Ongezeko la joto nchini, picha ya Mlima Kilimanjaro leo

Ongezeko la joto nchini, picha ya Mlima Kilimanjaro leo

Npo kilimanjaro..kijijini kwetu ambapo bili ya maji kwa mwaka ni shilingi 1000, kijiji kinaitwa nkweshoo. Lkn hali kwa ss ni mbaya kwani maji yamekuwa kidogo sana..na nikiangalia mlima kilimanjaro hakuna ile kitu nyeupe..na kijiji chetu ndio cha mwisho baada ta hapo ni msitu alafu mlima....sasa kama mimi napata taabu ya maji je huko dar..na kwengineko hali ipo aje..? Wadau nini kinaendelea kwenye hili zulia la tz?
Hata maeneo mengi ya machame hakuna maji, ni jambo ambalo haijawahi tokea miaka yote
 
Mabadiliko ya tabia nchi, tuendelee kuharibu mazingira... mazingira yatatulipa sawasawa na tunavyoyaharibu. To every action.......!
There is an equal and opposite reaction! ha ha ha
 
View attachment 2013193
Barafu inayeyuka kabisa kileleni.

Mungu atunusuru
Kuna uwezekano pia kuwa huko chini ya mlima kuna lava ambayo imeshaanza kupandisha juu ili itoke na hivyo imepelekea uwepo wa joto kubwa kileleni. Kumbuka kuwa Mlima Kilimanjaro una volcano iliyolala na ambayo ina uwezo wa kulipuka muda wowote ule
 
Suluhu ni kupanda miti hata ifike 1b na liwe lengo haswa
Serikali iwekeze kwa uhakika na sio Dili kwa baadhi ya wakubwa bali iwe muendelezo

Wote wanaojihusisha na Kilimo kinachohusu ukataji wa miti walazimishwe kupanda miti mingi na mbegu au mashina wapewe bure ila walipe wapandaji

Wafugaji wote wapewe miti na waitunze kwa lazima
Vijijini na kila kaya wapande miti
Hata pembezoni mwa barabara zetu

Vyanzo vya maji vilindwe sana
Wenye viwanda wakimwaga chemicals zao kwenye mifereji wapigwe faini yenye nusu ya thamani ya kiwanda chake na wanapopewa licence masharti yote yawemo

Watu wanaona ni jambo la kawaida ila ni janga kubwa sana

Wajukuu watatulaani sana tusipotetea ardhi leo

Mawaziri wawe serious sio majungu tu waje na mikakati
Kama wanazunguka na mabakuli hela zipo nje nje kuhusu tabia nchi

Je Mama kapata ngapi huko Scotland?
Mimi naogopa sana maana Waafrika hatuko makini tunajali sana maslahi binafsi kuliko maslahi ya walio wengi.
Ni rahisi kupokea rushwa kwa maslahi binafsi huku wengi wakiteketea!!!
 
Jamaa anakuambia Mungu atunusuru wakati kila mwaka iyo hali inatokea
Hii hali ni tofauti hii hali italeta ukame mkubwa sana na hata mvua ikijanyesha itakuwa sio mvua ya kawaida 2022 utakuwa mwaka mgumu sana yajayo yanatisha.
 
Mimi naogopa sana maana Waafrika hatuko makini tunajali sana maslahi binafsi kuliko maslahi ya walio wengi.
Ni rahisi kupokea rushwa kwa maslahi binafsi huku wengi wakiteketea!!!

Hilo lipo sana kwa nchi masikini na tatizo ni mifumo mibovu ya kulindana

Mabunge yanaogopa kuweka sheria ngumu kwa sababu wao ndio wavunjaji wakubwa wa sheria

Angalia mtu anakuwa Rais halafu anasema tu kuanzia leo fulani analindwa kutokushtakiwa sasa hapo unategemea nini
 
Back
Top Bottom