Onyo: serikali heshimu haki ya kuabudu ya raia wako

nimefurahi UFUFUO NA UZIMA wametoa maelekezo waumini wao wasiende kwenye majengo yao waliyopigwa stop kesho kusali, hii inaonyesha hawataki fujo, hawataki kupingana na serikali, wanataka kufuata utaratibu.

WAABUDUJE SASA, NA HAKI YA KUABUDU WAMEZUIWA AMBAYO NI KIKATIBA?
Ninashauri usishindane na serikali, fanya ibada nyumbani kwako. HOW? fanyeni ibada kwa njia ya mtandao, bado unaweza kuwa na wafuasi kwa njia ya mtandao. Tengeneza mahubiri, sambaza kwa njia ya mtandao, kuna x (ambayo wameifungia ila inapatikana kwa VPN.), instagram, facebook na whatsapp, waumini sambazieneni mahubiri kwa whatsapp, facebook, twitter x na instagram. kwa njia hiyo mnaweza kufikia waumini wengi kuliko hata wale ambao wangefika kwenye majengo waliyowapiga stop msikusanyike.

WATAFUNGIA MITANDAO, ila hawatafungia yote, hivyo haki yenu ya kuabudu bado itakuwa excercised tu hata kama in a limited way. Gwajima popote ulipo kesho toa mahubiri yasambae kwa waumini wako na kwa dunia nzima, ila yawe ya amani sio ya fujo. hapo hautakuwa umevunja sheria, kwa sababu hata kama wamefuta kanisa lako, ila hawajakuzuia kuhubiri mtandaoni.

MWISHO
: Lindeni brand ya Yesu, msifanye fujo, Mtu aliyeokoka huwa hafanyi fujo, huwa anapiga maombi rohoni Mungu aamue. hivo msopigane kimwili, msilazimishe mambo kimwili, msifanye fujo, mtachafua Jina la Yesu, lindeni brand ya Jina la Yesu ambaye hapendi fujo. Mungu awabariki.
 
Online republic
Kiburi chako ni kitu kidogo sana, mnatuonea kwa sababu ninyi mna mabunduki, mna mapolisi, mna jeshi, mna pingu, na pamoja na kwamba mnaamini sisi raia ndio waoga, ila ukweli wewe na wenzako ndio waoga kupita wote, ndio maana hamuwezi kumdhuru raia mwema hadi mummfunge pingu, mumteke hadi mbali ambapo mtahakikisha usalama wenu upo, yeye yuko peke yake na ninyi wengi na mna silaha yeye hana. hapo mwoga nani kama sio ninyi?

pili, namwomba Mungu akishushe kiburi chako hadi chini, you believe I am an online republic au online warrior, sawa, ila yupo Mungu hakimu wa wote, yeye hutenda kwa haki, haki ya kaa ndani yake, na akiwa mbinguni huangalia wapi haki inavunjwa ili ashuke kuwatetea victims wa haki. Huyo ndiye atapambana na wewe, na ndiye atakishusha kiburi chako kwa Jina la Yesu. Mnaamini nchi hii ni yakwenu peke yenu, mnaweza kufanya chochote kwa yeyote, bila kujua utendaji wenu una limit, kuna wengine hauwezi kuwagusa, ukigusa tu unakuwa umegusa mboni ya Jicho la Mungu, na Mungu lazima shuke kutetea. Mungu na ashughulike na wewe ili kuwaokoa hao unaowaharibia haki zao hadi unapata kiburi kwamba wale wanaotetea haki ni wa online tu. Ikiwa mimi ni mtumishi wa Mungu, basi kiburi chako kishushwe hadi kuzimu na wale wote mnaowaonea wakombolewe kwa Jina la Yesu.
 
Nisikilize Kwa makini nyumbu

Siko bongo na huna cha kunifanya…. Na kama ni imani ninayo njema sana and I bet you TRY ME!!! Miki ni mkatoliki, siyo hayo madhehebu yako ya wachungaji kukaza waumini na kujirekodi

Huna hoja zaidi na sonona

Hujawahi kujiuliza why makanisa na misikiti vinasajiliwa na serikali? Basics za Yesu zilikuambia nini kuhusu kaizari na Mungu?

Pumbaf wahed
 
mkiuka misingi ya kuabudu kwa mujibu wa sheria, yeye na kanisa lake watawajibishwa na watafutiliwa mbali bila kuchelewa hata sekunde moja.

waambie na wengine wenye makanisa binafsi nchini kama huyo askofu mzinifu 🐒
Vipi, mbona misikiti haifungwi, maana na penyewe siasa tunazisikia kila siku
 
sina cha kukufanya, but if you think you are on the right side, then God will decide, tumekukabidhi kwa Mungu ahukumu. Nakuhakikishia kuna siku utajua kama ulikuwa sahihi au la. Pia, uwe nchini au usiwe nchini sina la kukufanya, hata ungekuwa mbele yangu hapa siwezi kukufanya kitu, siwezi kukupiga hata kibao tu kwa sababu pengine hata ningekuja kimwili ungekuwa na nguvu ziadi yangu, ndio maana umekabidhiwa kwa Mungu atoe haki kulingana na matamshi yako na uyafanyayo. Pia, mimi sio nyumbu, trust me, mimi sio mwanachadema, wala sina chama, ina mlengo wangu ni kwenye haki. cha muhimu elewa tu kwamba, APANDACHO MTU NDICHO ATAKACHOVUNA, ukipanda kwa uharibiru utavuna uharibifu, ukitetea uovu kuna siku uovu wa aina hiyo hiyo iwe hapa nchini au huko uliko utakurudia tu, hii ndio sheria ya maisha na ndio haki ya Mungu ilivyo;, na mwisho moto wa milele au uzima wa milele.

Kuna mtu alipenda sana kushabikia wenzie wanapoonewa, kwa sababu yeye hakuwa kwenye nchi ile, kule aliko yalimkuta yale yale ya kupunjwa haki, akaumia moyo sawasawa na wale aliowaonea. sikuombei hayo, Mungu akusaidie. mwingine aliamini kwa pesa alizo nazo, kwa eneo alilopo, kwa watu waliomzunguka, hakuna baya litampata, Nebukadreza alikuwa mfalme, pesa, watu, majeshi n.k anayo, Mungu mwenyewe alishuka akavunja kiburi chake, akala manyasi miaka 7 kama ng'ombe hadi alipokuwa humble. wewe unaweza kuwa mtoto wa rais, mtoto wa waziri, mtoto wa fisadi fulani wa ccm, au mpambanaji tu aliyefanikiwa kwa jasho lake anayeamini kwa alivyo hakuna baya litampata na ana kiburi mno, JUA MUNGU HAPENDI KIBURI CHAKO,shuka, jinyenyekeshe,

nasema hivi kwa sababu, kuna wamama wamelia machozi mengi, watoto wamelia machozi mengi, familia zimeumia moyo na kulia machozi, KWA SABABU NDUGU ZAO WAMETEKWA NA KUUAWA. na wewe unatetea watekaji na wauaji, zaidi sana, unatetea KANISA KUFUNGWA, labda kwa sababu wewe sio muumini wa kanisa hilo au imani hiyo. jua kuwa, kama katiba ya hawa imevunjwa na wewe umeshabikia, kuna siku katiba itavunjwa na upande wako utapunjwa pia, ili ujue kuwa anayetawala ni Mungu, sio sisisemu, sio samia wala yeyote. katiba ya mwili wako au uhai wako inaweza kutikiswa pia, ili ujue atawalaye ni mmoja, naye ni wa haki, na anapenda tusambaze haki sio dhurma.

nakushauri, penda haki kuliko mauaji, utekaji na dhurma. Mungu ni Mungu wa haki.

WAGALATIA 6:7-9: Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele. Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho.

MIKA 6:8 6 Nimkaribie BWANA na kitu gani, na kuinama mbele za Mungu aliye juu? Je! Nimkaribie na sadaka za kuteketezwa, na ndama za umri wa mwaka mmoja? 7Je! BWANA atapendezwa na elfu za kondoo waume, au na elfu kumi za mito ya mafuta? Je! Nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa kosa langu, mzao wa mwili wangu kwa dhambi ya roho yangu? 8Ee mwanadamu, yeye amekuonyesha yaliyo mema; na BWANA anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!
 
Kagame kafunga mabanda yenu ya kuku meeengi sana huko Rwanda
 
Hapo ndo linapokuja suala la udini kwa sababu unadhani dini ya mwenzio inashikiriwa na mtu na ya kwako inashikiriwa na Mungu. Tuheshimu dini za watu jamani, haiwezekani ukawafungia watu wa Mbeya au Mwanza sehemu ya kuabudia kwa sababu tu askofu wao aliyeko Dar es salaam amegombana na serikali.
Kuna watu wanakuja na hoja ya kuwa makanisa ya kilokole yanamilikiwa na mtu mmoja ndio maana kiongozi anapofanya kosa yanafungwa. Huo ni uhayawani wa juu sana katika kuangalia dini ya mtu mwingine. Yaani wewe ndo unauwezo wa kupima Uungu wa kanisa fulani! Mkristo anayesupport kufungiwa kwa kanisa la ufufuo na uzima eti kwa sababu ya Gwajima ajitafakari mara mbili juu ya kumkili Yesu kwamba ni Mungu na Mwokozi wake.
Naweza kuona logic ya kulifungia kanisa kama miongozo na mafundidho yake yanapingana ustawi wa nchi lakini sio kwa matamshi ya muumini mmoja ndani ya kanisa.
 
Umeandika maneno meengi ila hujui nimekua victim wa nini

Katishe wale unaoweza kuwatisha….. lakini sio mimi

I live my battles, I don’t fight them anymore

Muache unafiq wa kujitakasa Kwa kushtakia watu Kwa Mungu mnapowekwa sehemu yenu

Nyambafff
 
asante bro.
 
Makanisa ya Walokole yanamirikiwa na hao maaskofu hata usajiri wake ni wa individual siyo kama KKKT, RC, Anglican, AIC n.k. Hivyo kanisa la Ufufuo ni mali ya Josephat Gwajima na wala si waumini.
Na wewe fungua lako alafu JIFUNZE kutofautisha r na l, eti udsm leaver
 
Shetani anatumia udhaifu wa umoja wa wakristo/makanisa ili afanikishe hujuma zake.
 
Mkuu kasajiri kanisa lako na wewe lililofungiwa ni la Gwajima amesajiri kama kanisa lake na kuna masharti ya kusajiri kanisa ndio maana Gwajima yuko kimya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…