Ongezeko la kuvunjika Ndoa, natoa RAI kituo Jumuishi cha Taifa cha Familia - Temeke kichunguzwe

Itungwe sheria mpya ya talaka na mirathi kama mwanandoa mmoja akiamua kuondoka ndoani aondoke tu bila kutaka kugawana mali. Mali zitabaki kwa mwanandoa anayebaki na watoto wake/mali zibaki kuwa ni za watoto tu. Kama ndoa haina watoto basi mali alizokuwa nazo mwanandoa kabla ya ndoa zibaki kwake, zile zilizopatikana wakiwa pamoja ndio wagawane.
 
Sheria ya ndoa inahitaji marekebisho, sijawahi sikia mali za mke kugawanywa ila zinagawanywa mali za mume pekee, huu ni wizi wa mchana kweupe.
Hapana nitarekebishwa kama nakosea

Malizote zinazochumwa au zilizochumwa kabla hamjaoana pandezote mbili haziingii kwenye mgao isipokuwa zilezote mlizoanza kuchuma kutoka siku mmetoka kanisani au vyovyote vile ,ilimradi mazingira yanathibitisha ni wanandoa
 
Polisi ndo wanatuchelewesha harafu wao ndowahanga namba moja ,badala wawambie serikali imetosha sheria hizi zimepitwa na wakati wao wapo tuuuuuu
 
Unaamini mchango wa kuchuma hizo mali mkiwa ndani ya ndoa, huwa una uwiano wa 50/50 kwa pande zote?, kama sivyo kwa nini mgawane 50/50 baada ya ndoa kuvunjika?
 
Hizo taasisi za kutetea wanawake hili suala huwezi kuta wakijadili
 
Hio ni Kenya, nasikia Bongo ni mali zote
 
Unaamini mchango wa kuchuma hizo mali mkiwa ndani ya ndoa, huwa una uwiano wa 50/50 kwa pande zote?, kama sivyo kwa nini mgawane 50/50 baada ya ndoa kuvunjika?
sheria,zimeundwa kukilinda kizazi chakike , kutokana na mfumedume wetu

Sawa
Tujiulize wakati wewe uko kusaidia fundi ujenzi huko ,ukirudi unakuta nyumba chafu ,watoto wachafu kama hapana nayeye kafanya kitu au kwamkunga kukushushia wanao nayo kazi mkuu
 
Naonaga TU Lile jengo kwa mbali 😊😊
 
Kikubwa kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake.
Ukichangia 5% basi ondoka na 5% yako usitake 50%.

Kwa sasa mnahimiza haki sawa kwa wote, iweje muendeleze sheria kandamizi kwa mwanaume wakati wote wana haki sawa?.
 
Pale sheria zinaporuhusu wahuni 'kushangilia' na kunufaika familia zinaposambaratika.
Ni ishara wazi kuwa hao wanaoitwa wasukuhishi, si wasukuhishi bali wanufaike wa migogoro ya ndoa
It's so sad!
 
Pole sana mkuu. Yamekukuta nini? Nchi hii opportunists wapo kila kona. Chukua tahadhali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…