Ongezeko la watoto wanaouza mifuko Sokoni ikiwamo Kariakoo linazidi kutia hofu

Ongezeko la watoto wanaouza mifuko Sokoni ikiwamo Kariakoo linazidi kutia hofu

Serikali tunailaumu Kwa kusababisha maisha magumu Kwa wazazi. Hakuna mzazi anaependa mtoto wake ateseke, asisome, awe chokoraa nk.
Lakini baadhi ya wazazi wanapitia changamoto wasizoweza kuzitatua mpaka wanaamua kukimbia familia.
Acha kutetea upumbavu wewe.
 
Ndo maana Tanzani ina wananchi wa aina ya ajabu.

Watoto wengi sana wanaacha shule wako mitaani. Kuanzia garage za magari, mama lishe, boda boda, machinga.

Panya road, na wahalifu. Wengi sana Tanzania na ni watoto kabisa.
Hii yote inatokana na watu kuzaa zaa hovyo kama mapanya ilhali hawana uwezo wa kuwahudumia hao watoto.

Nachukia sana mtu anayeleta kiumbe duniani halafu kulea hawezi.

Ingekuwa kuzaa ni mpaka uwe na uwezo wa kuhudumia, Hakuna mtu angezaliwa maskini.
 
Hali ni ngumu alaf hao wanaozurula mtaani hata wakikufateni muwape msaada mnawakataa alafu huku mnawaonea huruma
Mkuu, tunalia machozi ya mamba. Wakati mwingine tunashindwa kuwasaidia Kwa sababu na sisi tumebanwa kwenye angle Fulani Kwa kuwa na vipaumbele vya familia zetu.
Basi wakuu ambao mambo yenu ni mteremko mguswe kuwasaidia Hawa watoto, kuanzia wale walio jirani kabisa na ninyi..
Hii yote inatokana na watu kuzaa zaa hovyo kama mapanya ilhali hawana uwezo wa kuwahudumia hao watoto.

Nachukia sana mtu anayeleta kiumbe duniani halafu kulea hawezi.

Ingekuwa kuzaa ni mpaka uwe na uwezo wa kuhudumia, Hakuna mtu angezaliwa maskini.
Kuzaa ni mifumo ambayo Mungu alimwekea mwanadamu wakati wa uumbaji. Mwingine ana hustle anafika mpaka miaka arobaini hajatoboa, Sasa wataka asizae ili jamii imnyooshee vidole kwamba hajatimia kimaumbile?
 
Kama serikali inavyosema kila mara kuwa imejenga shule nyingi za kata na lengo kubwa ni kutaka watoto wa kitanzania wasome.

Lakini cha kushangaza ni kwamba watoto wengi sasa hivi wanauza mifuko Sokoni iwe shule zimefungwa au wakati wa masomo.

Waziri mwenye dhamana Dkt. Gwajima D tunaomba ulitazame hili na ulifuatilie ili watoto wote waende shule.

Inaelezwa kuwa watoto wengi wametoka mikoa tofauti tofauti na kwenda mikoa mingine kutafuta maisha kutokana na ugumu wa maisha katika familia zao.

Na watoto hao wanalala sehemu zisizo salama kwao na kufanyiwa vitendo vya kikatili.

Watoto ni taifa la kesho tusimamie usalama wao.
Wacha wajifunze katika hali hiyo, experience is a good teacher,mwisho wa siku akina Konde gang walipita humo na akina Frank knows na wengine wengi,plaese when it comes to human being tuache mengi, humo humo unaowasema kuna mtu atakuwa milionea na hakuna kumzuia na wengine wataaminiwa na kufungua matawi ya biashara
 
Mkuu, tunalia machozi ya mamba. Wakati mwingine tunashindwa kuwasaidia Kwa sababu na sisi tumebanwa kwenye angle Fulani Kwa kuwa na vipaumbele vya familia zetu.
Basi wakuu ambao mambo yenu ni mteremko mguswe kuwasaidia Hawa watoto, kuanzia wale walio jirani kabisa na ninyi..

Kuzaa ni mifumo ambayo Mungu alimwekea mwanadamu wakati wa uumbaji. Mwingine ana hustle anafika mpaka miaka arobaini hajatoboa, Sasa wataka asizae ili jamii imnyooshee vidole kwamba hajatimia kimaumbile?
Kama huna uwezo wa kulea na kuhudumia mtoto, Unazaa ukitegemea nani aje akusaidie majukumu?

Watu wa namna hii ndio mnaongeza idadi ya maskini duniani na watoto wa mitaani.
 
Kama huna uwezo wa kulea na kuhudumia mtoto, Unazaa ukitegemea nani aje akusaidie majukumu?

Watu wa namna hii ndio mnaongeza idadi ya maskini duniani na watoto wa mitaani.
Kwanini nisiwe na uwezo wa kuzaa na kulea watoto iwapo Kuna mifumo wezeshi?
Kukosekana na Kwa mifumo hii ndo kunakosababisha ongezeko la maskini na watoto wa mitaani.
Kila mtu ana haki ya kupata japo furaha kidogo ya kuwa na mtoto hata kama maeneo mwingine meengi atakosa furaha.
 
Kuzaa ni mifumo ambayo Mungu alimwekea mwanadamu wakati wa uumbaji. Mwingine ana hustle anafika mpaka miaka arobaini hajatoboa, Sasa wataka asizae ili jamii imnyooshee vidole kwamba hajatimia kimaumbile?
Haya ni mawazo ya hovyo, zaa kulingana na uwezo wako wa kuhudumia na kuhakikisha watoto watapata huduma zote muhimu na bora.
 
Kinachofanya familia zao ziwaeuhusu watumikishwe, na kinachofanya wao wakubali kutumika ni hicho alichoandika mkuu hapo juu, yaani kukosekana kwa uhakika wa chakula.
Hao wanachukuliwa mikoani mkuu kwa promise kedekede za uongo, it's more of education issue kuliko njaa.
 
Kwanini nisiwe na uwezo wa kuzaa na kulea watoto iwapo Kuna mifumo wezeshi?
Kwa hiyo kama hakuna mifumo wezeshi utazaa halafu utegemee hao watoto walelewe na nani?
Kukosekana na Kwa mifumo hii ndo kunakosababisha ongezeko la maskini na watoto wa mitaani.
Kila mtu ana haki ya kupata japo furaha kidogo ya kuwa na mtoto hata kama maeneo mwingine meengi atakosa furaha.
Nakuuliza hivi, 👇

Kama huna uwezo wa kuhudumia watoto, Unazaa ukitegemea nani aje akusaidie majukumu ya kulea?
 
Back
Top Bottom