jamani naomba nimzungumze Mbowe kibinaadamu na kijamii na sio kisiasa. Freeman Mbowe ninayemjua mimi ni mtu wa msaada hata bila kukujua. Natao ushuhuda binafsi wakati najiandaa kwa harusi yangu, Freeman alijitolea bure kutumia ukumbi wake wa Bilicanas bila gharama yoyote. Huu ni ushahidi tosha anajitolea kusaidia anapoweza.
Kuna wakati nilikutana naye Washington DC mimi nikibeba maboksi. Akaniuliza kama nina taaluma yoyote ama naweza kufaanya kazi gani kkati ya decent jobs. Alinichukua na kunipeleka mpaka nyumbani kwa aliyekuwa mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Voice of America, Emmanuel Muganda, maeneo ya Maryland. Akanitambulisha akaniiombea kusaidiwa kupata kazi VOA. Muganda alinielekeza taratibu za kufuata kujoin VOA, sio siri nikachemsha mwenyewe nikaendelea na kubeba mabox- toka jimbo moja hadi jingine.
Kunawakati tulikutana tena mjini Boston yeye akiwa na rafikiye kwa jina la Makundi. Kama kawaida watanzania tukikutana ugenini tunachangamkiana sana. Wakaniuliza kama ninaprogram yoyote, japo nilikuwa na ka program kangu mshenzi, nikajibu niko free. Akaniuliza sehemu gani kuna bia na nyama choma ilikuwa aibu maana wao walifurahi wakajua wana mwenyeji, kumbe mie mwisho wangu ni kwa junk food za -
Kentuck au Tennesee. Akampigia simu jamaa mmoja akiitwa Asante Nsilo Swai yeye mwenyeji Boston akatuelekesa mahali. Akawapigia wabongo wengine wawili kundi likawa kubwa sie hao tukaenda kula nyama choma na bia.
Tulipofika hapo mahali unalipa dola 20 unaingia ndani unakula nyama unavyotaka. Freeman mbowe alitulipia wote, dola zaidi ya mia. Sio siri watanzania tu wakarimu tukikutana bar tunazungusha lakini kukutana na mbongo tena katoka bongo anazungusha Marekani sio kawaida huyu jamaa ana wema wa asili
Hayo yote yalitokea kipindi cha nyuma kabla Freeman hajaingia kwenye siasa. Sasa hivi sijui kama bado anatoa ukumbi wa bills bure na kama bado anamwagaa offers.