Tetesi: Ongezeko la masharti ukitaka kufungua akaunti ya Benki lazima kuongezea kiapo cha mahakama licha ya kuwa na vitambulisho husika

Tetesi: Ongezeko la masharti ukitaka kufungua akaunti ya Benki lazima kuongezea kiapo cha mahakama licha ya kuwa na vitambulisho husika

Habari mkuu Britannica? Nashukuru sana kwa kuleta hii mada hapa jamvini, bila shaka kupitia majibu mawili matatu, watu wanaweza kujifunza kitu.
Kwanza napenda kuwapongeza serikali kupitia BOT kwa kuanzisha hili zoezi. Dhumuni la kuleta huu mchakato nikutusaidia mimi na wewe kupambana dhidi ya "Utakatishaji wa Pesa(Money laundering)". Kuwa na kitambulisho pekee haitoshi kuweza kutambuliwa maana hapa Tanzania hakuna miundo mbinu ya kuweza kuhakikisha vitambulisho vyako. Hii inamaana mtu yoyote anaweza kugushi kitambulisho na kukitumia kufungua akaunti kwa dhumuni la kutakatisha pesa. Nia ya kuonesha barua toka Mahakamani kutawarahisishia Bank kwamba vitambulisho vyako nivyakweli na sio gushi. Pia, benki wana haki kisheria kufuatilia na kukuhoji juu ya pesa zako kwenye akaunti.

Nawaomba tuwapongeze ma benk na serikali kuhusu hili zoezi. Kama kweli ma benki wataweza kulisimamia ipasavyo, tutafaidika sana kama nchi.

Asante.
Hata Mahakamani form zile watu wanatengeneza hata mihuri ya Mahakamani watu wanachonga
 
Subira Huvuta Heri Ila Ivumayo Haidumu
Mbaazi Ukikosa Maua Husingizia Jua


Sasa Watanzania
Kusikia Kwa Kenge Hadi Atoke Damu Puani Na Masikioni
 
Nakubaliana na hoja kadhaa isipokuwa suala la barua ya mahakama. Binafsi sioni kama mahakama inayomiundombinu ya kuverify vyeti, At least wangesema benki ipate verification kutoka NIDA na hiyo verification sio ya barua bali iwe system generated verification. Unaenda nida unaingiza fingerprint kuthibitisha kama ID ni yako kweli, then fingerprint zikimatch basi afisa wa NIDA anatuma system generated email kwenda benki kuwa fulani bin fulani anaruhusiwa kufungua akaunti kwa jina lake na taarifa zake ni sahihi.

Safi sana kaka nadhani ndivyo wanataiwa kufanya kama watu wote watakuwa kwenye data base ya NIDA. Nashukuru sana bila. shaka wahusika watalifanyia kazi.
 
Hata Mahakamani form zile watu wanatengeneza hata mihuri ya Mahakamani watu wanachonga

Nikweli kaka, nadhani labda barua iwe inatumwa moja kwa moja na mahakama kwenda kwa benki pasipo mhusika kujua ili kuepusha watu kugushi. Nashukuru sana kwa mchango wako mkuu.
 
Bitcoin ipo kusolve hizo adha zote.
 
TANGAZO TANGAZO Nauza vibubu vyenye ukubwa mbalimbali unaletewa popote ulipo Hata mikoani,bei nafuu wahi chako mapema
 
Huu siyo ujamaa ila ndivyo inavyotakiwa. Umewahi kufika Ulaya? Unajua masharti ya kufungua account ya benki au ku-deposit fedha nyingi ukiwa Ulaya? Sisi tumechelewa sana.
Ulaya if you have your proper id ama social security number, unafungua account kirahisi sana, ni muda wa saa moja tuu, pia unaweza kupokea any amout of funds hata mlions lakini lazima ziwe ma proper trackable records na zilingane na buashara yako.

Anything more than 10,000 usd in USA lazima utatakiwa kujieleza, na Europe nadahani more than 5000 BP ama Euros.

Hakuna cha kwenda kuhakisha kitambulisho mahakamani
 
Ila siyo deni siyo kesi,tunahamia kwenye Mobile Money labda waje na huku waseme mtu akitaka weka hela lazima akathibitishwe
 
Ujamaa huu unaharibu nchii na kuturudisha nyuma kimaendeleo.

Siujui ni wawekezaji gani watakuja kuwekeza kwenye nchi yenye sera mbovu kama hizi za ujamaa uchwara!
Huu sio ujamaa bali sheria za kipumbavu na ubinafsi wa wazizwazi.kwenye maswala ya uwekezaji huwezi kumzui mwwkezaji kutokuwa na akaunti mbili.huu ni uthibitisho kwamba serikali ya magufuli imeshindwa kubuni mbinu mbadala namna ya kuvutia investors.
 
Ulaya if you have your proper id ama social security number, unafungua account kirahisi sana, ni muda wa saa moja tuu, pia unaweza kupokea any amout of funds hata mlions lakini lazima ziwe ma proper trackable records na zilingane na buashara yako.

Anything more than 10,000 usd in USA lazima utatakiwa kujieleza, na Europe nadahani more than 5000 BP ama Euros.

Hakuna cha kwenda kuhakisha kitambulisho mahakamani
Of course ukiwa na Social Security Number Ulaya ina maana unajulika . Sasa mazingira ya huku Bongo siyo kama Ulaya. Nchi haijui raia wake ni kina nani na wako wapi. Kila ukitaka huduma lazima ujitambulishe kulingana na unyeti wa huduma. Kuhusu ku-deposit: Nchi nilizoishi HUWEZI ku deposit hata euros 1000 bila kueleza umezitoa wapi. Kuhusu fedha kuingia nyingi kwenye account: Of course kama unajulikana ni mtu mwenye shughuli ya kuingiza fedha nyingi hakuna doubt. Lakini kama fedha zilizoingia haziendani na shughuli zako ni lazima kutakuwa na kufuatilia. Tusichanganye mazingira ya nchi ambazo zinajua raia wake wote na zina-control ya mipaka yake na nchi kama zetu ambazo watu hawajulikani na wanaweza kuingia na kutoka kama chooni.
 
Hiki ni chanzo cha Tanzania kuwa na kitu knaitwa BLACK MONEY, kuna aina mbili ya blqck money.

1. Ni pesa za drugs
2. Pesa za kukwepa kodi ambazo zinakuwa zinafichwa majumbani na sehemu zingine za siri.

India inaongoza sana kwa Black Money, matajiri wakizeweka hizo pesa mabenki India, basi benki zitafurika.

Tulumbuke enzi ya Sokoine, watu walitupa magunia ya pesa mitoni na porini.

Tuna rudi a full circle to 1970s na 80s.
Siyo sasa hiyo ilikuwa zamani ndugu.!
 
Pamoja na kwamba hata kama utakuwa na vitambulisho vyoote husika lakin muhim kuwa na kiapo cha mahakamani kwa taarifa unazotoa wakati wa ufunguzi wa akaunt,

Wakati huo huo akaunt zote ambazo zitaonekana kupitisha hela kubwa kubwa zitachunguzwa na wakibaini hela inapita tu bila kuwa na uthibitisho wa hela zako, akaunt inazuiliwa, na kiasi chenyewe ni zaid ya milion 50 kwa miezi kadhaa
Kwa wafanyakazi wa ENI EMU BII ninyi ni mashahidi wamepokea waraka toka BII OO TII kwamba hakuna mtu ku deposit zaid ya milion 40 bila maelezo zimetoka wapi

Pia kwamba Huruhusiwi kufungua akaunt mbili za aina moja ndani ya benki moja kama ilivyokuwa zamani,

Stay tuned,


Britannica,
Wakumbuke kuwa kuna ambao hawana fedha kwenye akanti lakini wanajenga na kumiliki majengo yenye gharama za mabilioni .
Na wengi wao ni wanasiasa. Siamini kuwa Mali zote zilizoko nchini hasa majumba na mahoteli ni ya watu kutoka nje!!
 
Itafika wakati serikali itataifisha pesa za watu zilizo benki. Kama unafikiri tuko kwenye light tlack unajidanganya.
 
Back
Top Bottom