Ona hapa aina mbili mpya za wizi wa pikipiki ulioshamiri mijini

Zamani kwenye hii kazi ya Bodaboda risk kubwa ilikuwa ni muda wa usiku but siku hizi wezi nao wameendelea sana, kuna dogo moja akikuwa na pikipiki mpya akaja mtu aliyevaa kimasai ampeleke sehemu yenye umbali kidogo kama km 35, walipofika eneo lenye pori abiria aliomba kujisaidia aliposhuka tu alitoa sime na dogo akakabidhi Boda kiulaini.
 
Ni wazo zuri ila wezi nao huwa kidigitali wanaweza kuharibu hiyo security system kama wamegundua ipo ili lengo lao litimie.

Wahuni sio watu.
 
Kuna jamaa mmoja alienda sehemu kwenye kijiwe cha bodaboda akachukua bodaboda siku ya kwanza akaenda site jamaa akashuka akaenda ongea na wale mafundi then akarudi kwa bodaboda akarudi kituoni jamaa akapanda daladala akaondoka

Siku ya pili the same way

Siku ya tatu the same way

Siku ya nne jamaa alivyoshuka kwenye daladala alikuwa amebeba ndoo ya rangi mpyaaa

bodaboda akamkimbilia akamwambia kama kawaida jamaa akasema naaam jamaa akaenda site mshkaji akamwambia tushuke uone nyumba wakawa wanaelekea kwenye nyumba

Ile wanakaribia kufika kwenye nyumba this time jamaa kununua na rangi yaani ile wanakaribia jamaa akamwambia unajua nimesahau misumari hebu nishikie hii ndoo ya rangi nikakimbilie misumari pale road

Bodaboda likawa limebeba ndoo ya rangi akimsubiri jamaa dakika 5, 10, 20, 30 ikabidi awaulize mafundi kama ana namba ya mshkaji ili ampigie amuulize shida nini mbona kachelewa

Kuuliza washkaji wanamwambia Yule sio mwenye nyumba huwa anakuja pale kutafuta kibarua siku ya kwanza hakukutana na fundi mkuu siku ya pili hakukutana na fundi mkuu siku ya tatu hakukutana pia na fundi mkuu na wao walishangaa kumuona anakuja na rangi wakajua maybe wameshaonana na fundi mkuu

Yaani mwamba alikuwa anamdanganya bodaboda naenda site yangu nyumba yangu najenga, mwamba akifika kwa mafundi anafika kuulizia nafasi ya kibarua bodaboda anakaa mbali anajua mwenye nyumba anafanya ukaguzi wa nyumba yake

Jamaa bodaboda alivyoambiwa vile ushuzi ulimtoka bila yeye kujua
 
Ni wazo zuri ila wezi nao huwa kidigitali wanaweza kuharibu hiyo security system kama wamegundua ipo ili lengo lao litimie.

Wahuni sio watu.
Inapofungwa hats mwenye Piki piki hujui...unawakabidhi chombo inakuja imeshafungwa na haionekani...inapunguza risk kwa kiasi kikubwa sana.
 
Aisee hatari sana
 
Hiyo style ya pili waliijaribu mtaani kwetu. Na mtaa ulivyo mtulivu walidhani hauna watu.

Hivi ninavyoongea jizi moja limeweka makazi ya kudumu ahera madukani.
 
Inapofungwa hats mwenye Piki piki hujui...unawakabidhi chombo inakuja imeshafungwa na haionekani...inapunguza risk kwa kiasi kikubwa sana.
Haionekani? unajua iyo ni wireless communication lazima kutakuwa na hardware kwenye pikipiki dereva hata asipojua hakuna shida lakini mwizi kama yupo makini anaweza akatafuta na kuharibu hiyo system maana inàmuhusu yeye sio dereva.
 
Dereva tu hajui ilipo,ndio aje kujua mwizi!
Udogo wa pikipiki unaashiria kuwepo na sehemu chache za kuweza kuficha hicho kifaa. Hivi wezi hawawezi kuwa na uzoefu wa kujua sehemu zote muhimu kwenye pikipiki ambazo wataalamu upendelea kufunga kifaa hicho ili mara tu wanapoiweka pikipiki mikononi kazi ya kwanza inakuwa ni kukagua hizo sehemu zote zenye uwezekano wa kuficha kifaa hicho na kukiondoa kwa haraka?
 
wamekusikia
 
Aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…