Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 10,448
- 8,705
Swala hapa isiwe kwa nini. Serikali ina jukumu la kuwajengea makazi bora raia wake wawe wafanyakazi wa benki, makarani au wakulima etc. Makazi bora kwa wananchi wote, hili ni jukumu ambalo lilianza tulipopata uhuru kama unakumbuka NHC ndio walipewa jukumu la kujenga nyumba na idara yoyote ya serikali ikihitaji nyumba wanakwenda kwa wataalamu wao ambao wamepewa hilo jukumu.
.Pasco mara nyingi nakubaliana sana na insights zako,lakini pia huwa unanichanganya sana mara nyingi,Sasa haufagilii lavish spending lakini hapo hapo unataka tuwe na the best money can buy?
Sehemu zote posting imetulia kasoro hapo tu....Na ndio maana nimetoa sanks lakini nikiwa critical kwenye red highlights.
Japo siungi mkono hiyo PR Capaign ya Guardian, lakini niko curious kujua what a big deal ya hiyo nyumba ya 1.4 Bil. Baada ya kina Mramba, Yona na Mgonja kutiwa ndani, Ndugu jamaa na marafiki wa Mgonja na Mramba, walichangishana kupata thamana. Yona alijidhamini mwenyewe na miongoni mwa dhamana zake ni nyumba yake ya Makongo Juu, 1.2 Bilion. What's so big deal kuhusu hii ya 1.4 kabla hatujapata what are reasons behind justifying it.
Si jukumu la serikali kuwajengea raia wake makazi bora. Jukumu la serikali ni kuweka mazingira ambayo yatawawezesha raia wake kupata( Kujenga au kupanga) makazi bora. Dhana ya kuwapatia wafanyakazi au raia wake makazi ndiyo iliyotufikisha hapa.
Amandla.......
Usimuonee yeye ameandika kama alivyoona na sio mtaalam. Ameona granite tiles zimetumika, akaambiwa madirisha ni bullet proof na vikolombwezo kibao alipouliza wakamwambia hiyo ndio Japanese technology etc etc. Ujumbe umefika.
.
Mzee Mwanakijiji, nyumba ya 1.4 Biliion ni nyumba ya Gavana, siyo nyumba ya Ndulu. Kila kitu kilipangwa kabla ya ujio wake.
Nyumba anayokaa ni nyumba ya Benno Ndulu siyo ya gavana, sasa maadam imetokea gavana ndie Benno Ndulu, mwache akae nyumba ya stahiki yake.
Kwa walio dar, si mnapajua pale kwa JK, piteni muune, nini bilioni 1.4!, majirani wamehamishwa hekalu linateremka, si JK yule yule aliyeishi hapo miaka yote?, why now?.
Kama kuna nyumba za mpaka bilioni 10 ila kwa vile ni za wahindi, hao hao wanaoendesha serikali kwa remote, hizo ni hizo hizo top up za rada, gulf stream etc, hatusemi, lakini akijengewa mwenzetu!.
Mtu wa kwanza kuendesha Ferari bongo Bongo ni mhindi, wa pili mwarabu, mswahili bado sijaona na akitokea ataitwa fisadi.
Nasisitiza siungi mkono matumizi yoyote mabaya ya fedha za umma, bali siungi mkono shutuma kwa matumizi yanayoonekana, japo mabaya, huku tuko kimya kwa mabilioni na mabilioni yanatumiwa kwa vitu visivyoonekana.
Pale kwa gavana, si angalau jengo lipo, nimewaambia kila safari moja ya mkulu, zinatumika zaidi ya hizo, kipi kinaonekana?.
Tumemlipa Prof. De Sotto, consultancy ya Dola, 1,000,000 kwa siku moja iliyokuja nchini, tunawalipa wangapi kwa huduma kama hiza and what do we get there after? Si afadhali hapo jengo la hadhi ya gavana lipo?.
Kuweka mazingira na kujenga kuna tofauti gani? Au unaongelea mazingira ya rushwa?
Pasco. Nenda taratibu, mbona unataka kutufanya wote limbukeni?
Hauwezi kutumia titanium kama nondo. Hata huko japan hawatumii. Titanium quality zake hazikidhi mahitaji. Titanium inatumika zaidi katika kufunika jengo na sio kwenye zege.
Hakuna kitu kama Japanese technology ya kujengea skyscraper. Ujuzi ni ule ule. Hesabu za structure ni zile zile. Ubunifu ni kwa watu binafsi na sio kwa taifa, Kwanza skyscrapers nyingi hazijengwi kwa zege. Ni chuma mtindo mmoja.
Light wood ndio nini? Kupunguza uzito kwenye nini? Unaweka sakafu na kuta za granite halafu unaogopa uzito!
Bullet proof windows za nini? Hivi wao wasiwasi wao ni watu kupigwa risasi au jengo kulipuliwa? Hizi ndiyo specification za kipuuzi.
Naona aliyekutembeza amekuingiza mkenge. Ukweli ni kuwa kwenye lile jengo hakuna value for money ya aina yeyote.
Amandla.......
Very true, tatizo hapa naona jazba ndio zinatawala. Nyumba ni kweli inaweza kugharimu bilioni 1.4 kutegemea na material yalitumika, security systems nk.
Ningekuwa mimi ningeuliza mchanganuo wa gharama kwanza kabla sijaita watu wajinga( MMK anasema Guardian are stupid).
Pia umefafanua vizuri kuwa ni nyumba ya Gavana wa benki kuu sio ya Beno Ndulu.
MMK sometimes naona kama sifa zimezidi na kudhani wate ambao hawafikiri kama yeye ni wajinga. NA mara nyinyine anapinga kila kitu.
Hasa siku hizi unaonyesha kama umeshuka kidog.. u complain on everything , ooh sijui Haiti hutujasaidia yani sijui vipi .. unaboa at times ile mbaya.
We say the said expenditure was a pretext because available evidence indicates that, based on the annual rent of 113 million/- BoT had been paying for the governors accommodation in rented premises
Mazingira ni pamoja na kumwezesha mwananchi kupata mahali pa kujengea, kuweza kupata pesa ( kipato kizuri au uwezo wa kukopa) au malighafi ya kujenga kama anataka. Ni mwananchi ndiye anayejenga sio serikali. Unaposema jukumu la serikali ni kujenga ina maana serikali inajenga na kumkabidhi nyumba mwananchi! Na kuwa na makazi mazuri si lazima yawe yako. Panatakiwa pawe na makazi mazuri yanayoweza kupangwa kwa bei inayomudika.
Si kila kitu ni rushwa.
Amandla........
Tatizo sio nyumba kugharimu kiasi hicho. Tatizo ni kutumia pesa za umma kujenga nyumba ya gharama hiyo. Kama ingekuwa kajijengea binafsi wengi tusingemchachamalia. kama Yona ana uwezo wa kujijengea nyumba ya mabilioni, hilo si shauri letu ili mradi akituhakikishia kuwa pesa zilizotumika hazikutoka serikalini. Pasco kuwa na simu ya $milioni moja haituhusu. Ni pale Pasco atakaponunuliwa na shirika la serikali simu ya $milioni ndipo panapotokea tatizo. Upuuzi fanyia pesa yako mwenyewe lakini si ya umma! Hakuna justification kwenye hilo.
Amandla........
Hiyo nyumba walipanga kutoka kwa nani? Na ilikuwa wapi? Na ikoje?
Amandla........
Very true, tatizo hapa naona jazba ndio zinatawala. Nyumba ni kweli inaweza kugharimu bilioni 1.4 kutegemea na material yalitumika, security systems nk.
Ningekuwa mimi ningeuliza mchanganuo wa gharama kwanza kabla sijaita watu wajinga( MMK anasema Guardian are stupid).
Pia umefafanua vizuri kuwa ni nyumba ya Gavana wa benki kuu sio ya Beno Ndulu.
MMK sometimes naona kama sifa zimezidi na kudhani wate ambao hawafikiri kama yeye ni wajinga. NA mara nyinyine anapinga kila kitu.
Hasa siku hizi unaonyesha kama umeshuka kidog.. u complain on everything , ooh sijui Haiti hutujasaidia yani sijui vipi .. unaboa at times ile mbaya.
Hiyo nyumba si itatumiwa na Ndulu, na Gavana wa BOT atakayefuata baada ya Ndulu?