Samcezar
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 13,095
- 22,731
Muda mwingine nasema wacha tuangamie kwasababu tumechagua kuwa kimya.Pale rushwa inaposhindwa kudhibitiwa katika nchi madhara yake ndio hayo!! Watu wa maliasili wametajirika kupitia misitu, mkaa malori kwa malori yanaingia miji mikubwa kila siku!! Uliza sasa huo mkaa na mbao zimeingiaje,yaani ni rushwa mwanzo mwisho kwenye mageti ya maliasili.Serikali isipomulika idara ya maliasili hali itaendelea kuwa mbaya zaidi.
Haya mazingira tumeyakuta na tutayaacha. Miti ikiisha ikatoweka maji yatapotea ukame utatokea watu watakufa kaa njaa na miili yao itakuwa mbolea ya ardhi then dunia itaanza kujiumba tena na misitu ya miti na mapori itaota tena.
So vyovyote tunavyofanya dunia haipati hasara ni vizazi vijavyo ndio watalipia kwa viburi vyetu na watalipia kwa gharama kubwa sana.