Katika muendelezo wa kuzinyanyasa nchi za Afrika kupitia mahakama zao za kibeberu.
Mahakama nchini Canada imeyakataa madai ya watanzania 21 dhidi ya kampuni ya madini ya Barrik kutokana na vitendo vya mauaji ambavyo watanzania hao wamedai vikihusishwa na kampuni hiyo.
Mahakama hiyo imeyakataa madai hayo kwa kudai kuwa haina mamlaka ya kusikiliza madai ya aina hiyo.
Hili ni jambo la kusikitisha mno kwani imekuwa ni kawaida kwa mahakama za nchini Canada kutoa hukumu dhidi ya nchi yetu kwa madai ya aina yeyote ile yatayofunguliwa.