Oneni huyu shabiki wa nyuma mwiko alichowaandikia Al masry.

Geranimo E K I A

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2018
Posts
3,254
Reaction score
5,392
Screenshot_20250403-215529_Chrome.jpg
 
Kuna wakati nawaza Simba ikifika hatua hizi, icheze mechi zake zote zinazobaki nje ya nchi. Chuki na roho mbaya dhidi yake ni kubwa saana.
Watanzania akili hazipo
Watu wana kiherehere
Watu hawaangalii maslahi wa nchi wana ushabiki tu
Hizo shutuma kama zipo inafaa zibaki Siri ya ndani tujuane sisi Kwa sisi
 
Inasikitisha aisee sijui mtu kama huyo anapata faida gani

Watanzania akili hazipo
Watu wana kiherehere
Watu hawaangalii maslahi wa nchi wana ushabiki tu
Hizo shutuma kama zipo inafaa zibaki Siri ya ndani tujuane sisi Kwa sisi
Kuna watu wengine wanashindwa kutofautisha matani tuliyonayo na kuwa na roho mbaya.

Leo nimemsikia mshabiki wa Yanga anasema swaumu yake kama imepokelewa na Mungu anamuomba Simba isivuke kwenda nusu fainali, mambo gani sasa hayo?

Ni jambo moja kutopendelea upande wa pili usifanikiwe, ila kufikia hatua ya kumuomba Mungu, kufanya ushirikina au kuwapa mbinu maadui kama huyu mpuuzi alivyofanya ili mtani wako ashindwe kupata mafanikio ambayo hayana uhusiano wowote na timu yako, hapo unakuwa umefuzu kuwa mchawi grade 1. Tutoke huko!
 
Utani utakuwa uhasama
 
Utani utakuwa uhasama
Natamani sana baada ya hili sakata la derby kuisha, Simba na Yanga kama timu kongwe zaidi Tanzania zikae chini pamoja kiroho safi kabisa, zijenge mfumo mpya wenye tija kwa mpira wetu. Kuna mambo ya kizamani na kishamba inabidi tuachane nayo. Wakijenga mfano bora, wengine wote ikiwemo mashabiki watafuata.

Nimewahi kusema humu ndani zaidi ya mara ya moja, tufikie wakati tushirikiane kimataifa au kama inashindwa kushirikiana basi usimuwekee mwenzio vizingiti katika harakati zake za kufanikiwa. Ni ngumu lakini inawezekana.
 
Hakika
Huwezi kwenda Egypt kucheza dhidi ya Ahly, Zamalek wakakupa mbinu

Huwezi kwenda Congo kucheza na Tp Mazembe, As Vita wakawa na muda na wewe

Huwezi kwenda Morocco kucheza na Raja, Wydad wakawa na habari na wewe

Huwezi kwenda South Africa kucheza na Orlando, Kaizer chiefs wakawa na muda na wewe

Huwezi kwenda Rwanda kucheza na APR, Rayon sports wakawa na muda na wewe

Ila hapa tutapokea wapinzani hadi wapinzani wanapata hali Fulani ya kujiona wenyeji
 
Wengi hatujaelewa faida pana kwa nchi kutokana na mafanikio ya nchi kimpira
 
Back
Top Bottom