Ongezeko la watu ambao hawana tabia ya utu ya kusalimia au kuitikia salamu

Pang Fung Mi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2022
Posts
6,653
Reaction score
13,919
Hello!!

Anaandika Wadiz a.k.a Baharia

Moja ya sifa na upekee wa binadamu ni utashi wa kusalimiana na kuitikia salamu.

Kumekuwapo ongezeko kubwa la ujeuri, dharau, kibri, vijana wa kiume, wa kike, baadhi yao wakubwa tu hawatoi salamu au kuitikia salamu iwe mnapishana njiani, akukute sehemu labda bar, dukani, kwenye bus, kwenye daladala.etc. Angalizo simaanishi kusalimia hovyo hovyo.

Dadadadeki kuna mfano videmu ukimsalimia haitikii salamu na hata hana tabia ya kusalimia, hakika salamu yangu isipoitikiwa natema mate na nihakikisha huyo mtu aone nikitema mate.

Ingalikuwa watu wanatilia maanani umuhimu wa salamu kama sehemu mojawapo kuu ya utashi wetu sisi binadamu maisha yangalikuwa yenye ubuheri sana.

Mungu wenu wa kanisani na misikitini ni yupi?, malezi na makuzi bora ya jamii ni yanapotea.🙄🙄

Je, tunaenda wapi kama jamii?

Wadiz.
 
Kuna jamaa aliagizwa kuja ofisini kwangu sababu ya tatizo alilokuwa nalo ambalo ningeweza kumsaidia.
Jamaa alipofika eneo la ofisi alikuta watu kadhaa nikiwemo na mimi. Alipita bila kusalimia yeyote na kwenda sehemu alipokuwa amekaa dada wa reception.
Alipofika akaulizia jina langu ndio dada kumjibu mbona umempita hapo nje.

Kimbembe ikawa kuja tena hapo nje na kuniulizia tena ikizingatiwa hakuwa ametoa salamu na alipita katikati yetu maana ilikuwa kama tumekaa kwa mistari 2 na kuacha uwazi katikati.

Mshkaji alirudi nje kinyonge sana na kuuliza mwenye jina langu ni nani hapo. Watu wote wakauchuna kama hawamsikii na hii ilichangiwa na kutosalimia hata aliporudi mara ya pili japo aliuliza kiupole.
Nilikuja kumjibu baadae baada ya yeye kumpigia simu mtu aliemulekeza kwangu ambae nae alinipigia kunambia mtu wake kafika.

Kabla ya kumshughulikia tatizo lake nilimchana kwanza ajifundishe ustaarabu.
 
Kuna jamaa aliagizwa kuja ofisini kwangu sababu ya tatizo alilokuwa nalo ambalo ningeweza kumsaidia.
Jamaa alipofika eneo la ofisi alikuta watu kadhaa nikiwemo na mimi. Alipita bila kusalimia yeyote na kwenda sehemu ilipokuwa amekaa dada wa reception.
Alipofika akaulizia jina langu ndio dada kumjibu mbona umempita hapo nje.

Kimbembe ikawa kuja tena hapo nje na kuniulizia tena ikizingatiwa hakuwa ametoa salamu na alipita katikati yetu maana ilikuwa kama tumekaa kwa mistari 2 na kuacha uwazi katikati.

Mshkaji alirudi nje kinyonge sana na kuuliza mwenye jina langu ni nani hapo. Watu wote wakauchuna kama hawamsikii na hii ilichangiwa na kutosalimia hata aliporudi mara ya pili japo aliuliza kiupole.
Nilikuja kumjibu baadae baada ya kupiga simu kwa aliemulekeza ambae alinipigia na mimi.

Kabla ya kumshughulikia tatizo lake nilimchana kwanza ajifundishe ustaarabu.
safi sana!
 
Hello!!

Anaandika Wadiz a.k.a Baharia

Moja ya sifa na upekee wa binadamu ni utashi wa kusalimiana na kuitikia salamu.

Kumekuwapo ongezeko kubwa la ujeuri, dharau, kibri, vijana wa kiume, wa kike, baadhi yao wakubwa tu hawatoi salamu au kuitikia salamu iwe mnapishana njiani, akukute sehemu labda bar, dukani, kwenye bus, kwenye daladala.etc. Angalizo simaanishi kusalimia hovyo hovyo.

Dadadadeki kuna mfano videmu ukimsalimia haitikii salamu na hata hana tabia ya kusalimia, hakika salamu yangu isipoitikiwa natema mate na nihakikisha huyo mtu aone nikitema mate.

Ingalikuwa watu wanatilia maanani umuhimu wa salamu kama sehemu mojawapo kuu ya utashi wetu sisi binadamu maisha yangalikuwa yenye ubuheri sana.

Mungu wenu wa kanisani na misikitini ni yupi?, malezi na makuzi bora ya jamii ni yanapotea.[emoji849][emoji849]

Je, tunaenda wapi kama jamii?

Wadiz.
Unalazimishaje salamu kwa mtu ambaye humjui na wewe hakujui?

Wewe una matatizo gani ya kisikolojia ya kutaka salamu, urafiki na kujuana na kila mtu?

Kwani kusalimiana lazima?
 
Hivi salamu ni lazima?
Si ndo hapo unashangaa sasa?

Mimi hata kama mtu kanipita hajanisalimia, kaenda kuongea na receptionist, akaambiwa unayemtafuta yule pale umempita, akarudi akanisalimia, siwezi kuona issue.

Kwa sababu sitegemei kusalimiwa na kila mtu ninayekutana naye.

Kwanza itakuwa usumbufu hata kwangu kusalimiwa na kila mtu ninayekutana naye.

Can you imagine umekaa sehemu unafanya mambo yako halafu kila anayepita anakusalimia na anategemea umrudishie salamu?

Ni usumbufu wa kujipa umuhimu usio nao kwenye maisha ya watu baki tu.
 
Mimi sema ukweli salamu hua sipendi, kwanza ni kupoteza muda tu
 
Acheni ujinga. Salimia watu Kwa kuwapungia mkono, salama wakubwa, habari zenu au kwema hapo!!!
 
Back
Top Bottom