Ongezeko holela la vinywaji vikali na baridi,huenda ndio chanzo cha ugonjwa wa kisukari kwa vijana wadogo

Ongezeko holela la vinywaji vikali na baridi,huenda ndio chanzo cha ugonjwa wa kisukari kwa vijana wadogo

Chinga One

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
11,494
Reaction score
12,466
Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na wimbi la vinywaji vya sukari na pombe ambazo havina viwango na vinauzwa bei rafiki ambayo hata watoto wa shule wanamudu kununua huko mitaani.

Ukichunguza sana hivi vinywaji havina hata TBS na vingi ni feki yani vinatengenezwa na viwanda vya kificho bila kufuata taratibu na kanuni za utengenezaji wa bidhaa zinahusu afya ya mlaji.

Huenda vitu hivi ndio vinavyosababisha ongezeko kubwa la ugonjwa wa kisukari kwa vijana wadogo kabisa,maana tulizoea miaka ya nyuma ugonjwa huu unawakumba wazee kutokana na sababu mbambali lakini siku hizi ni kawaida kabisa kukuta kijana wa miaka 15-25 anaumwa kisukari.

Mamlaka zinazohusika zichukue jitihada stahiki kudhibiti vinywaji feki mtaani wanaoumia ni watoto wetu.
 
Kuna yule mkemia aliandika juu ya dosari ya vinywaji toka Azam nk akashambuliwa sana
Azam na Mo ni vinara wa bidhaa za vinywaji vyenye kemikali...they are killing us!
 
Biashara hizo za pombe chafu zisizo na viwango ni mkakati maalum wa kuangamiza vijana masikini wengi wasio na kazi wala ajira. Tuwaelimishe vijana waache kutumia sumu. Wakishupaza shingo achana nao.
 
Uangalizi yakinifu unatakiwa kwa watoto wadogo, kama mzazi usiruhusu wala kukubali vinywaji vyenye sukari nyingi hasa hivi vya bei rahisi, viwe ndo vinywaji pendwa vya mwanao.

Kwa watu wazima nadhani kila mmoja ana uelewa juu ya uhatari uliopo kwenye pombe kali na hata hivi vinywaji vingine, siku zote asiye sikia la mkuu huvunjika guu.
 
Kuna kampeni inaendelea ya kuwamaliza vijana

Wanatumia Mpira ,pombe na sasa ngono
Pombe, ngono, Mpira, kamali vinashusha vichocheo kama Dopamine, Serotonin, Oxytocin na endorphins.

Hivi vichocheo vikiwa chini vinasababisha energy ya mtu kuwa chini hatimaye hata uwezo wa kufanya maamuzi sahihi na kufikiria unapungua.
 
Back
Top Bottom