Tetesi: Ongezeko la masharti ukitaka kufungua akaunti ya Benki lazima kuongezea kiapo cha mahakama licha ya kuwa na vitambulisho husika

Tetesi: Ongezeko la masharti ukitaka kufungua akaunti ya Benki lazima kuongezea kiapo cha mahakama licha ya kuwa na vitambulisho husika

Jamaa linabolonga na kutinyanga nchi yetu
 
Sasa ndio utelewa maana ya kufuata vicoba na saccos na vicoba
 
Habari mkuu Britannica? Nashukuru sana kwa kuleta hii mada hapa jamvini, bila shaka kupitia majibu mawili matatu, watu wanaweza kujifunza kitu.
Kwanza napenda kuwapongeza serikali kupitia BOT kwa kuanzisha hili zoezi. Dhumuni la kuleta huu mchakato nikutusaidia mimi na wewe kupambana dhidi ya "Utakatishaji wa Pesa(Money laundering)". Kuwa na kitambulisho pekee haitoshi kuweza kutambuliwa maana hapa Tanzania hakuna miundo mbinu ya kuweza kuhakikisha vitambulisho vyako. Hii inamaana mtu yoyote anaweza kugushi kitambulisho na kukitumia kufungua akaunti kwa dhumuni la kutakatisha pesa. Nia ya kuonesha barua toka Mahakamani kutawarahisishia Bank kwamba vitambulisho vyako nivyakweli na sio gushi. Pia, benki wana haki kisheria kufuatilia na kukuhoji juu ya pesa zako kwenye akaunti.

Nawaomba tuwapongeze ma benk na serikali kuhusu hili zoezi. Kama kweli ma benki wataweza kulisimamia ipasavyo, tutafaidika sana kama nchi.

Asante.
Wapongeze peke yako mkuu.
 
Kwa mwendo huu itafika sehemu ukienda kuchukua Fedha hata milioni tatu tu ujaze fomu ya maombi wiki tatu kabla na uambatishe na mchanganuo wa matumizi wa fedha yote,

Kila leo unahubiri kuondoa urasimu wakati huo huo unaongeza urasmu zaidi ya ule uliokuwepo....!
Aisee
 
Wakumbuke kuwa kuna ambao hawana fedha kwenye akanti lakini wanajenga na kumiliki majengo yenye gharama za mabilioni .
Na wengi wao ni wanasiasa. Siamini kuwa Mali zote zilizoko nchini hasa majumba na mahoteli ni ya watu kutoka nje!!
Kuna mbinu ya kuwawajibisha pia
 
Pamoja na kwamba hata kama utakuwa na vitambulisho vyoote husika lakin muhim kuwa na kiapo cha mahakamani kwa taarifa unazotoa wakati wa ufunguzi wa akaunt,

Wakati huo huo akaunt zote ambazo zitaonekana kupitisha hela kubwa kubwa zitachunguzwa na wakibaini hela inapita tu bila kuwa na uthibitisho wa hela zako, akaunt inazuiliwa, na kiasi chenyewe ni zaid ya milion 50 kwa miezi kadhaa
Kwa wafanyakazi wa ENI EMU BII ninyi ni mashahidi wamepokea waraka toka BII OO TII kwamba hakuna mtu ku deposit zaid ya milion 40 bila maelezo zimetoka wapi

Pia kwamba Huruhusiwi kufungua akaunt mbili za aina moja ndani ya benki moja kama ilivyokuwa zamani,

Stay tuned,


Britannica,
Tatizo sio kuweka 40k, ni kutoa; tangu EPA mpaka escrow watu walitoa mabilioni wakagawana!
Sinema zingine tutapoteza senti ya popcorn bure!
 
Waulize waMarekan, kuna taass inaitwa IRS (inland revenue service)... Hao jamaa wakukute umefngua akaunti kinyemela au una dollars 1000 mknoni bila maelezo, cha moto utakiona!
Internal* revenue service under federal government sio inland
 
Tuendeleeni tu kucheka cheka tukishatumbukia hakuna wakututoa na tukitoka itakuwa karne nyingine duniani..

Aliyeiingiza Congo DRC kwenye hali iliyopo ni Mobutu Seseseko alikuwa akichekewa na wajinga waliokuwa wakifaidi keki lakini mambo yalivyoharibika hayakuchagua nani alikuwa shabiki wa nani...
Itafika wakati woote tutaungana na kudai UHURU wa kweli
 
Mkuu Britannica, asante kwa taarifa hii, kwenye ukweli unaleta za kweli kabisa tena za Moto moto kutoka jikoni, ila pia ni mpishi mzuri, ukiamua kupika, na viungo unavyo pikia, pilau na biriani zitasubiri, kama ile ya kisiwa cha Guam.
P
....
...hahaha Pasco wa J4 Ngika
 
Uzuri hapa hata "wajeda" nao wataguswa pamoja na watu wa chama chake.

Ni swala la muda tu kila mtu atamchoka na wote tutaongea lugha moja.
.....
....Mkuu ukianza kubanguwa watoto wa kambo ipo siku utabanguwa WATOTOWAKO
 
Sio itafika sehemu...Imeshakua

Nimeshangaa sana wiki jana natoa kiwango kadhaa eti teller ananirudisha nikasainiwe na manager gani sijui

Upuuzi upo
Kwa mwendo huu itafika sehemu ukienda kuchukua Fedha hata milioni tatu tu ujaze fomu ya maombi wiki tatu kabla na uambatishe na mchanganuo wa matumizi wa fedha yote,

Kila leo unahubiri kuondoa urasimu wakati huo huo unaongeza urasmu zaidi ya ule uliokuwepo....!
 
Back
Top Bottom