Ongezeko la mabinti (wanawake) waliochora tattoo sehemu mbalimbali za miili yao, nini tatizo? Haliwezi kuhatarisha makuzi ya mabinti wa kesho?

Ongezeko la mabinti (wanawake) waliochora tattoo sehemu mbalimbali za miili yao, nini tatizo? Haliwezi kuhatarisha makuzi ya mabinti wa kesho?

Kwa nini unataka kupangia watu baki jinsi ya kuishi?

Mtu mwili wake, kaamua kuchora tattoo kivyake, wewe unajiwekaje ukiranja wa kumpangia afanya na asifanye nini?

Unamlinda mtu kivipi ukimzuia asichore tattoo?

Yani kama mtu anakwenda kuwa na mawazo mabaya ukimzuia asichore tattoo ndiyo hayo mawazo mabaya yatashindwa kumuingia?

Kwa nini unajiona wewe una wajibu wa kuwapangia watu baki nini ni sawa wafanye na nini si sawa wasifanye?

Wewe mtu ambaye nchi yako ina matatizo ya chakula, malazi, mavazi, elimu, magonjwa, kazi, na mengine kemkem, mighorofa inaanguka na kuua watu huko Kariakoo, watu wanakufa kwa kipindupindu Simiyu, maana yake wanakunywa maji yenye mavi ya watu, hivi tattoo ndiyo umeona ni tatizo kubwa kabisa la kulivalia njuga?

Kweli jamani? Tattoo?
Mkuu jifunze kuheshimu mchango wa mawazo ya mtu. Kwanini afikirie mambo uliyoorodhesha hapo wakati hayo kuna Mamlaka zipo na zinaweza kuyasimamia ?
Hili la tatoo nalo lijadiliwe aisee.
 
Watanzania wengi kama mtoa mada wanajali sana muonekano wa watu wa nje, kuliko fikra za ndani za hao watu.

Ndio maana majambazi yanayovaa suti na kufanya wizi wa kalamu maofisini yanawaibia mamilioni kika siku. Wala hayasumbuliwi sana.

Halafu vijana wenye roho safi tu walio na muonekano wa nje unaochukuliwa kuwa ni mbaya, kama kuwa na dreadlocks au tattoo, wanapigwa vita sana bila sababu ya muhimu.

Muhukumu mtu kutokana na matendo yake, si kutokana na muonekano.

Huo muonekano wa nje ni rahisi sana kwa mtu mbaya kujipa muonekano ambao wewe unaufikiria ni mzuri, na pia ni rahisi sana kwa mtu mzuri kujipa muonekano ambao kasumba zenu za kibongobongo zinauona kuwa ni muonekano mbaya.

Ila watu wenye akili ndogo hawawezi kuishinda kasumba ya kuangalia muonekano wa nje bila kujali undani wa mtu.
 
Mwamba angekuwepo hapa angekuwa anawaangalia anacheka tu hiiii
1000016414.jpg
 
Mwamba angekuwepo hapa angekuwa anawaangalia anacheka tu hiiii
View attachment 3161642
Watanzania wengi hawajui maana ya uhuru.

Wamezoea kupigwapigwa na kuswagwaswagwa kama ng'ombe. Kwa sheria za kijingajinga tu

Tangu watoto.

Wakikutana na watu wanaoanza kuutumia uhuru wao wa kujieleza kidogo tu, wanaona hili ni tishio.

Wanaanza kuburuzana wenyewe kwa wenyewe kupangiana sheria zisizo na kichwa wala miguu.

Ndiyo maana mara nyingine nasema hata hiyo katiba mpya sijui kama itawasaidia kitu.

Kwa sababu haki za katiba hii ya sasa na haki za kibinadamu bado hawazielewi.

Na wao wenyewe wanaminyiana haki zao.

Kwa mfano hapa tattoo ni sehemu ya haki ya self expression tu, haki ya kikatiba na kibinadamu.

Ila Tanzania tattoo kwa watu wengi ni kipengele.
 
Mkuu ni kweli Tattoo zinashamiri sana!

Ila siyo bongo tu, ni Dunia nzima!

Aidha, kushamiri kwa Tattoo kunaenda sambamba na watu kuweka vyuma mwilini, na mapete fulani vidoleni.

Wapo wanaoweka Tattoo kama urembo na mara nyingi huwa under 25.

Lakini wengi wanoweka tattoo, wanaojitoba pua, wanaotoboa matundu zaidi ya moja masikioni tena wakiwa watu wazima huwa ni kutekeleza takwa la imani fulani.

Ukimuona mtu ana combinations ya Pete ya ajabu, pua katoboa kama ambaa luluu, masikioni ana matundu kadhaa na ana tattoo ya mdudu/mnyama/ndege chukua taadhari. Ukijichanganya tu ukakuchomekwa au ukamchomeka imekula kwako mazima!

Bila Mungu peke yetu hatuwezi!

Mungu vilinde vizazi vyetu.
 
Habari ndugu wana jamvi,

Leo nimekuja na jambo ambalo linaweza kunipa wasiwàsi kwa namna moja au nyingine.

Kama jamii hivi Sasa ,kumekuwa na wimbi kubwa La wadada ,wasichana na wanawake kujichora tatoo Katika miili Yao.

Na tattoo hizo mara nyingi uchorwa sehemu ambazo inakuwa rahisi kwa MTu kuweza kuiona.

Jambo ilo baadhi yetu tumeliona kamq tishio kwa makuzi na kizazi kijacho ,kuona tattoo ni sehemu ya furaha,urembo ,na lazima Katika miili yao.

Biła kujali hasara za tattoo hizo, mabinti WENGI wamekuwa wakichora kila uchwao.

Siingilii uamuzi ,wała furaha ya MTu Bali najaribu kuona je tunawezqje kuwalinda watoto wadogo na aina Hii ya makuzi wakiwa wanajionea walezi,mama ZAO,Dada NK wakiwa wamejichora.

Asanteni wanajamvi🙏🏿
Umeenda club,kwenye madanguro na makasino,......baaasi una fikia muafaka kua mabinti wengi wapo hivo?.......this is fallac of generalization
 
Niliwahi kuwa obsessed once nikiwa na binti toka mbalala ug yeye alikuwa nayo moja begani ila baada ya kuikumbuka leviticus 19:28
 
Leviticus 19:28
"You shall not make any cuts on your body [in mourning] for the dead, nor make any tattoo marks on yourselves; I am the LORD". This passage prohibits tattoos, likely because they were associated with pagan practices.
 
Hata ukiangalia wacheza mpira wa siku hizi,
wengi wamejichora Tattoo ukilinganisha na wachezaji wa zamani,

Moja ya sababu pia ni kukua kwa teknolojia,imekua rahisi sana kuchora Tattoo kwa vifaa vya kisasa ukilinganisha na teknolojia ya zamani,

Kila zama na kitabu chake.
 
Mwanamke hata awe mzuri kiasi cha pekee, akishakuwa na tattoo kwangu Mimi thamani yake imeshaporomoka namchukulia kama chuda fulani
 
Almanusura nimchore mtoto wa mtu kwenye paja, nakumbuka mchora tattoo kaja yeye kachora imefika zamu yangu roho ikakataa, nashukuru sana uamuzi ule japo bado tupo wote lakini naifikiria sana kesho kutwa yangu,

Mdau aliyesema ni generation yao yuko sahihi kila zama na vituko vyake, huenda ikafika kipindi asiye na tattoo anatengwa 😂
Tempo tatoo kama ina haina tatizo ukitaka unaifuta, ila ile permanent ni kimeo.

Kuna demu baba yake alikuwa mtu mzito kwenye majeshi yetu, post zílipotoka akampeléka binti yake kumbe mwilini ana tatoo, ilishindikana kuandikishwa jeshini hawaruhusu kabisa tatoo wala wasenge wala unfit.
 
Leviticus 19:28
"You shall not make any cuts on your body [in mourning] for the dead, nor make any tattoo marks on yourselves; I am the LORD". This passage prohibits tattoos, likely because they were associated with pagan practices.
Na masanamu?
 
Back
Top Bottom