Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 60,050
- 104,466
Mbona unaandika vitu usivyovijuwa kama mlevi wa Chimpumu?Narudia tena dada yangu kama mwaka jana uliweza kugundua mapema una mole msukule ndani ya team ukamkataa na aka force kwa nauli za maadui zetu kwenda south africa na kulala kwenye coach basi jua safari hii mziki utakuwa mkubwa sana
Niko chini ya miguu yenu uongozi wa simba, hawa wanaoitwa waandishi kuweni nao makini sana wawekeni mbali na wachezaji huko south africa najua watakuja wengi sana na lengo ila asilimia 99 yao ni nyie mpigwe goli za kutosha SIYO MARAFIKI ZETU KABISA
Msirudie lile kosa la mwaka jana kushoboka na wanaoitwa watanzania waishio south africa..maisha kule magumu na watu wana roho ngumu sana kupata maelekezo yoyote ya mtu kufanya kwa wachezaji kwa kigezo cha kukumbatian na kusalimiana watu hawashindwi nyie mkijua ni watanzania wenzenu
Ikiwezekana muingie usiku siku mbili kabla ya mechi kama orlando na mazoezi yafanyika uwanja wao siku moja kabla ya mechi msiwe na open session kama mwaka jana vs kaizer chiefs
Msisahau kubeba mtu wa uchawi (Muthi) maana jamaa wako vizuri kwa hilo
Kabala ya mechi watingisheni kwamba mmehisi kuna sumu vyumbani lalamikeni kwa kamisaa kuwatoa mchezoni siyo mnaonewa kama moroko mnakuwa kama makondoo
Msisahau kuweka watu wawili kulinda vyumba
Hii ngoma ngumu tenga fungu la maana Abbas gaza atafute hata watu wa kaizer chiefs wampe ujanja hata njia ya kwenda uwanjani siku hiyo ikiwezekana mbadili njia ya kwenda uwanjani na muwahi muda wa kutoka hotelini
Uwanja upo Soweto, najuwa kwa vyovyote Simba itafikia hotel za Rose bank au au Sandton city hii ni miji ya uzunguni, sasa utaruka wapi kutoka sehemu hizo kwenda Soweto ulipo uwanja?
Ongelea kuhusu ufundi kama ni mambo ya sangoma wale ndio wenyewe na usisahau hii ni timu ya Wazulu wenyewe na tickets zimeanza kuuzwa, hii siyo habari njema kabisa kwa Simba, mechi na Kaizer haikuwa na mashabiki ila mechi hii serikali yao imeruhusu mashabiki.