Oneni huyu shabiki wa nyuma mwiko alichowaandikia Al masry.

Oneni huyu shabiki wa nyuma mwiko alichowaandikia Al masry.

Kuna wakati nawaza Simba ikifika hatua hizi, icheze mechi zake zote zinazobaki nje ya nchi. Chuki na roho mbaya dhidi yake ni kubwa saana.
Mnasahau mapema sana, mechi zote za Yanga, mashabiki wa simba walikuwa wakiwaandikia ujumbe timu pinzani za Yanga
 
Natamani sana baada ya hili sakata la derby kuisha, Simba na Yanga kama timu kongwe zaidi Tanzania zikae chini pamoja kiroho safi kabisa, zijenge mfumo mpya wenye tija kwa mpira wetu. Kuna mambo ya kizamani na kishamba inabidi tuachane nayo. Wakijenga mfano bora, wengine wote ikiwemo mashabiki watafuata.

Nimewahi kusema humu ndani zaidi ya mara ya moja, tufikie wakati tushirikiane kimataifa au kama inashindwa kushirikiana basi usimuwekee mwenzio vizingiti katika harakati zake za kufanikiwa. Ni ngumu lakini inawezekana.
Swala sio simba na yanga kukaa chini. Yanga wana roho mbaya, chuki na husda kwenye mafanikio ya simba. Rejea matukio ya yanga kwenye kuwapokea wageni airport, manara kuwaambia wapinzania wasinywe maji ya simba etc. Ila hayo yote bure wanakuja kufa nyingi sana hapa
 
Hakika
Huwezi kwenda Egypt kucheza dhidi ya Ahly, Zamalek wakakupa mbinu

Huwezi kwenda Congo kucheza na Tp Mazembe, As Vita wakawa na muda na wewe

Huwezi kwenda Morocco kucheza na Raja, Wydad wakawa na habari na wewe

Huwezi kwenda South Africa kucheza na Orlando, Kaizer chiefs wakawa na muda na wewe

Huwezi kwenda Rwanda kucheza na APR, Rayon sports wakawa na muda na wewe

Ila hapa tutapokea wapinzani hadi wapinzani wanapata hali Fulani ya kujiona wenyeji
Big up sana👊
 
Back
Top Bottom