Ongezeko la Wanawake (Mabinti) Wenye Vitambi (Obesity) Mtaani

Ongezeko la Wanawake (Mabinti) Wenye Vitambi (Obesity) Mtaani

Miq
Habari za Muda Ndungu Zangu,

Leo nijadili kuhusu Swala la Vitambi Kwa Wanawake. Naongelea Wanawake kwasababu nawajali na nawapenda.

Kumekua na Ongezeko Kubwa la Wanawake Wenye Ndambi Kubwa mtaaani Kila ninapokutana na Wanawake 10. Saba kati yao Wana Ndambi mpaka unaweza kudhani ni Mimba.

Mfano: Unene wa kupindukia nchini Afrika Kusini ni wa juu zaidi kwa wanawake kuliko wanaume. Kulingana na ripoti ya serikali iliyochapishwa mnamo 2019, karibu 41% ya wanawake na 11% ya wanaume wenye umri wa miaka 15 na zaidi walikuwa wanene. Je Leo hii Itakuaje?

Chanzo:
• Hali hii inatokana na Kula Chakula kingi, na Kushugulisha mwili Kidogo au pasipo kujishughulisha kabisa. Yaani unaingiza calories nyingi Kuliko unazochoma.

• Ulevi wa kupindukia, unakuta Mwanamke anakunywa Pombe mpka anakojoa Kitandani, anakunywa Pombe kama Vile amesikia kiwanda kinafungwa, hii sio Nzurii dada Zangu Punguzeni jameni.

• Kunywa vinywaji vya Sukari Sukari nyingi, mfano Soda, Juisi etc

• Junk Food , Hapa naongelea Vitu kama chipsi, mayai ya kisasa isikauke Sana, weka na Mayonaisi. Hii ni Hatari.

• Kutokufanya Mazoezi. Hii hupelekea Ishu Ya Uzito Mkubwa. Nakushauri ufanye Cardio Workout. Utakuja Kunishukuru Baadae.

Hatari za kiafya na matokeo
Kutokana na tafiti mbali mbali zinasema Kwamba Uzito Mkubwa unaweza kukuweka katika Hatari ya Shida Zufuatazo:

• Kupunguza Kunyonyesa, kwasababu ya Kujishtukia na maumbile Makubwa.
• Tatizo la Moyo.
• Ugonjwa Wa Kisukari.
• Ugumba
• Maumivu na Uharibifu wa Viungo.
• Sonona (Depression)
• Stroke
• Dementia
• Kansa (cervical, breast)

Nimejaribu kufupisha Kwa Kifupi na Kiswahili Rahisi ieleweke Kwa Wote....

Jinsi ya Kuzuia Unene
• Punguza Vyakula vya Sukari Sukari.
• Punguza kula Chips Kila Saa Saaa.
• Mboga Mboga na Matunda Kwa Wingi.
• Jitahidi Upige Zoez hasa Cardio Workout. Ingia YouTube Tafuta training Schedule uishi nayo. Walau Nusu Saa Kila Siku. Fanya Mazoezi hapo Hapo Ulipo Sio lazima Gym. Zingatia Sana Cardio Workout.
• Fanya kitu Kinaitwa intermittent fasting ( hii ni Kufunga kutokula Kwa Muda Flani.) Ingia Google utapata Maelekezo Zaidi na Zaidi. Uchague ambayo Mwili wako unakubali na unaendana nayo. Kama Uko na Obese Jitahidi Juu Chini Ratio ya Kula Iwe 23:1. Au 16:8 hizo ni Aina za intermittent fasting.

Aina ya intermittent fasting ninayopenda (Kufunga kula)
• 16:8 Hapa utafunga Masaa 16 na Kula ndani ya Masaa Nane. Mfano: Unakula kuanzia Saa 6 Mchana mpaka Saa Moja Jioni Dinner, ndio Mwisho Wa Kula Mpka Siku Inayofuata Saa 6 Mchana.

Aina Nyingine ya Kufunga Napenda. Kwa Kizungu Inaitwa 23:1 OMAD (One Meal A Day) Yaani Hapa utakula mlo Mmoja Kwa Siku. Mpka Siku Inayofuata. Ili Kufika Hapa Anza hyo ya 16:8 maana hii ya 23:1 Yahitaji Moyo. Pambana.
• Punguza Stress. Ukipiga Zoezi Kuna Namna Inapunguza Stress.
• Lala Vya Kutosha walau Masaa 7-9.
• Kunywa Maji ya Kutosha Walau ltr 3 na kuendelea..

Je utajuaje wewe ni Uko kwenye Kundi la Obesity?
Kuna kitu Kinaitwa BMI (Body Mass Index) ukiwa Juu ya 30. Wewe unakua kwenye Kundi obese. Wala Usishtuke ndio Maana Niko Hapa Kwa Ajili Yako.

Ingia google tafuta BMI Calculator. Piga Hesabu Uzito wako na Urefu Vinaendana kama Haviendani Chukua Hatua Mapema.

Hitimisho
Unene unazidi kuongezeka na una athari pana katika masuala mbalimbali ya afya ya wanawake. Madaktari wanapaswa kuwashauri wanawake wote kuhusu athari mbaya za unene na umuhimu wa kudhibiti uzito ili kuzuia matokeo mabaya.

Kila la Heri Dada Zangu.

"Don't Forget To Love 💕 Yourself"

Bob Lee Swagger


View attachment 2309021View attachment 2309022View attachment 2309023
Mianamike ya ckuiz Ni milafi na Tena milaji Sana,unakuta limwanamke linakula ugali mkubwa ambao unaweza liwa na wanaume wanne na wakashiba vizuri tu.
 
Vyakula vya wanga vingi bila zoezi inabadirisha na kuwa fat hivyo sehemu zote ambazo fat huhifadhiwa ndo inayoathirika

Ila wanakuwa naniii eeeee kunako naniiiieeee
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Hata wanaume ukiwa na kitambi kupitiliza sio poa, msituseme sisi Tu na nyie pia hili linawahuau
 
Hata wanaume ukiwa na kitambi kupitiliza sio poa, msituseme sisi Tu na nyie pia hili linawahuau
Wanawake hali ni mbaya zaidi.

Mnapoteza mvuto kabisa, mnaonekana wamama. Dogo wa 25 yrs anakua kama ana 40 yrs kisa ndambi na minyama uzembe kibao. Na bora awe mrefu sasa, hili janga huwapata sana wanawake wafupi.

Hakuna nguo itamkaa mwanamke mwenye ndambi ya kwenda, bora hata wanaume huvaa suti walau huonekana nadhifu hata kama ana kitambi.

Pia kwa mwanaume kitambi hakionekani akiwa na pesa, lakini mwanamke hata awe na pesa kiasi gani bado ataonekana mbovu na muonekano mbaya kisa ndambi.
 
Wanawake hali ni mbaya zaidi.

Mnapoteza mvuto kabisa, mnaonekana wamama. Dogo wa 25 yrs anakua kama ana 40 yrs kisa ndambi na minyama uzembe kibao. Na bora awe mrefu sasa, hili janga huwapata sana wanawake wafupi.

Hakuna nguo itamkaa mwanamke mwenye ndambi ya kwenda, bora hata wanaume huvaa suti walau huonekana nadhifu hata kama ana kitambi.

Pia kwa mwanaume kitambi hakionekani akiwa na pesa, lakini mwanamke hata awe na pesa kiasi gani bado ataonekana mbovu na muonekano mbaya kisa ndambi.
Basi sawaaa🤣🙌
 
Back
Top Bottom