Maswali ya kujiuliza,
4 Je nyumba hizi zimejengwa kuwa kutumia malighafi na Rasilimali ambazo zinazalishwa Tanzania? Kama sivyo, ni kwa nini BOT ambayo inatakiwa kuchochea uzalishaji wa mali na kukuza uchumi wetu ilikubali mkandarasi alieagiza mbao kutoka Malaysia, huku tuna mbao nyingi kule Mufindi? Je udongo ulaya, misumari, fito, madirisha, samani, nyaya na hata udongo vilitoka nje ya nchi na hivyo kuongeza gharama za ujenzi?
Rev. Kishoka, swali hili, nimeliona very objective. Kutafuta na reasons behind any move/action/uamuzi hatimaye hutufikisha kwenye justification ya whatever is done/has been done. Baada ya kelele za Twin tower, mpaka leo ripoti ya value for money haijatolewa ili kuestablish genuine expenditure ni kiasi gani na ulaji ni kiasi gani.
Nliyaona hayo majengo, sakafu na kuta zote ni granite, hakuna tofali, wamemwaga zege ya foam tangu chini mpaka juu, wametumia japanese technology ya skyscrepers za kule kwa kutumia nondo za titanium ili hata likitokea tetemeko, jengo litaswing up to 45 degrees bila kubomoka. Wameweka fire resistant materials kwenye kila kuta ili moto ukitokea chumba kimoja, unaishia hapo hapo. Ndani wametumia light wood ili kupunguza uzito, hoja eti finishing ya cyprus yetu, haiwi smooth enough, na mbao ya Iringa ni too heavy and too expensive to process. Mambo mengine ni security issues kama bullet proof windows etc. etc.
Pamoja na vikolokolo vyote hivyo, sio justification ya lavish spending.
Kama Balali aliidhinisha ujenzi wa vikolokolo hivyo na bodi ikaridhia, naamini ndicho walichokifanya kwenye nyumba ya gavana, wameimimina zege tupu kama Ubalozi wa Marekani, Bomb proof as if Gavana anawindwa, hata Ikulu yet sio fotress kihivyo.
Watu huweza kufanya yote kutokana na preferences na purchasing power. Wakati saa ya kawaida Dar inaanzia Sh. 500 ya kibongo, kuna mtu anavaa saa ya mwaka 1933 gold Patek Phillipe kwa $11 million au hii 1 – $25 million – 201-carat Chopard iko sokoni na watu watafika bei, what for?. There must be a reason!.
Wakati brand new mobile phone ya kawaida ndani ya bongo, inaanzia Shiling 15,000! kuna watu wananunua mobile phone ya Goldvish "Le million" au Vertu Signature Cobra, au Sony Ericsson Black Diamond na kutumia kwa $1,000,000, ambayo ni sawa na nyumba ya Gavana!. What for?. Its for a reason.
No matter what, yes we can't justify such spending, but at least we should get the reasons behind ili tujustify at least what BOT Board were thinking about.
Tikisha pata hiyo justification yao, then tupige makombara kisawasawa to hit the target.
Japo siungi mkono hiyo PR Capaign ya Guardian, lakini niko curious kujua what a big deal ya hiyo nyumba ya 1.4 Bil. Baada ya kina Mramba, Yona na Mgonja kutiwa ndani, Ndugu jamaa na marafiki wa Mgonja na Mramba, walichangishana kupata thamana. Yona alijidhamini mwenyewe na miongoni mwa dhamana zake ni nyumba yake ya Makongo Juu, 1.2 Bilion. What's so big deal kuhusu hii ya 1.4 kabla hatujapata what are reasons behind justifying it.