Yep.......... nia hasa na madhumuni ya ...on second thought ....ilikuwa ni kubainisha kuwa
....... Wanaume wanajisikia vibaya sana juu ya limbwata, na katu hawaliafiki hata kidogo so sisi kama kina dada, si vema kuwafanyia limbwata watu tunaodai tunawapenda kwa sababu kama kweli unampenda huwezimfanyia kitu ambacho unajua kabisa kuwa akijajua atasikia vibaya na hapendi. Pili hakuna kitu kiitwacho Limbwata ya mapenzi na hiyo iitwayo limbwata la mapenzi si la mapenzi kweli bali la kuharibu na kujenga uadui na njia ya kutajirisha wanaojifanya waganga wa mapenzi.
So wito wangu kwa wadogo zangu na wale ambao wanayo bahati ya kupendwa...jiaminini na uzuri wa kujiamini unakuwa na hata uhuru wa kuwa mbunifu na kulifanya penzi lako kwa mwenzi wako kuwa jipya kila siku.
Wanaume pia wale wanaotumia limbwata na tego............wanawake mbona ni wepesi sana kutuhandle jamani? Kasema Babu Acid ...nyama ya ulimi tu inatosha.
Nawatakia kila la kheri katika mapenzi mwaka 2011.