DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Ndani ya kipindi kisichozidi miezi miwili Kata ya Kemondo imeshuhudia ajali 3 za barabarani zilizoua watu watatu, kufuatia matukio haya ya ajali Afisa Tarafa ya Katerero iliyopo Bukoba mkoani Kagera Ndugu Bwanku M Bwanku, Ijumaa Oktoba 3, 2025 ameongozana na Polisi Kata wa Kemondo Afande Huruma Kulinganila pamoja na Watendaji kupita kijiwe kwa kijiwe ndani ya Kata ya Kemondo kutoa elimu ya kukabiliana na ajali.
Afisa Tarafa Bwanku akiwa na Polisi na Watendaji walihimiza bodaboda kuacha mwendokasi kwani ndiyo husababisha madhara makubwa hata ajali ikitokea, kuvaa kofia ngumu maarufu kama helmet ili hata ajali ikitokea kupunguza madhara kwa mtu pamoja na kuhamasisha bodaboda kukanyana pindi mmoja wao akiwa na tabia hatarishi kama mwendokasi n.k.
Kwenye ziara hiyo ya Afisa Tarafa na Watendaji, walihimiza pia bodaboda na wananchi wengine kuendelea kulinda amani na utulivu hasa nyakati hizi Taifa likielekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu na kupuuza wale wote wanaohubiri maandamano na machafuko.