Ongezeko la ajali barabarani linahusiana na kauli ya kuondoa trafiki barabarani?

Ongezeko la ajali barabarani linahusiana na kauli ya kuondoa trafiki barabarani?

Hakuna popote trafic wamekuwa wakizuia ajali za barabarani nchi hii badala ya kujikita kwenye rushwa barabarani.
Sikia!.

Madereva walikuwa wanaenda kwa mwendo pole sababu ya uwepo wa trafic kila sehemu, maana wanaogopa kupigwa fine!

Hivyo ndivyo ajali zilikuwa zinazuiwa!

Asie ona hili ni mpumbavu
 
Barabara mbovu siku zote, sasa nini kimebadilika na kufanya ajali ziongezeke?
Tukubali tusikubali hizi ajali zinavyoongezeka kuna uhusiana na mambo ya kiroho au Mungu. Kuna kitu viongozi wetu wa kitaifa wamefanya kikamchukiza Mungu. Na vifo vimeongezeka sio ajali kubwa kubwa tu. Hata mauaji yasiyodhaniwa tunayashuhudia. Kumbuka mauaji ya albino yalivyoshamiri. Sababu ni zile zile za hizi ajali. Mbona mauaji ya albino yaliisha viongozi wale walipoondoka? Walioingia wakati ule wameondoka wakaingia hawa wenye nchi yao tunashuhudia vifo vinatapakaa mara ajali mara ndugu kwa ndugu. Polisi, sheria nk havitakomesha. Tufahamu tulichomkasiridha Mungu tutubu kweli kweli. Hata hii hali ya hewa ni matokeo ya kumkosea Mungu.
 
Hivi karibuni kiongozi wetu mmoja "aliteleza" na akasema kwamba trafiki wamekuwa wengi barabarani. Watu wengi walishangilia. Ila militia shaka.

Naona ongezeko kubwa la ajali za barabarani baada ya tamko Hilo, nadhani kuna uwiano wa kauli hiyo na matukio ya ajali, trafiki wamepunguzwa barabarani, Sasa madereva wanajiachia bila woga, na wananchi wanakufa kwa ajali

Nadhani Polisi waachwe wafanye kazi yao kitaalamu, mapungufu yalikuwepo, lakini maisha yaliokolewa
Kwa Nini wasiweke kamera za kudhibiti mwendo maeneo.mengi husika! Pesa ya kuiba wanayo na za kutembea kutizama kila Kona na safari. Tunashindwa Nini??
 
Hakuna uhusiano wa ajali barabarani na kuwepo/kutokuwepo kwa trafiki barabarani. Trafiki hawakuwa na kazi nyingine zaidi ya kujipatia pesa za ubwete
 
Back
Top Bottom