Once-in-a-lifetime experience: Sayari ya Mshtarii na Zohali zinatarajiwa kuonekana kama umbo moja usiku wa leo

Once-in-a-lifetime experience: Sayari ya Mshtarii na Zohali zinatarajiwa kuonekana kama umbo moja usiku wa leo

Sam Gidori

Senior Member
Joined
Sep 7, 2020
Posts
165
Reaction score
417
night-sky-map-great-conjunction.jpg


Baada ya zaidi ya miaka 400, leo usiku sayari mbili kubwa zaidi katika mfumo wetu wa jua, sayari ya Mshtarii (Jupiter) na Zohali (Saturn) zinatarajiwa kuonekana katika umbo moja kutoka duniani.

Tukio hili linalotokea mara moja katika muda wa uhai wa mwanadamu linafanya sayari hizo mbili kuonekana kama 'nyota' moja. Mara ya mwisho tukio kama hilo kuonekana ilikuwa zaidi ya miaka 400 iliyopita, Julai 16 mwaka 1623.

Si kweli kwamba sayari hizo mbili zitaungana na kuwa kitu kimoja, kuna umbali wa zaidi ya kilomita 733,205 kati ya sayari hizo mbili, na umbali wa kilomita 886,440 kati ya dunia na sayari ya Zohali, ila sayari zote mbili zitakuwa katika mstari mmoja wa mwonekano kutoka duniani.

Sayari hizi mbili kubwa zinaonekana kwa urahisi kutoka duniani, na tukio hili linaweza kuonekana katika maeneo mengi duniani. Tafuta sehemu nzuri usiku wa leo utazame upande wa Kaskazini Magharibi uweze kuona tukio hili ambalo hautaweza kuliona tena katika maisha yako.
 
Zilianza jana..Jana nimeona nyota zimekaribiana magharib nikajua TAYARIII
 
Nini kinasababisha ziwe ktk mstari mmoja wa mwonekano
 
Kweli utawala ukipitishwa na Mungu mambo mema hutokea.

Tangu rais Magufuli aingie madarakani ishara nyingi za utukufu zimetokea kote duniani..

Kasi ya rais Magufuli ni kubwa.

Sent from my Infinix X622 using JamiiForums mobile app
 
Leo asubuhi zimeonekana, hivyo jioni ya leo kama jua likizama zitaonekana tena. Kiukweli zinang'aa sana
 
Back
Top Bottom