Ona CRDB Dodoma aibu, teller wapo 8 halafu watatu tu ndio wanatoa hudumu kwingine kutupu

Wewe unaishi kwenye Ujima!
 
Na hapo kumtrace aliyepiga picha ni rahis tu..
 
tusamehe kwa usumbufu, leo ni siku ya usafi mkuu wa mkoa amatuagiza tufagie lami ndiyo tunamalizia muda huu.
 
Mambo ya kusimama foleni benki yamepitwa na wakati,utaanguka bure
Kuna CRDB fahari,kuna moblie,ukishindwa njoo STANBIC hakuna foleni za kipuuzi
 
MKUU AWAKENGEE N WAKUHAMAAA NA.MBAYA MADEMU WENGI WAMEKUWA.N NDUGU AMA MAHUSIANO NA MABOSI WANATESAAA KINYAMAAAA SOLN N KUPUNGIZA WALIOKUWEPO NA KUAJORI UPYA WASAHAU MAZOEEAA
 
Siku hizi kuna mawakala kila kona, hakuna haja ya kwenda kupanga foleni bank kwa ajili ya kuweka kudeposit. Labda kama mzigo mkubwa kiasi.

na kuna sim banking kama unaijua!
 
Mie huwa naenda benki ku renew kadi tu! Huduma nyingine namalizana na mawakala
 
Mkuu umeingia lini Tanzania mbona hio ndio modus operandi ya hili Taifa
 
Bora hao CRDB yasikukute yaliyonikuta BOA(Bank of Africa) nimefanya transaction kutoka account ya Bank via Mobile banking kwenda M-Pesa toka saa saba mchana tar 24 hadi leo tar 25 saa tisa hii pesa haijafika M-Pesa TZS 600,000, nikawapigia simu jana jioni simu ipo kwenye foleni kwa muda wa zaidi ya kd 40 na ukizingatia namba yao ya huduma kwa wateja sio bure kuipiga unakatwa bundle ulilojiunga, nimewafuata ofsini kwao hapa nasubiri sms ya kurudishiwa hiyo pesa kwenye account

ki ukweli wanakera sana, nimejaribu kuwaza ingekuwaje kama hiyo pesa ingekuwa naituma kwa mgonjwa sijapata jibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…