekiti mwanzalishi wake Aboud Jumbe mwaka 84 ambae wakati huo alikuwa ni raisi wa Zanzibar, wakaja wakina Seif mwaka 88 sif akiwa Waziri kiongozi, taifa halipaswi pia kusahau mtikisiko wa Hayati Horace Kolimba amabe amewahi kuwa katibu mkuu amabe mauti yalimkuta katikati ya ‘utatatuzi' wa mgogoro leo upo mgogoro wa Nape!
Hivyo lazima watu waelewe moigogoro ipo na itaendelea kuwepo! Cha msingi na uimara wa chama katika kuisimamia na kuipatia ufumbuzi, kwa hiyo wanaosubiri CHADEMA ife kwa ajili ya mgogoro kwa maelezo kuwa wapinzani ‘hawajakoma' wana uhuru wa kufanya hivyo hata mpaka mwisho wa dahari. CHADEMA imweza kuibua na kukuza mashujaa wake yenyewe wapo watu kama Zito Kabwe ambao wamekuwa pamoja na ukuaji wa kitaasi, kwa wasiojua zito alijiambatanisha na CHADEMA tangu akiwa na miaka 16! Freeman mwenyewe amekuwa kisisasa sambambaba na taasisi anayoiongoza kumbuka alianza kama Mkurugenzi ya vijana! Leo wapo watu kama John Mnyika(Bingwa halisi wa harakati na mapambano ya kizazki kipya), Tundu Lissu , Halima Mdee na weng wanaoendela kuibuka kama uyoga.
CCM wanatambua hilo sasa wanatumia kila aina ya uhuni na ufisadi ilikukiondolea uhalali wa kisiasa CHADEMA! Vyama kama CUF, TLP na NCCR sasa vimeingiwa na wivu navyo vinashambulia pia CHADEMA, hawajui wenzao wamefanyia kazi kufika walipo, mvungi juzi kakurupuka kurupukua na kuelezea hisia za viongozi wengine wa vyama vya upinzani dhidi ya CHADEMA! Wenye akili wamekwisha elewa, vyama vingie viweke duara mapambano ya fikra na kimkakati sasa ni kati ya CHADEMA Na CCM. Chaguzi za 2010 na 2015(mwaka wa ahadi ya kinabii) zitakuwa ni chaguzi za kihistroia).
Changamoto iliyonayo sasa CHADEMA ni kuvutia zaidi watu wenye uelewa mkubwa pekee hawa kwa sehemu kubwa ni wachambuzi na wenye uwezo wa kutoa mawazo kukimarisha chama kimakati ni wachache sana wanaweza kuchafuka mikono na kuingia mzigonim hawa sio ‘risk takers' hufanya mambo yao kwa unagalifu wakitaka kwanza kukamilisha mambo yao binafisi. Ni muhimu sana kuwa na watu hawa lakini kuana haja ya kuwa na mchanganyiko na kuongeza wengi zaidi hasa wale amabao wako tayari kuchafuka mikono ambao wako wachache!
. Itapendeza pia ukikumbuka CHADEMA ndio chama pekee ambao kilipata "endorsement" ya mwalimu Nyerere. Alisoma na kukubali kuwa CHADEMA ndio mbadala wa kweli wa CCM, haya ni maneneno mazito sana toka kwa mwanzalishi wa Chama cha Mapinduzi! Huko nje kuwa ‘endorsesed' na watu wenye weledi wa mwalimu ni chapuo kubwa sana kisiasa.
Sisemi kuwa CHADEMA hakina hitilafu, zipo za hapa na pale kwa maana kinakuwa na kukabili changamoto kila siku. Utashangaa nikikwambia mimi hukosoa kwa hoja baadhi ya maamuzi ya chama kwa lengo la kujenga. Kwa maana rengo wa kati(socio0 democrats) kwa hiyo ni muanganiko watu wenye tofauti ndogo juu ya namna ya kuongoza nchi wakati CCM ni chama chenye mguso wa ukumunisti wa kale wenye mtazamo kuwa ni mkusanyiko wa watu waliowa sawa kimtazamo na fikra katika namna ya kuongoza nchi.