Kitchener
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 13,833
- 27,753
Chezea vitu vyooote, ila usichezee haki ya kikatiba ya kuabudu. kama padre mmoja amefanya kosa, ashughulikiwe yeye, lisishughulikiwe katholic lote na makanisa yake nchi nzima, kama TAG au lutheran kuna mchungaji au hata mkuu wao amekosea, mshughulikieni yeye, waumini wake hawana kosa kwa sababu hawamwabudu yeye, wanamwabudu Mungu, kufunga makanisa yote ya kundi hilo wakati mkosaji ni mmoja tu, waumini wana kosa gani sasa?
Waumini wakasali wapi sasa? kwanini waumini wanaadhibiwa kwa kosa la mtu mmoja? muumini aliyeop mwanza hajawahi hata kufika dsm anaadhibiwaje kwa kuambiwa asisali kwenye kanisa lake kwa sababu kiongozi wake aliyepo dsm amekosea? kwanini usiadhibu mtu binafsi badala yake unaadhibu hata innocent na kunyima watu haki ya kuabudu?
Tangu lini nchi hii imeanza kufuta usajili wa makanisa? je, kutakuwa na kushughulikia misikiti pia? naomba isiwe hivyo, kama kuna shehe mmoja amekosea ashughulikiwe yeye wasiumizwe na waumini/members wake, natural justice ipo wapi kwamba mimi niadhibiwe kwa kosa la mtu mwingine? ninyimwe kuabudu kwa sababu muumini au askofu wangu amefanya kosa? kwanini msishughulike na askofu wangu mkaumiza sisi waumini tusio na kosa?