Ongezeko la watu ambao hawana tabia ya utu ya kusalimia au kuitikia salamu

Safi uzi nimeupenda huu.Mimi huwa napenda sana kusalimia na huwa sijisikii vizuri kuwapita watu/mtu bila kumsalimia,lkn kuna watu wanakera sana unawasalimia lkn wao hawajibu salamu au wanakupita tu km kisiki.Tabia mbaya sana hiyo.
 
Mjini utasalimia wangapi, utachoka bure. Nina uhakika hata wewe uliyeandika hufanyi hicho kitu otherwise unaishi kijijini au pembezoni mwa mji au Jiji ulilopo. Lakini chukulia sehemu Kama Dar kusalimia Kila unayepishana nae. Huwezi hicho kitu.
 
Tatizo unataka kuishi maisha ya kijijini kwenu mjini. Mjini wanasalimiana watu wanaofahamiana tu.
 
Hiyo ni ofisi au kijiwe mnakaa nje kupiga hadithi
 
Mpaka nikasema hii Dar, kusalimia watu njiani ni kusumbua akili yako tu, unakuta kundi la watu unawasalimia hawaitkii, ukiwa na bahati anaitika mmoja tu.

Wakupishana nao ndiyo kabisa, Mpaka unajiuliza kwani una shida gani lwao, unaamia kupishana bila kusalimiana nao, hapa naongelea maeneo yasiyo na pilika, maana kwenye pilika utasalimia wangapi.
 
Mimi sema ukweli salamu hua sipendi, kwanza ni kupoteza muda tu
Wabongo wengi wana tabia za kuweka vipaumbele kwenye mambo yasiyo na umuhimu, wakati mambo ya muhimu hawaweki vipaumbele.

Kwa mfano, unaweza kuwa jambazi unayevaa suti, ukawaibia vizuri sana wabongo, kwa sababu wana tabia ya kuheshimu watu wanaovaa suti. Na unaweza kuwa mtu safi kabisa wa msaada sana, lakini ukapingwa sana hata kuingia ofisini, kwa sababu umevaa jeans iliyochanikachanika.

Watu wengi ni very shallow katika kuangalia mambo ya msingi. Wanafuata formula za kizamanizamani katika dunia inayobadilika kwa kasi sana.

Hapo ndipo unapata hizi habari za kulazimishana kusalimiana na watu ambao huwajui na wao hawakujui mmekutana barabarani tu.

Mtu anaweka msisitizo kwenye kusalimiana na watu asiowajua, ukimuuliza kama anaelewa soko la hisa linavyofanya kazi na "angel investors" ni kitu gani, jibu mara nyingi ni mgogoro.

Atapata wapi muda wa kufuatilia soko la hisa wakati muda wote anataka kusalimiana na watu asiowajua?
 
Huyo alikuwa hamnazo kabisa. Suala la kusema tu HABARI ZENU JAMANI wakati anapita alionao gumu. Hakukuwa na haja ya kuvaa miwani ya mbao Ilhali anahitaji msaada kwenye ofisi za watu
 
Mimi nikisalimia kikundi Cha watu huwa nafanya marking.. usipoitikia sahau kukusalimia tena. Kuna wamama niliwahi kuwasalimu, ni rafiki zake mama.. walikuwa watu, wawili waliitikia mmoja hakurespond na nilisalimu kwa sauti ya kusikika kabisa.. Hadi Leo, hata kesho na hata milele, sijawahi, sitowahi na haitokaa itokee nikamsalimia hata tukikutana face to face, hata niende home nimkute..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…