fimboyaukwaju
JF-Expert Member
- Aug 3, 2020
- 2,977
- 3,798
Najaribu kukata tiketi kwa njia ya mtandao lakini sifanikiwi, mfumo haufanyi kazi, nifanyeje?
Pia soma: TRC: Tumewakamata Watu kadhaa waliokuwa wanafanya ulanguzi wa tiketi za SGR na kufanya udanganyifu
Habari wadau. Kumekuwa na changamoto kubwa hasa kwenye ukataji wa ticket online. Suala hili limekuwa linaenda kimya kimya bila kutolewa ufafanuzi. Sifahamu hili linatokea by coincidence au limepangwa. Kama train imejaa ni kwanini mfumo hausemi kwamba train imejaa kama ilivyo mifumo mingine ya ukataji ticket? Limebakia suala la Sisi abiria kujipa majibu wenyewe kwamba huenda train imejaa ndio maana mfumo inasumbua.
Tunaomba uongozi walifanyie kazi hili suala Kwa haraka na weledi ili raia tuweze pata huduma stahiki.
Pia soma: TRC: Tumewakamata Watu kadhaa waliokuwa wanafanya ulanguzi wa tiketi za SGR na kufanya udanganyifu