Ongezeko la mabinti (wanawake) waliochora tattoo sehemu mbalimbali za miili yao, nini tatizo? Haliwezi kuhatarisha makuzi ya mabinti wa kesho?

Mkuu jifunze kuheshimu mchango wa mawazo ya mtu. Kwanini afikirie mambo uliyoorodhesha hapo wakati hayo kuna Mamlaka zipo na zinaweza kuyasimamia ?
Hili la tatoo nalo lijadiliwe aisee.
 
Watanzania wengi kama mtoa mada wanajali sana muonekano wa watu wa nje, kuliko fikra za ndani za hao watu.

Ndio maana majambazi yanayovaa suti na kufanya wizi wa kalamu maofisini yanawaibia mamilioni kika siku. Wala hayasumbuliwi sana.

Halafu vijana wenye roho safi tu walio na muonekano wa nje unaochukuliwa kuwa ni mbaya, kama kuwa na dreadlocks au tattoo, wanapigwa vita sana bila sababu ya muhimu.

Muhukumu mtu kutokana na matendo yake, si kutokana na muonekano.

Huo muonekano wa nje ni rahisi sana kwa mtu mbaya kujipa muonekano ambao wewe unaufikiria ni mzuri, na pia ni rahisi sana kwa mtu mzuri kujipa muonekano ambao kasumba zenu za kibongobongo zinauona kuwa ni muonekano mbaya.

Ila watu wenye akili ndogo hawawezi kuishinda kasumba ya kuangalia muonekano wa nje bila kujali undani wa mtu.
 
Mwamba angekuwepo hapa angekuwa anawaangalia anacheka tu hiiii
View attachment 3161642
Watanzania wengi hawajui maana ya uhuru.

Wamezoea kupigwapigwa na kuswagwaswagwa kama ng'ombe. Kwa sheria za kijingajinga tu

Tangu watoto.

Wakikutana na watu wanaoanza kuutumia uhuru wao wa kujieleza kidogo tu, wanaona hili ni tishio.

Wanaanza kuburuzana wenyewe kwa wenyewe kupangiana sheria zisizo na kichwa wala miguu.

Ndiyo maana mara nyingine nasema hata hiyo katiba mpya sijui kama itawasaidia kitu.

Kwa sababu haki za katiba hii ya sasa na haki za kibinadamu bado hawazielewi.

Na wao wenyewe wanaminyiana haki zao.

Kwa mfano hapa tattoo ni sehemu ya haki ya self expression tu, haki ya kikatiba na kibinadamu.

Ila Tanzania tattoo kwa watu wengi ni kipengele.
 
Mkuu ni kweli Tattoo zinashamiri sana!

Ila siyo bongo tu, ni Dunia nzima!

Aidha, kushamiri kwa Tattoo kunaenda sambamba na watu kuweka vyuma mwilini, na mapete fulani vidoleni.

Wapo wanaoweka Tattoo kama urembo na mara nyingi huwa under 25.

Lakini wengi wanoweka tattoo, wanaojitoba pua, wanaotoboa matundu zaidi ya moja masikioni tena wakiwa watu wazima huwa ni kutekeleza takwa la imani fulani.

Ukimuona mtu ana combinations ya Pete ya ajabu, pua katoboa kama ambaa luluu, masikioni ana matundu kadhaa na ana tattoo ya mdudu/mnyama/ndege chukua taadhari. Ukijichanganya tu ukakuchomekwa au ukamchomeka imekula kwako mazima!

Bila Mungu peke yetu hatuwezi!

Mungu vilinde vizazi vyetu.
 
Umeenda club,kwenye madanguro na makasino,......baaasi una fikia muafaka kua mabinti wengi wapo hivo?.......this is fallac of generalization
 
Niliwahi kuwa obsessed once nikiwa na binti toka mbalala ug yeye alikuwa nayo moja begani ila baada ya kuikumbuka leviticus 19:28
 
Leviticus 19:28
"You shall not make any cuts on your body [in mourning] for the dead, nor make any tattoo marks on yourselves; I am the LORD". This passage prohibits tattoos, likely because they were associated with pagan practices.
 
Sijawahi kuona tattoo parlor Tanzania.

Zipo sehemu gani?
 
Hata ukiangalia wacheza mpira wa siku hizi,
wengi wamejichora Tattoo ukilinganisha na wachezaji wa zamani,

Moja ya sababu pia ni kukua kwa teknolojia,imekua rahisi sana kuchora Tattoo kwa vifaa vya kisasa ukilinganisha na teknolojia ya zamani,

Kila zama na kitabu chake.
 
Mwanamke hata awe mzuri kiasi cha pekee, akishakuwa na tattoo kwangu Mimi thamani yake imeshaporomoka namchukulia kama chuda fulani
 
Tempo tatoo kama ina haina tatizo ukitaka unaifuta, ila ile permanent ni kimeo.

Kuna demu baba yake alikuwa mtu mzito kwenye majeshi yetu, post zílipotoka akampeléka binti yake kumbe mwilini ana tatoo, ilishindikana kuandikishwa jeshini hawaruhusu kabisa tatoo wala wasenge wala unfit.
 
Leviticus 19:28
"You shall not make any cuts on your body [in mourning] for the dead, nor make any tattoo marks on yourselves; I am the LORD". This passage prohibits tattoos, likely because they were associated with pagan practices.
Na masanamu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…