Mkuu
Msanii ,japo siungi mkono matumizi ya lugha kali ya machukizo na matukano kwa kutumia maneno "huu upumbavu wa EWURA", kwasababu whatever EWURA does ni kwa mujibu wa mamlaka yake, sio busara kumtukana mtu mpumbavu wakati anatimiza wajibu wa kwa mujibu wa mamlaka yake!, mtukane aliyetunga hayo mamlaka!.
Ila ume raises a very important issue ya kitu kinachoitwa the doctrine of Separation of powers check and balance kati ya mihimili ya serikali, Bunge na Mahakama.
Bunge ndio mhimili wa kutunga sheria na kuisimamia serikali, Mahakama ni mhimili wa kutafsiri sheria na kutoa haki, serikali ni mhimili wa kutekeleza sheria na kuzihudumia Bunge na Mahakama.
Lakini serikali kupitia by laws inatunga sheria na kupoka madaraka ya Bunge, na mamlaka za Udhibiti zina quasi judicial bodies ambazo zimepoka mamlaka ya Mahakama kwa kusikiliza mashauri na kutoa maamuzi final and conclusive kitu ambacho is not right!.
Huu ni ujinga, only Spika Sitta ndio aliwahi kuukemea, EWURA ilivifungia baadhi ya vituo vya mafuta kwa hoja ya kuuza mafuta machafu. Uamuzi huo ulikuwa ni final and conclusive. Wenye vituo wakalalamika Mahakama kuwa aliyewaletea mafuta machafu ndie awajibike na aadhibiwe, mahakama iamuru EWURA wavifungulie!, EWURA wakatia pamba Masikioni na kugoma kuvifungua. Spika Sitta akaingilia kati
kuwa ni Mahakama Kuu pekee ndio yenye mamlaka ya kutoa maamuzi final and conclusive!, ila kuvifungulia kuendelea kuuza mafuta machafu sio uamuzi wenye maslahi kwa taifa hivyo Spika Sitta akaikomelea Mahakama, Jaji Mkuu wa wakati huo, Jaji Agustino Ramadhan akasema Spika Sitta ameghafilika, Bunge lina uwezo wa kuisimamia serikali tuu na sio kuingilia Mahakama!, Spika Sitta akajibu mapigo kuwa ni Jaji Mkuu ndiye amefilisika, mamlaka Kuu ya nchi ni katiba, na katiba hiyo inapata mamlaka toka kwa wananchi ndio wenye katiba, hivyo Bunge ndilo wawakilishi wa wananchi, Mahakama inapotoa maamuzi ya ajabu ajabu ambayo hayana maslahi kwa taifa, Bunge haliwezi kunyamaza!. Spika Sitta alisema kati ya mihimili mitatu ya dola, mhimili wa Bunge ndio supremacy!.
Spika Sitta alishitakiwa kwenye chama ili anyanganywe kadi ya CCM!, JK akamnusuru, ila alipogombea tena uspika, CCM wakampiga chini kwa hoja ya kumjaribu Mwanamke!.
Spika Sitta: Kelele za Kingunge hazininyimi usingizi
P