Ongezeko la kuvunjika Ndoa, natoa RAI kituo Jumuishi cha Taifa cha Familia - Temeke kichunguzwe

Ongezeko la kuvunjika Ndoa, natoa RAI kituo Jumuishi cha Taifa cha Familia - Temeke kichunguzwe

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
59,045
Reaction score
94,974
Sipingi Watu kutengana kwa kukubaliana kutokukubaliana, LAKINI inafikirisha zaidi pale unapogundua kuwa "kuachanishwa" kwenu kulikua na nguvu flani nyuma yake.

Katika pita pita Zangu mara kadhaa nimeona kituo hiki kikitajwa kuwa na "Vishoka" kama ilivyo sehemu nyingine kama TANESCO ambao hufuatilia na kujua Mali zilizopo kwa huyo anayetakiwa "kupewa talaka" na wakishajua huwa wanajenga mazingira ambapo madalali wanakua standby kuuza Mali hizo ili mgawane.

Maana yake ni kwamba, Leo hii ukienda pale hata kama kuna namna ya kuokoa "Umoja" huo tayari kunakua na "ushawishi" mwingine WA kukujengea Tamaa ya kupata "mgao" mzuri mara baada ya talaka kupatikana! Kinachoumiza ni kwamba mara nyingi victims ni Wanaume ambao Mali hizo huzipata kwa gharama kubwa ya maisha Yao, na waathirika WA pili wakiwa ni Watoto.

Naomba Sana Serikali ichunguze Jambo hili, tusione fahari idadi ya ndoa zinazovunjwa kuongezeka.

IMG-20240523-WA0035.jpg
 
staili yake hiyo ndio wanaume wanaiga. Kaoa tena ila huyo mke wake mpya akileta za kuleta hataambulia kitu
Sijajua sheria za ndoa zinasemaje kwabongo kuhusu kumilikisha mali mnazochuma kama familia ya ndoa yamungu mtu mwingine,mimi nimilikishe mama yangu na akifa kwahapa bongo dingi anaweza asikuelewe na unakuta unamadogo nunda
 
wanaoandikisha mama zao ni wale wasiokuwa na baba, yaani baba zao walishakufa kabla hawajaoa. Wanafanya hivyo kukwepa kupata hasara pindi ndoa ikivunjika
 
wanaoandikisha mama zao ni wale wasiokuwa na baba, yaani baba zao walishakufa kabla hawajaoa. Wanafanya hivyo kukwepa kupata hasara pindi ndoa ikivunjika
Naona hata kama baba yu hai heri anifirisi yeye lkn sio mwanamke wangu inauma mno.. Imagine Boss wangu mke wako anaolewa ukiwa bado upo hai na anaishi kwenye nyumba uliyojenga wewe. Inauma inauma inauma mnoo
 
Back
Top Bottom