On Ndulu: The "Guardian" must be kidding me!

On Ndulu: The "Guardian" must be kidding me!

Hiyo nyumba si itatumiwa na Ndulu, na Gavana wa BOT atakayefuata baada ya Ndulu?

ndiyo.. so what? kama kwa vile nyumba ni ya Gavana na siyo ya Ndulu na ni nyumba ya Magavana wengine watakaokuja kwanini tusiongezee vikolombwezo ifikie na thamani ya bilioni 5 hivi.. tuweke barabara ya lami hadi inapofika, tuongeze eneo la waandishi wa habari; tuongeze ofisi ya mikutano kwa wageni wanaofikia nyumbani kwake (si tayari tumewajengea vyumba hapo); Mnaonaje, tuhakikishe vile vile kuwa Gavana anakuwa na IT connection na Satellite connection ya kuwasiliana na magavana wengine wa dunia..

hivi vyote vitatumiwa na magavana wengine wajao. Kwanini tuishie kwenye nyumba ya Bilioni 1.4? Nikifiria sana naona gavana wetu anastahili nyumba ya bilioni 5? unasemaje?
 
ndiyo.. so what? kama kwa vile nyumba ni ya Gavana na siyo ya Ndulu na ni nyumba ya Magavana wengine watakaokuja kwanini tusiongezee vikolombwezo ifikie na thamani ya bilioni 5 hivi.. tuweke barabara ya lami hadi inapofika, tuongeze eneo la waandishi wa habari; tuongeze ofisi ya mikutano kwa wageni wanaofikia nyumbani kwake (si tayari tumewajengea vyumba hapo); Mnaonaje, tuhakikishe vile vile kuwa Gavana anakuwa na IT connection na Satellite connection ya kuwasiliana na magavana wengine wa dunia..

hivi vyote vitatumiwa na magavana wengine wajao. Kwanini tuishie kwenye nyumba ya Bilioni 1.4? Nikifiria sana naona gavana wetu anastahili nyumba ya bilioni 5? unasemaje?




Oh my god yaani nimecheka basi tu, ama kweli asiyejua maana haambiwi ... ...
 
Pasco said:
jmushi, asante sana kwa maoni yako, ninaposema sifagilii lavish spending, ninamaanisha kuna matumizi ya mabilioni na mabiliona yanakuwa spent na serikali yetu for nothing, or not accounted for. Hii ndio naita lavish spending.
Ok sawa,lavish spending ina maana "Matumizi ya serikali for nothing" ama "Not accounted for" Kwahiyo ku support matumizi hayo ndiyo unamaanisha kuwa "Accounted for?"

Pasco said:
Nimesema we deserve the best money can buy not the luxury. Mimi ni mtu wa Nyerere time, ile miezi 18 ya kujifunga mikanda ndio nilikuwa primary na foleni nimepanga mpaka zile za kupanga mawe nimeshiriki kupata kilo ya unga wa yanga!. Uniform tumevaa 'madurufu'. Kipindi hicho Nyerere alituaminisha personal car ni laxury, tv ni luxury etc. Nyerere ndie alitembelea benzi, mawaziri peogeot 504. Hivyo hata gari la kutembelea na tv kwa wakati huo ilikuwa lavish spending.

Once again,ndo maana nikasema unanichanganya,the best money can buy that is not "The luxury"..... Sio kwamba sijakuelewa na mifano yako ya kuhusiana na utawala wa mwalimu,lakini ninaposema "Unanichanganya" Ni kwamba you are exaclty right but in a definetly wrong way....Mifano ya miaka ya nyuma ya luxury za 504,tv nk eti kuonekana lavish spending sio mfano unaolingana na matumizi ya fedha za umma kuwalipa watumishi wake mishahara ama yenye kulingana ama hata kuzidi ile ya nchi kama USA.

Kuonekana kuwa ni Luxury,ni kwamba watu hawawezi ku afford,wananchi wa Tanzania kwa ujumla wao hawawezi ku afford matumizi hayo yanayoitwa "The best money can buy" eti na nyumba za viongozi zenye miaka mingi!

Mambo eti ya Nyerere alitembelea benzi mawaziri wake 504 hayana mantiki kwasababu hata benzi lenyewe si liliachwa na mkoloni?Mwache mzee wa watu apumzike,hata kama kuna aliyochemsha lakini nampa sifa kwenye uadilifu na heshma ya mali ya mtanzania....Huu upuuzi ndo ulimpa wazimu!

Narudia tena,hiyo mifano yako miwili haiendani kabisa,kwasababu kumbuka kuwa si kwamba mwalimu alishindwa kufanya hayo yote,ila kubwa moja ambalo hakusahau ni kwamba wananchi cannot afford all of that,kwasababu kama Taifa lazima tuwe na malengo,malengo ya masikini wa Tanzania si kuwatajarisha viongozi,hilo lieleweke.

Pasco said:
Leo gari tv, dish ni ordinary emenities sio laxury tena. Hivyo hiyo nyumba ya gavana, japo kwa sasa itaonekana lavish na laxury, imejengwa idumu miaka 100. Ile swimming pool ambayo leo inaonekana ni laxury, kwa wengine ni exericise ground for tension releave na relaxation, labda Balali angekuwa na swimming pool home na gym, asingekufa mapema vile, angekuwako on the dock na kutegua vitendawili kibao kikiwepo cha Kagoda.

Kwa vile hatuna detailed value for money ya hiyo nyumba na ina nini, then to me spending 1.4 billion kwa nyumba ya hadhi ya gavana itakayoishi for 100 years is not a big deal despite all our povert stinking nation kama hiyo ni fedha ya kununua only a single mobile phone ya Goldvish "Le million".
Kama kweli mnapiga mahesabu ya maisha ya nyumba ya gavana 100 yrs to come,je maisha ya wananchi yanapigiwa mahesabu gani?Mnasema mjenge nyumba ya gavana yenye life expectancy ya 100 yrs,lini wamesha piga mahesabu ya namna ya ku raise life expectancy ya mtanzania?Vipi kuhusu infrastructrures zenye kudumu kipindi hicho kama madaraja?Vipi kuhusu shughuli za uzalishaji nk?
Vipi kuhusu kizazi cha watanzania miaka mia ijayo?What are our priorities?

Pasco said:
Rev. Kishoka amekuwa objective kuhoji hivi hiyo nyumba ina nini?. ukishajua what it takes to swallow hiyo bilioni, then tunajustify lawama. J.Mushi huwezi amini, taasisi kama TACAIDS inatumia mara kumi ya kiwango kama hicho kwenye warsha, semina na makongamano kuhusu Ukimwi, huku waathirika wakiuliwa na retroviral kufuatia mlo mmoja kwa siku!.
Once again unachanganya,mifano isiyoendana,hao watu wa warsha za UKIMWI wanafanya hivo kwasababu ni pesa za misaada wao wanajipanga kuzikinga,na ndio maana kuna wakati ilikuwa dili kufungua NGO za UKIMWI hata mama Mkapa alifungua yake,ni kwamba wanajuwa wanazikinga,kama mashirika hayo ama nchi wafadhili wanatoa misaada hiyo kwa ajili ya wathirika wa UKIMWI na hayo ni mambo mawili tofauti kati ya njaa na ugonjwa....Na kwasababu TACAIDS wanafanya huo upumbavu basi na serikali iendeleze?

Pasco said:
Bilioni 1.4 is a lot of money in a small picture, but in a bigger picture, its nothing!. We are spending like hell for nothing, tunahaki ya kupiga kelele, ila pia sometime kelele zinazidi hata kama we are spending for something.
Mkuu nisikufiche ndio unazidi kama si kunichanganya basi naona sasa hata kujichanganya,hizo small and big picture ni zipi hizo unazozitumia kujustify matumizi kama hayo kwa niaba ya Taifa masikini?Eti unasema we're spending like hell for nothing na hapo hapo eti unadai tunaspend sijui the best money can buy?

The problem siyo eti kuspend tofauti na mafisadi kama wewe unavyoelekea kusema,the problem hapa ambayo naona tumepishana sana,ni kuwa we as a Nation,have nothing to spend as such....Na wewe unadai kuwa bado sisi ni washamba na kwamba eti tuwafundishe mafisadi namna ya kuzispendi pesa za watanzania kwanamna ambayo kuna "Kitu" kwamba it has not been spent for nothing,really?

Kwasababu kuna watu wenye mawazo kama yako na bado wataendele kuwepo,wenye kujua kula na vipofu,basi kulikomboa Taifa inaweza ikawa ni gharama ambayo bado hatuja i estimate wala kukaribia kufanya hivyo.
Tanzania haitaweza kubadilika kamwe bila mapinduzi,mark ma words.

Madai yako hapo hapo ni kwamba eti matumizi hayo siyo luxury ni ya kushangaza,mambo yote uliyoyaelezea mbona ni luxuries t?. Kwahivyo unatumia nguvu zako zote kutuaminisha sisi watanzania wa kawaida kuwa matumizi hayo si luxury ila kwasababu tuliishi chini ya ujamaa wa Nyerere(ambaye kwa mujibu wako aliwafanya mawaziri wake wapumbavu kwa kutembelea benzi na wao 504)Basi ndio mana tunashangazwa na hivi vijisenti na vitu vidogo vidogo,unasahau ile dhana kuwa chini ya mwalimu heshma ilikuwepo pale inapokuja kwenye mali za wananchi na rasilimali za Taifa?
 
Madai yako hapo hapo ni kwamba eti matumizi hayo siyo luxury ni ya kushangaza,mambo yote uliyoyaelezea mbona ni luxuries tu. Kwahivyo unatumia nguvu zako zote kutuaminisha sisi watanzania wa kawaida kuwa matumizi hayo si luxury ila kwasababu tuliishi chini ya ujamaa wa Nyerere(ambaye kwa mujibu wako aliwafanya mawaziri wake wapumbavu kwa kutembelea benzi na wao 504)Basi ndio mana tunashangazwa na hivi vijisenti na vitu vidogo vidogo,unasahau ile dhana kuwa chini ya mwalimu heshma ilikuwepo pale inapokuja kwenye mali za wananchi na rasilimali za Taifa.
jmushi, nimepanga hoja zangu, umezipangua moja baada ya nyingine, nimefika mahali, nimekubali, nimeishiwa hoja. Namalizia kwa kusema pamoja na hoja zote ni jumla tuu ya mauzauza ya serikali iliyopo, tusiishie kusema, huu ni mwaka wa kutenda, October ndiyo hiyo inakuja.
Asante.
 
jmushi, nimepanga hoja zangu, umezipangua moja baada ya nyingine, nimefika mahali, nimekubali, nimeishiwa hoja. Namalizia kwa kusema pamoja na hoja zote ni jumla tuu ya mauzauza ya serikali iliyopo, tusiishie kusema, huu ni mwaka wa kutenda, October ndiyo hiyo inakuja.
Asante.

Mkuu Pasco si kweli kabisa kwamba umeishiwa hoja,hoja yako ni ya msingi kabisa,tena nimeshasema toka awali,ila kuna pahala hapa na pale unanichanganya kidogo mkuu....Kiasi kwamba nashindwa kuelewa kwamba unakubaliana ama unakataa kuhusiana na matumizi mabaya ya pesa za wananchi masikini wa Tanzania wanaoombewa misaada kila kukicha.
 
Naomba kuuliza, je ni lini tulianza kuona Dola Millioni moja kama ni kitu cha kawaida Tanzania?
 
Naomba kuuliza, je ni lini tulianza kuona Dola Millioni moja kama ni kitu cha kawaida Tanzania?

Maswali ya kujiuliza,

1. Kwa nini bado tuna utamaduni wa mashirika, taasisi na Serikali kujengea wafanyakazi nyumba? Kwa nini wasijihudumie wao wenyewe kwa kutumia mishahara yao?
Mchungaji,
Yako hapo juu ni maswali yaliyoenda shule kwa kwenda mbele. Hata wenye dola yao ukiongelea milllion moja wewe siyo wakawaida labda uwe unaongelea pesa chafu

jmushi, nimepanga hoja zangu, umezipangua moja baada ya nyingine, nimefika mahali, nimekubali, nimeishiwa hoja. Namalizia kwa kusema pamoja na hoja zote ni jumla tuu ya mauzauza ya serikali iliyopo, tusiishie kusema, huu ni mwaka wa kutenda, October ndiyo hiyo inakuja.
Asante.
Kwa hili Pasco umekuwa muungwana. Haki ya shetani kule mwanzo nilipokuwa nasoma utetezi wako nilichora picha yako kichwani mwangu na nikatamani kukuweka mbele ya "firing squard" kama China vile.
 
Nikupe mfano wa UK. Serikali ina jukumu la kuwapatia makazi raia wake. Kama hawana nyumba inawapatia mahali pa kuishi na kuna system ya kuweza kuona uwezo wa kila raia wake. Ukiweza kulipa kodi kwa miaka kadhaa wanakuuzia kwa bei poa nk. Na hii ni kwa sababu ya kukusanya kodi na kuweka vitu muhimu kama makazi nk.

Unachosema wewe ni kwamba wale waliopata ndio basi wengine walie tu. Yaani waliowahi kuingia NHC warithishane hadi kiama. Je kulikuwa na muongozo gani hadi hawa wakodishwe na wengine wasiweze kukodishwa kwenye nyumba za NHC?

Je katiba ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema nini kuhusu hili?

Ukipitia yote hayo utarudi hapa na kuniambia jukumu ni la serikali na hapo ndipo utakata mzizi wa Wizi ambao umekubuhu na hauna tija kwa taifa. Pesa ambazo serikali inakusanya kwenye kodi nk ni tosha kabisa kufanya mambo makubwa ambayo wengine wanaona ni miujiza.

Mkuu, unachanganya. Hakuna serikali inayowapa watu nyumba. U.K inawapangisha watu wake wasio na uwezo kwenye nyumba za manispaa( wenyewe wanaziita council housing). Serikali ya U.K. iliweka sera ya manispaa zake kujenga nyumba za bei nafuu ambazo zitapangishwa kwa watu wenye kipato kidogo. Cha msingi ni kuwa, watu hawa hawapewi bali wanapangishwa. Pango katika nyumba hizi ni controlled na ni za chini kuliko zilizo kwenye soko huria. Watu wenye kipato cha chini wanalipa pango kutokana na pesa wanazopewa na serikali kuweza kujikimu. Hilo la kuwauzia wapangaji lililetwa na Margaret Thatcher, na inategemea zaidi sekta za fedha kuweza kutoa mikopo nafuu, inakayowawezesha hao watu kununua nyumba. Kitu serikali au manispaa inachofanya ni ku-guarantee mikopo hiyo.

Njia nyingine ambayo serikali ya uingereza inafanya kuwawezesha watu wake kuishi katika mazingira bora ni kuwalazimisha developers wote watakaopata kibali kujenga katika viwanja vyake kutenga baadhi ya nyumba kwa ajili ya watu wenye kipato kidogo.

Lakini pamoja na yote haya bado watu wengi tu hawana makazi halisi. Na ukweli ni kuwa nyumba nyingi hizo unazozingumzia siyo makazi bora. hali yake ni ovyo tu ukilinganisha na standard za kule.

Kwa maelezo zaidi bofya hapa:http://england.shelter.org.uk/housing_issues/Improving_social_housing/what_is_social_housing

Unataka kuniwekea maneno mdomoni. N.H.C. ilianza kwa kujenga nyumba za bei ya chini ambazo ziliuzwa kwa wale ambao nyumba zao zilibomolewa. Moja ya matatizo yaliyoikumba NHC ni kuchukua neno kujenga literally, wao walikuwa ndiyo developers, wachoraji na wajengaji. Mfumo huu ukaongeza ukiritimba kiasi cha kufanya uwezo wao wa ku-deliver nyumba nafuu kuwa compromised. Tatizo lako ni kuwa unadhani kuwa kupata ni kupanga nyumba ya NHC. Watanzania wengi wanapanga katika soko lisilo rasmi. Serikali, badal ya kuwekeza huko N.H.C. wangeweka jitihada za kuahamasisha wananchi wake kuwa na vyombo vyao vya kujijengea ambavyo vitapata mikopo nafuu na kupewa upendeleo katika bidhaa na vifaa vya ujenzi (kwa kupunguziwa kodi, kwa mfano) naamini wangekuwa na mafanikio zaidi. Watanzania wengi hawangojei nyumba za NHC, wanadunduliza kidogo kidogo na kujijengea. Serikali ingeelekeza nguvu zake kwa hawa na siyo kwa NHC kama unavyotaka wafanye. Manispaa zetu hazina uwezo wa kufanya wanavyofanya wenzao wa uingereza.

Narudia,Mkuu. Si jukumu la serikali KUWAJENGEA watu wake bali ni kuweka mazingira ambapo watu wake wanaweza kujipatia makazi bora.

Amandla.......
 
Wacha 1. Kwa mfano kwenye hili la Ndullu, badala ya kumjengea nyuma basi wangempa mshahara ambao ungemwezesha kupanga au kujijengea nyumba yake mwenyewe. Hii iwe kwenye mshahara na si kama kiji-allowance.

Amandla.....
 
Highest Paid Central Bank Governors:

#1 Joseph Yam, Hong Kong Monetary Authority
Salary: $874,474


#2 Mervyn King, Bank of England
Salary: $562,004

#3 Jean-Claude Trichet, European Central Bank
Salary: $533,035

#4 Axel Weber, Bundesbank Germany
Salary: $432,883

#5 Svein Gjedrem, Norges Bank
Salary: $274,672 (includes benefits)

#6 Stefan Ingves, Riksbank Sweden
Salary: $245,664

#7 Ben Bernanke, Federal Reserve
Salary: $191,300
 
Wakati umefika sasa wa kuziangalia upya TAASISI za UMMA zinazokusanya mapato kwa mujibu wa sheria zetu kama BOT, NSSF, PPF, EWURA, TCRA, SUMATRA, NHIF,....ili kuona kama matumizi wanayofanya yanaendana na hali halisi ya NCHI yetu au wanazitumia tu kwa kuwa ziko mikononi mwao na hawana pa kuzipeleka mbali na kwamegea kidogo wanasiasa wetu.
Tunachangisha wananchi masikini kabisa kujenga madarasa, kununua madawati, watoto wao wanakopeshwa ili wasome elimu ya juu; huduma za barabara, reli zimeshindikana; Polisi wetu wanashinda mabarabarani kuomba rushwa kwa sababu ya mishahara duni; Walimu wetu wanadai mabilioni; Watanzania kwa mamilioni (mijini na vijijini) wanakula mlo mmoja kwa siku;......
Huku Gavana wa BOT anajengewa "mbinguni" yake hapa hapa Tanzania. Ni lini na kwa njia gani mambo haya yatafikia mwisho?
 
Naomba kuuliza, je ni lini tulianza kuona Dola Millioni moja kama ni kitu cha kawaida Tanzania?

Tangu siku Chenge alipoziita vijisenti...........!!! Sasa tumeanza kuamini kumbe kwa tabaka viongozi, dola milioni moja ni vijisenti.
 
Wacha 1. Kwa mfano kwenye hili la Ndullu, badala ya kumjengea nyuma basi wangempa mshahara ambao ungemwezesha kupanga au kujijengea nyumba yake mwenyewe. Hii iwe kwenye mshahara na si kama kiji-allowance.

Amandla.....

well.. mtu anayelipwa dola 15,000 kwa mwezi anastahili allowance ya kiasi gani ya nyumba? miye hata naogopa kufikiria!
 
well.. mtu anayelipwa dola 15,000 kwa mwezi anastahili allowance ya kiasi gani ya nyumba? miye hata naogopa kufikiria!
Hata umlipeje. Pesa lazima itoke tu. Waliomweka pale wanataka pesa, chama tawala kinazitaka pesa,....Tusubiri tuone ripoti ya CAG itasemaje. Tunakwenda kumfukuza Mkurugenzi wa halmashauri masikini kama ya Bagamoyo tunawaacha hawa jamaa wanaojenga mabwawa ya kuogelea. Tuwaache wajenge hata viwanja vidogo vya ndege hapo ili wasipange foleni wakati wa kwenda makazini!
 
Highest Paid Central Bank Governors:

#1 Joseph Yam, Hong Kong Monetary Authority
Salary: $874,474


#2 Mervyn King, Bank of England
Salary: $562,004

#3 Jean-Claude Trichet, European Central Bank
Salary: $533,035

#4 Axel Weber, Bundesbank Germany
Salary: $432,883

#5 Svein Gjedrem, Norges Bank
Salary: $274,672 (includes benefits)

#6 Stefan Ingves, Riksbank Sweden
Salary: $245,664

#7 Ben Bernanke, Federal Reserve
Salary: $191,300


unaweza kwenda hadi namba 10-15 hivi maana wa kwetu anatengeneza $180,000 hivi bila malipo.. sidhani kama atakuwa mbali sana na Bernanke..
 
unaweza kwenda hadi namba 10-15 hivi maana wa kwetu anatengeneza $180,000 hivi bila malipo.. sidhani kama atakuwa mbali sana na Bernanke..

Atakuwa kamzidi Bernake maana sidhani kama Bernanke anapewa nyumba, walinzi, luku, maji na vikolombwezo vingine anavyopewa Gavana wetu. Hivyo vikolombwezo ukivipa bei, Bernanke haoni ndani!

Amandla.....
 
unaweza kwenda hadi namba 10-15 hivi maana wa kwetu anatengeneza $180,000 hivi bila malipo.. sidhani kama atakuwa mbali sana na Bernanke..
Mwanakijiji, baada ya mishahara hiyo hawajiingizi kwenye madudu kama haya ya hapa kwetu na uchumi wao unaibeba mishahara hii.
 
Mwanakijiji, baada ya mishahara hiyo hawajiingizi kwenye madudu kama haya ya hapa kwetu na uchumi wao unaibeba mishahara hii.

lakini wa kwetu anafanya kazi nzuri ya kuokoa uchumi wetu na ameshafanya mengi mazuri na ya mfano kwa hiyo anastahili.. halafu kwa vile yeye ndiyo mkuu wa benki hivyo anajua kuwa uchumi wetu unaweza kubeba mshahara wake..
 
lakini wa kwetu anafanya kazi nzuri ya kuokoa uchumi wetu na ameshafanya mengi mazuri na ya mfano kwa hiyo anastahili.. halafu kwa vile yeye ndiyo mkuu wa benki hivyo anajua kuwa uchumi wetu unaweza kubeba mshahara wake..
Ah! Haya bwana. Moja zuri la mfano nadhani ni haya majumba mawili ya 2.5bn!
 
Siku za hivi karibuni,nimeendelea kuamini kwamba vyombo vya habari vinavyo milikiwa na MENGI,vimekuwa vikiandika au kutoa habari ambazo ni kwa ajili ya maslahi binafsi ya MENGI au ya kundi lake kisiasa.Si shangai kuona The Guardian wanatoka na article ya kumsafisha Ndulu na benki kuu.
 
Back
Top Bottom