Ondoa ''misconception'' kuhusu Wanyarwanda

Ondoa ''misconception'' kuhusu Wanyarwanda

Kaka hayo yanayotokea kwingine mimi hayanihusu, naiongelea nchini niliyozaliwa mimi, ambayo nilizaliwa ndani ya ardhi yake zaidi ya miaka 40 iliyopita. Eti kwa sababu watu wengine wanatembea uchi basi na sisi tutembee uchi, eti kwa sababu wachina wanakula nyoka, na sisi tule nyoka!!!. Naizungumzia nchini, na ninapoiongelea ukumbuke kuwa mimi ni mzalendo kama yoyote yule unayemjua wewe. Lakini ukweli kwanini usisemwe?, kwanini uogopwe?. Tusipoambiana ukweli yule anayeuona kutokea nje, hataacha tabia ya kutudharau na kutucheka. Nayaandika haya ili yaweze kuchangia katika kubadilisha mindsets zetu.
We nawe usiwe kichwa kigumu.duniani pote wapo watu wa aina zote.unapokomalia watanzania wabadilike as if huko Rwanda wanaishi malaika nakushangaa .eboo. Haya hizo tabia wanazowasema sijui Watusi naamini si wote wako hivyo so tusipende kugeneralize. Kumasimita
 
Ninacho gundua tz ni wivu umewajaa hasa wadada wa bongo hawapendi kabisa wanayarwanda maana waliwafunika mbali sana kisura kiumbo wale watoto wazuri kuanzia nywele hadi unyayo tabia ni misconception tu mwakani naoa mtusi
hahahaaa, utakufa ww, daah totoz za kitutsi ni noma
 
My friend tusisumbuane akili kama unaweza uka google then why should you tell me to tell you things that you can find by yourself. Mheshimiwa kama huna jambo la kufanya vuta shuka ulale. Hii ni mada ya juzi unaendele kuivuta kwa misingi ipi?. Tafuta la kufanya ufanye, hii mada sio mpya.
Usikimbie.jibu maswali aliyokuuliza
 
We nawe usiwe kichwa kigumu.duniani pote wapo watu wa aina zote.unapokomalia watanzania wabadilike as if huko Rwanda wanaishi malaika nakushangaa .eboo. Haya hizo tabia wanazowasema sijui Watusi naamini si wote wako hivyo so tusipende kugeneralize. Kumasimita
Kaka kuna watu wameurlewa ujumbe wangu. Usitake nilazimike kurudia kitu kile kile muda wote.
 
Usikimbie.jibu maswali aliyokuuliza
Heshima kitu cha bure ndugu yangu, siwezi kuongea the same thing two days in a row. Siwezi kukimbia kwa mambo hayo madogo, kero kwangu ni mtu kuja kutaka niongee naye kwa muda ambao yeye yupo comfortable na mimi sipo tayari kuongea naye.
 
Heshima kitu cha bure ndugu yangu, siwezi kuongea the same thing two days in a row. Siwezi kukimbia kwa mambo hayo madogo, kero kwangu ni mtu kuja kutaka niongee naye kwa muda ambao yeye yupo comfortable na mimi sipo tayari kuongea naye.
Haya kalale.kumaasimita
 
Haya kalale.kumaasimita
Kuzungumzia issue moja sio kibali cha mtu mmoja kujenga ukaribu kupita kiasi, jaribu kujichukulia kama mtu mzima. Pengine unaweza ukawa unaongea na mtu mwenye umri mmoja na mzazi wako. Be careful the way you are talking my friend.
 
Kwa hiyo facts huwa ni positive tu, zikiwa negative sio facts bali mihemuko? Doh umenishinda tena.
we unaziona ni facts lakin kiuhalisia sio facts, ndo maana nikasema facts gani za vile? elewa zile sio facts positively wala negatively bali ni mihemuko yako tu ya kila siku hapa jukwaani
 
Bukililo ni mtanzania Mnyarwanda...ana damu ya Kitutsi, anaongozwa na ukabila ulioko moyoni.
 
Umeandika mema na mazuri na ukweli mtupu. Rwanda ni nuru katika eneo la maziwa makuu. Wanaoitukana Rwanda hapa ni mahasimu wa Kagame au masalia na washabiki wa FDLR au waswahili wasiojua kinachoendelea Rwanda. Aidha, kuna wenye kuchukia Tutsi bila sababu za msingi.
 
Waungwana kaka yenu nakaribia kurudi nyumbani baada ya kuishi hapa DRC kwa Takriban miaka 2.

Katika kipindi chote nilichokaa hapa nimejifunza mengi sana ila leo nitazungumzia kuhusu hawa jirani zetu Wanyarwanda.Maana nimekua nikipita hapa mara kwa mara. Kwa kifupi ondoeni dhana potofu kuhusu hawa jamaa maana mimi dhana hiyo tayari nimesha ifuta. Wengi wenu kama sio wote mnadhani kuwa wanyarwanda ni watu ''wasio poa'' au ni wenye majivuno labda wengine mnadhani eti hawatupendi Watanzania.

Dhani hizi ni potofu kweli kweli, mwanzoni nikipita hapa sikua nikiongea kiswahili ili nisitambulike maana niliogopa kweli hawa jamaa. Baadae nikagundua dhana yangu sio sahihi kabisa na Mungu anisamehe.

Hawa jamaa hawana shida kabisa na wageni hasa Watanzania. Nimekaa Hoteli mbali mbali hapa nikiwa transit kwenda DRC au kurudi Home Tanzania, na kote huko nimechukuliwa vizuri sana tu.

Sio hotel tu , nimepanda boda boda, nimefika masokoni, msikitini , madukani kote huko hawa jamaa ni wakarimu sana na nimetendewa vizuri kwa kweli.

Wacha niweke mifano michache hapa mnielewe, nasisitiza michache mana nimengi nimeyaona positive.

1. Nikitoke DRC kurudi home ( niko njiani) tukiwa pale Kingarama Restaurant nikapata shida kidogo ya chenji ya Dollar kwa FRC ya Rwanda ili nipate Supu, wakati nikitaka kutoka nikatafute nje chenji mzee mmoja akasema kumwambia mhudumu mwache apate hiyo supu nitalipa mimi kama 'felistation' maana walitufunga kombe la CHAN huyu mzee alijua mimi ni Mkongo, nikala na wala hakukaa kuni bore kwa vile ameninunulia supu alitimua.... nikashangaa maana DRC husema hawa jamaa hawawapendi

2. Mh PK alitoa ma Bus kadhaa kuja pale Gisenyi kuchukua mashabiki wa DRC bure ili waje washangilie timu yao .... BUS zilijaa wakongo na walilindwa na wakarudi kwa amani.

3. Nilipofika Kigali na baada ya kuchukua Hotel, nikataka kwenda Masjid kusali , nikauliza Reception , kwa mshangao akadakia jamaa mmoja na kuniambia ''msikiti uko mbali ila subiri nitakupeleka maana naelekea njia hiyo hiyo huyu hakua musilam na hakua akinijua , ni tax man tu alie leta mteja pale. Njiani tulipiga soga sana.

4. Nikiwa hapa kwa siku ya pili na ticketi yangu ikiwa ya jioni nikaona ni negotiate nikae mpaka jioni kwa kulipa kidogo chumba maana check out ni saa tano asubuhi... Manager akasema ''kaa tu usilipe chochote , karibu tena wakati mwingine''.

5. Huko mitaani niliko kwenda kutembea jana usiku, nilikutana na ukarimu sana hasa unapouliza direction na mengine. hawa jamaa wana smile sana na sio ya smile ya kinafiki au ya kutegemea kitu

(a) Kitu nimegundua labda unaweza sema cha kushangaza au sio kizuri ni kwamba watu hapa hawaongelei siasa sana , ni aghalabu kukuta watu wakiongelea siasa hapa tofauti na home TZ kila mtu politician

(b) Printing media sio nyingi ila TV station wanazo nyingi tu

(c) Polisi ni vijana na hawacheki cheki wako serious kweli ila ukiuliza kitu wanakujibu vizuri tu

(e) Rushwa hapa sio sana labda niseme hakuna, polisi akikumata unaandikiwa charge hakuna zile za kuvutana nyuma ya gari na watu wanatii sheria kweli kweli

(f) Ule mfumo wa ukusanyaji kodi kila duka hapa, na kuna ka machine kama ka fingure print sijauliza ni ka nini ila ni ka mamlaka ya Kodi ya Rwanda. ( hapa nikakumbuka zile machine zetu sijui zilishia wapi maana zilileta sintofamu)

(g) Taxi zina Automatic Counter kama za Europe


NIMEONA MENGI WACHA NIACHIE HAPA NA WENGINE WACHANGIE MAANA NATUMAINI KUNA WENGI WAMEPITA HAPA PIA, WITO WANGU KAMA UNA JIRANI YAKO MNYARWANDA USIMTENDEE VIBAYA HAWA WATU WENGI WAO NI WAZURI SANA KWETU
umesahau kuuliza kwa nn anawabagua wahutu, mfano hoteli uliyo lala wahudumu wote ni watusi.
 
Bukililo ni mtanzania Mnyarwanda...ana damu ya Kitutsi, anaongozwa na ukabila ulioko moyoni.
Laiti ungenijua wala usingeandika maneno kama haya, ujumbe wangu ni mpana kuliko huu unaosomeka moja kwa moja. Lengo langu ni jema kwa Tanzania na watanzania wenzangu kwa ujumla wetu.
 
Plse i just cant read end of most reply which are typicaly Tanzanian as usual ukitaka mbongo akuchukie mwambie ukweli! And wanasema "WHERE IGNORANCE IS BLISS IT IS FOOLISH TO BE WISE" am so much suprised na wote wanao bisha ati Kagame!Rwanda hajafanya lolote kweli? Kindly ingia just you tube andika city of Kigali ukishatazama then andika Rwanda! Mh ndo u will have the smooth eye opener of what Kagame has done to Rwandans despite the Genocide of 1994 which many of u have used as a weapon to lash back to Rwandans,such unmerceful Souls ur! kwanza a good example Rwanda air! je muna shirika la Taifa la ndege Tanzania?Mumewai ona usafiri wao wa mabasi ulivo wa kisasa?na wenyewe walivo wastaarbu? Mabus sio ya kupgania kama bongo! My God in years to come almost wanya Rwanda wote wanaongea ENGLISH/FRENCH/KINYARWANDA/KISWAILI! Perfectly?KAGAME very clever after kuhama Francophone (french)na kuenda Anglophone basicaly kutumia English(worlds widely used language)alichukua best teachers toka Kenya and Uganda! Wao wamejiandaa kuuzika kimataifa kielimu very well! Huezi pata mafake ya kichina ovyo Rwanda just 1grade toka China! Vitambulisho vyao nice kama va bank do u have IDC ? si pesa imeliwa yote? Kila mtoto anapozaliwa ana pasport Rwanda! do u do that in Tanzania? Nimempenda ukifanya ushenzi kwa serikali yake no discusns justice take its path then jail! And KAGAME hana masihara what a leader!
kwa informatn walifanya referendum na asilimia 94 ya wanyarwanda walimpendekeza aendelee kuongoza manake amewabadilishia nchi sana! Huduma za afya clasic! Jamani pendeni kugoogle to know the facts! Last point ingia you tube andika Thikahighways/Kenya another eye opener finaly yotube andika city of Malabo/Guenea Equatorial kanchi kadogo kama pemba ila uchumi matata! Finaly youtube City of Port au Prince/Mauricious wanategemea utalii only ka nchi size ya Zanzibar another eye opener kote huko good governance kama ya Kagame!after then! U can just challenge a motion tabled kwa JF with concreate examples!kuna wakati MTN RWANDA(vodacom ya kwao) wakawa mara networkdown/call ended/mara mtandao haupatikani/mara network busy/KAGAME aliwambia wasouthafrica anawapa 48hrs hataki kuona such ushenzi ama sivo watoe mitambo yao alete a best kampan ya simu toka Europe mbona wakawa perfect hao MTN RWANDA hata siku moja hamna manetwork error/problem tuliozoea Bongo kwa kampun zao za sim !lastly umeme hakunaga kukatika ovyo ovyo kama bongo!kuna dharura wanatangaza! Umeme wao hau pungui mara kuongezeka ghafla kama wa bongo upo stable always! Wow the Next SOUTH AFRICA of East Africa!
 
umesahau kuuliza kwa nn anawabagua wahutu, mfano hoteli uliyo lala wahudumu wote ni watusi.

Ukiwa Mtusi ni rahisi kujua kama hotelini kuna mtusi au mhutu, na ukiwa mhutu hali kadhalika mpaka hapo labda na wewe ni miongoni mwao, Kabila huambatana na Lugha ya kabila husika, Rwanda ni ya wanyarwanda na wanaongea kinyarwanda hakuna lugha ya kitusi au ya kihutu... wengi wetu huangalia maumbile ili kuwatofautisha na ukiwa sio mbaguzi huwezi kuwajua kwa kuwatofautisha.... kama ni urefu hotel niliyolala wako wafupi na warefu sasa jijajua kama niwatusi au wahutu
 
Atakuja mtu hapa naye atasema jaman ondoen misconception mliyo nayo dhidi ya waarabu, waisrael,wachina n.k huu nao ni aina ya ibaguzi flan hivi. Ukisoma katikati ya mistari utaona kuwa huu wote ni ubaguzi tu. Ukishasema watu flan tayari umewabagua. Nami nataka niwaondoe watu misconception kuhusu mimi.Si kweli kwamba nmetembea sana na dada zenu. Ni wao wenyewe huwa wanataka niwacheck n.k na pia watunatufikiria vibaya sisi kabila letu kuwa tunapenda sana ku drill...hamna basi tu inatokea sabab ya mambo mambo flan. Anyway....tusiendeleze ubaguzi. Mi ninachojua kila taifa lina watu wazuri na wabaya.wema na wakatili,wakorof na watulivu sikuwah kufikiria kuwa rwanda ina tatizo maaana. Nmekaa na wamarekani,wa uk,waisrael, canada,south africa,kenyans,norway, na nimeona ni watu wema na wabaya wapo pia kama tanzania,rwanda,burund,kenya n.k
Eti dada zenu!!!!
 
Tukiachana na Kagame kuijenga Rwanda lakin spirit yao haija badirika. Na haita badirika. Maana vita haijahisha. Kuna Mtoto Wa Abyalimana aliyetoroka na ndege za kijeshi bado wanaishi. Wakimbizi Wa kambi za maeneo ya kigoma walitoroshwa na ndege waliko kwenda hatujuhi. Kuna mambo mengi ukitaka kuyajua jitahidi kufuatilia.
 
......Wengi wenu kama sio wote mnadhani kuwa wanyarwanda ni watu ''wasio poa'' au ni wenye majivuno labda wengine mnadhani eti hawatupendi Watanzania.
.........huyu mzee alijua mimi ni Mkongo,
Ndugu yangu hapa HUELEWEKI kabisa. Unachosema NININI? Kuwa wanyaRwanda hawawapendi watanzania? Upendo ulioupata ulikuwa FEKI kwa sababu WEWEMwenyewe ULIFEKI maisha yako kwa dhana hiyohiyo ya woga. Ulijifanya Mkongomani. Je, unadhani huyo muzee angekununulia thubu kama angejua hakika wewe ni Mtz?
Maelezo mengine uliyotoa..(mf. namba 2 mpaka 5) hayana MAUDHUI ya kichwa cha habari yako...
Nakushauri ukirudi tena Rwanda (kama umeshatoka huko) ujitambulishe kama Mtanzania na uone watakavyo kuchukulia, kisha utwandikie kutupa mrejesho...
 
Back
Top Bottom